Mauaji ya Sir David Amess yalikuwa ugaidi, polisi wanasema

Sir David Amess

Chanzo cha picha, Rex/Shutterstock

Mauaji ya mbunge wa chama cha conservative nchini uingereza Sir David yanachukuliwa kama kitendo cha ugaidi. Sir David Amess alichomwa kisu katika eneo bunge lake huko Essex siku ya Ijumaa.

Polisi walisema kuna uwezekano wa tukio hilo kuhusishwa na msimamo mkali wa Kiislam.

Polisi walisema mwanamume mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa kwa tuhuma za mauaji baada ya shambulio hilo katika kanisa huko Leigh-on-Sea.

Kama sehemu ya uchunguzi, maaafisa wanapekua maeneo mawili ya makazi mjini London, polisi ilisema.

Maafisa wanaamini mwanamume huyo alitekeleza mauaji hayo peke yake lakini uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea. Manamume huyo anazuiliwa mjini Essex, poliai iliongeza.

Vyanzo vya serikali vimeambia BBC kuwa ni raia wa Uingereza, kutokana na uchunguzi wa awali, anaonekana kuwa wa asili ya Somali.

Sir David, 69, ambaye alikuwa anawakilisha eneobunge la Southend West, alikuwa akikutana na watu wa eneo lake -ambapo wapiga kura wanakutana na mbunge na kujadili masuala yanayohitaji kushughulikiwa - katik akanisa la Belfairs Methodist siku ya Ijumaa wakati aliposhambuliwa.

Mkuu wa Polisi wa Essex Konstebo BJ Harrington alisema Sir David alikuwa "akitekeleza majukumu yake wakati maisha yake yalipokatizwa vibaya".

Polisi wa kukabiliana na ugaidi wanashirikiana na polisi wa Essex na kitengo cha eneo la mashariki cha oparesheni maalum.

"Tukio la Leigh-on-Sea limetajwa kuwa kitendo cha ugaidi, na uchunguzi unaongozwa na polisi wa kukabiliana na ugaidi," the Polisi ilisema.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa motisha inayoweza kuhusishwa na msimamo mkali wa Kidini."

Maafisa wanaomba kwa mtu yeyote aliye na habari yoyote au na picha kutoka kwa kamera ya CCTV, au video ya kengele ya mlangoo, kuwasiliana nao

'Shambulio lisilo na maana'

Waziri wa mambo ya ndani Priti Patel ameomba vikosi vya polisi kukagua mara moja mipango ya usalama ya wabunge, akisema mauaji hayo yanawakilisha "shambulio lisilo na maana kwa demokrasia yenyewe".

Aliongeza kuwa "maswali yanaulizwa kwa usahihi juu ya usalama wa wawakilishi wa nchi yetu waliochaguliwa".

Sir David ni mbunge wa pili kuuawa akiwa bado anahudumu katika miaka mitano iliyopita, kufuatia mauaji ya Mbunge wa Kazi Jo Cox mnamo 2016.

Waziri Mkuu Boris Johnson alimtaja kama "mmoja wa watu wazuri zaidi, na mtulivu i katika siasa".

line
Floral tributes have been left at the scene of the stabbing

Chanzo cha picha, TOLGA AKMEN

Maelezo ya picha, Watu waliweka maua katika eneo la tukio kwa heshima ya marehemu
Two women gather their thoughts at a church before lighting a candle for Sir David Amess

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ruth Verrinder (kulia) na kansela wa zamani na meya mayor Judith McMahon (kushoto) walikuwa kanisa la St Michael and All Angels kuwasha mshumaa
Map showing the location of the killing of Sir David Amess