"Kuna tofauti ndogo ya uraibu wa simu na dawa za kulevya"

Marc Masip.

Chanzo cha picha, Marc Masip

Maelezo ya picha, Mwansaikoloji kutoka Hispania Marc Masip anafanya kazi na vijana kuwaelemisha kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia ili kuepuka uraibu.

Ikiwa una wasiwasi ukifikiria kwamba itakuwaje kama hakutakua na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram au WhastApp ulimwenguni basi angalia utegemezi wako kwenye teknolojia mpya, kuna uwezekano mkubwa ukawa umeathirika na uraibu wa teknolojia hii.

Jaribio hili limekwishafanyika Oktoba 4 mwaka huu, wakati mamilioni ya watu walipogadhabishwa wakati huduma za mitandao hii ilipokuwa haipatikani kwa muda wa saa sita tu. Kufadhaika huku ni mifano yake, kuna wale ambao wanathubutu kufananisha kama kile kitendo cha kujiondoa kwenye uraibu wa dawa za kulevya, pombe au sigara. Inaweza kuonekana kama mfano uliongezwa chumvi, lakini mwanasaikolojia wa Hispania Marc Masip anatetea hili kwa hali zote, katika mahojiano yake na BBC.

"Simu ya mkononi ni heroine (daya ya kulevya) ya karne ya 21, " anasema. 'tulipokosoa huduma za Facebook, WhatsApp na Instagram, uliona watu walivyochanganyikiwa, ni kwa sababu tumevipa umuhimu sana'.

Mwanasaikolojia huyu anasema uraibu ni uraibu tu, na hakuna tofauti kubwa kati ya uraibu wa dawa za kulevya na uraibu wa simu ya mkononi

'Ni kweli kwamba dawa za kulevya hazina matumizi mazuri na simu zina matumizi mazuri, hiyo ni faida'. 'Bila kusahau, baadhi ya watu wanavyoumizwa na visa vya kushambuliwa na kutukanwa mitandaoni, kuna madhara yanayosababishwa na afya ya akili ambayo bado hatuyalewi na yanayotokana na kutumiwa vibaya kwa simu za mkononi'.

Marc Masip

Chanzo cha picha, Desconecta

Maelezo ya picha, Marc Masip anajaribu kuwaelimisha upya vijana kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia mpya.

Nini madhara ya uraibu wa teknolojia?

Marc Masip anasema yako matokeo mawili unapotumia dawa za kulevya kwa mfano heroin: kifo kutokana na kutumia kiwango kikubwa kupita kiasi au kupelekwa kwenye kliniki maalumu ya kuondoa sumu mwilini. Je nini kuhusu uraibu wa teknolojia?

'uraibu wa teknolojia pia unaweza kusababisha tatizo kubwa la afya ya akili na hata wakati mwingine matatizo ya afya ya mwili. Inashuhudiwa uwepo wa matokeo mabaya darasani kwa vijana, ajali za barabarani, wasiwasi, mfadhaiko, kuchanganyikiwa, matatizo ya kula yanayosababishwa na mtandao kama Instagram na aina ya picha zinazowekwa. Wakati mwingine ajali zinatokea kwa mtu kuendesha gari huku akiendelea kufuatili ya kwenye mtandao, ama mtu akagongwa kwa sababu ya matumizi ya simu barabarani', anasema Masip.

Nini kinafanyika kwenye kliniki za kuondoa uraibu huu?

Kwa mujibu wa mwanasaikolojia Marc Masip, vijana wenye uraibu wa teknolojia wanapewa elimu ya kutumia vizuri simu zao. Ni jukumu kubwa.

'Jaribu kufikiria, ukiwa unatibu uraibu wa heroin, cocaine ama bangi, ambavyo kuna sehemu nyingi haziruhusiwi, kwa sababu watu wanaamini uvutaji na unywaji wa kupindukia ni mbaya'.

'Lakini kwa upande wa teknolojia, ni ngumu zaidi, kwa sababu sio suala la kuzuia kutumia, jambo linalofanywa ni kuwaelemisha upya namna bora ya kutumia teknolojia. Ni ngumu kwa sababu matumizi yanafana karibu kwa kila anayekuzunguka'.

Foto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Utegemezi ni kinyume kabisa cha uhuru."

Itakuwaje ikiwa teknolojia inakuwa kwa kasi na kuiunganisha dunia?

Marc Masip anasema 'ni kweli teknolojia inakuwa kwa kasi, lakini tunahitaji kutambua kwamba haijalishi kwa kiasi gani wanatengeneza teknolojia na kiasi gani wanawekeza kwenye teknolojia, hakuna ambaye atakupongeza au kuja kukubusu kama mtu anayempenda'.

'Naamini kwamba kwa kuelemisha vijana tutarudi nyuma kidogo kwneye teknolojia. Fikiria kwmaba tuna teknolojia nyingi. Lakini lazima kuwe na mipaka.'

Marc Masip.

Chanzo cha picha, Marc Masip

Maelezo ya picha, Masip pia haungi mkono matumizi ya simu kwa watoto walio na umri chini ya miaka 16.

Kuna mbinu inayoweza kusaidia mtu kujitambua kiwango chake cha uraibu?

Marc Masip anasema 'hilo ni jambo tata na gumu. Mtu anapaswa kusaidiwa, lakini sio rahisi. Naweza kukupa vitu vitakavyokusaidia kutambua utegemezi ama uraibu wako wa teknoklojia.'

'La kwanza, jipime kama unaweza kujitoa. Pili angalia shughuli mbadala unazoweza kufanya. Inawezekana, jaribu kutumia muda na familia , tembea, endesha, shiriki michezo ama ondoka nyumbani.'

'Angalia kama unaweza kukaa hata lisaa limoja bila kushika simu yako, hii ni mifano ambayo unaweza kuitumia kutathimini uraibu wako'.

Iconos de Whatsapp, Instagram y Facebook

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kutopatikana kwa mitandao kwa saa 6 tu za wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ilizua kizaza na kuonekana kama kipimo kizuri cha kiwancho cha uraibu cha mtumiaji wake

Namna gani tunaweza kutumia teknolojia vizuri?

Marc Masip anajibu swali hili kwa kusema 'ni kutumia tu akili yako ya kuzaliwa.'

'tunatumia teknolojia kama huduma,ndo maana tunalipia, kwa mfano nataka kuingia kwneye mkutano, naweza kutumia teknolojia kuhudhuria mkutano.'

'unaweza kutumia Simu yako ya mkononi kutuma barua pepe bila kufikiria kompyuta. Ukiwa na marafiki zako, mwenza wako jaribu kuepuka simu au wakati unakula ama uko karibu na watu wengine.' Anasema Masip na kuongeza 'watu wako ni muhimu, WhatsApp ni muhimu pia lakini isipopatikana kwa sababu ya mtandao, watu wako wa karibnu kama mwenza wako ataendelea kuwa karibu nawe na mnaweza kuzungumza.'