Vimbunga vya Kentucky : Idadi ya waliofarioki kupita watu 100,gavana asema

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Idadi ya vifo kutokana na vimbunga vikali vilivyoharibu miji ya Kentucky huenda ikapita 100, gavana wa jimbo hilo anasema, huku matumaini ya kupata manusura yakipungua.

Andy Beshear alisema hili lilikuwa tukio baya zaidi la kimbunga katika historia ya jimbo hilo, na vifo vya angalau 80 vimethibitishwa.

"Hakuna kitu ambacho kilikuwa kimesimama kwenye mstari kimbunga ambacho bado kimesimama," alisema.

Vifo 14 vimeripotiwa katika majimbo mengine manne.

Huko Kentucky, wafanyikazi wa uokoaji walichakura vifusi kuwasaka walionusurika huku timu zikisambaza maji na jenereta kwa wakaazi. Zaidi ya wanachama 300 wa vikozi vya National Guard walikuwa wakienda nyumba kwa nyumba na kuondoa vifusi.

"Bado tunatumai tunaposonga mbele kwa miujiza mingine kupata watu zaidi," gavana huyo alisema wakati wa ziara yake katika mji wa Mayfield, mmoja wapo ya maeneo yalioathiriwa vibaya zaidi.

Walakini, hakuna mtu aliyepatikana akiwa hai tangu Jumamosi asubuhi.

Bw Beshear alisema kimbunga kilikuwa kimeharibu maeneo yote kwenye njia yake ya maili 227 (365km). Maelfu ya watu waliharibiwa nyumba zao ingawa idadi kamili bado haijafahamika.

Hapo awali, kimbunga kirefu zaidi kilikuwa kimesafiri ardhini nchini Marekani kwa dhoruba ya maili 219 huko Missouri mnamo Machi 1925 ambayo ilisababisha maisha ya watu 695. Matukio makubwa kama haya nje ya miezi ya majira ya joto ni nadra sana.

Huko Mayfield, kituo cha zima moto na ukumbi wa jiji viliwekwa viliangushwa. "Sidhani kama kuna kioo katika gari au mali yoyote ambayo jiji inamiliki ambayo haijavunjwa," Meya Kathy Stewart alisema.

Vifo vinane vilithibitishwa kwenye kiwanda cha mishumaa ambacho kiligongwa wakati wafanyikazi 110 waliaminika kuwa ndani, msemaji wa kampuni hiyo aliambia shirika la habari la Reuters. Watu wengine wanane bado hawajulikani waliko

Kyanna Parsons Perez, mfanyakazi wa kiwandani ambaye aliomba msaada kwenye Facebook kutoka chini ya mabaki hayo, aliambia BBC kwamba biashara nyingine zilifungwa kutokana na dhoruba hiyo na wafanyakazi hawakupaswa kuwa kazini.

Gavana Beshear alisema aliuliza utawala wa Biden kutangaza janga kuu la serikali katika jimbo hilo, uboreshaji kutoka kwa jina la dharura la sasa. Hatua hiyo ingefungua pesa za ziada za urejeshaji kutoka kwa serikali kuu

Huko Illinois, watu sita waliuawa katika ghala la Amazon lililoporomoka huko Edwardsville na wengine bado hawakupatikana.

Vifo vinne vilithibitishwa huko Tennessee huku watu wawili wakiuawa huko Arkansas, mmoja wao katika nyumba ya wazee baada ya kuporomoka kwa sehemu ya jengo . Kifo kimoja kilithibitishwa huko Missouri.

Rais Joe Biden alisema atauliza Shirika la Ulinzi wa Mazingira kuchunguza ni jukumu gani mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuwa katika kusabaisha dhoruba hiyo kali.