Miundombinu Mipya ya Makombora ya Nyuklia ya China inayoipa hofu Marekani

Chanzo cha picha, FAS/PLANET LAB INC
Ujenzi wa ajabu wa chini ya ardhi unaendelea kufanyika kwenye jangwa huko magharibi mwa China.
Katika eneo hilo kame katika jimbo la Xianjiang, kilomita zaidi ya 2,000 kutoka Beijing, wanasayansi wa Marekani wamegundua kile wanachoamini kwamba ni moja ya juhudi kubwa muhimu zaidi kwa nchi hiyo ya Asia kuongeza uwezo wake wa nyuklia.
Picha za setelaiti zilizonaswa na watafiti katika Kituo cha James Martin huko Monterey, California, zinaonyesha kile wanachoamini wao kuwa, ni sehemu itakayoweza kuhifadhi karibu makombora makubwa 110.
Ugunduzi huo wa ujenzi, karibu na jiji la Hami kilometa kadhaa kutoka makambi ya waislamu wa jamii ya Uighur yalipo, unaendelea ikiwa chini ya mwezi mmoja baada ya kuonekana kwa ujenzi mwingine kupitia picha za satelaiti kartibu na mji wa Yumen.
Shirikisho la wanasayansi wa Marekani (FAS) linakadiria kwamba nchi hiyo inaweza kuhifadhi makombora 120 ya nyuklia .
"Matokeo haya ni muhimu ikizingatiwa kuwa, kwa sababu ya usiri ambao Uchina imekuwa nao kwa muda mrefu juu ya silaha zake za nyuklia, na haya ndio makadirio tuliyonayo kwa kile kinachotokea huko, "Howard Zhang, mhariri mkuu wa huduma, ameiambia BBC Mundo
"Sera za China kuhusu silaha zake za nyuklia ni kutokuweka wazi taarifa zake kuhusu silaha, kwa hiyo kwa ujumla tunachokifahamu ni kwamba ripoti hii imetayarishwa na wataalam na wanasayansi kutoka sehemu nyingine, hasa kutoka Marekani," aliongeza.
Hofu
Ujenzi wa miundo mbinu hiyo imeibua hofu na udadisi hasa kutoka kwa wachambuzi, kwa kile kinachoonekana ni mabadiliko ama muelekeo mpya wa sera za China khusu silaha za nyuklia.
"Ujenzi wa mnara huko Yumen na Hami ni sehemu ya upanuzi mkubwa wa Nyiklia unaofanywa na China," sehemu ya utafiti wa FAS unasema.
Na kwa mujibu wa Zhang ni kwamba, tangu ifanye majaribio yake ya kwanza kabisa ya bomu la atomiki katika miaka ya 1960s, Beijing imeendelea kuhifadhi silaha ndogo za nyuklia, kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na nguvu zingine za atomiki, lakini kinatosha kutambua uwepo wake.

Chanzo cha picha, FAS/PLANET LAB INC
Lakini wataalam wanahofia kwamba kwa sasa uongozi wa China, ambayo sasa inafuata sera kali za kimataifa, inataka pia kuifanya nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zenye nguvu linapokuja suala la nyuklia.
Minara ya Yumen na Hamis - ni miundo mbinu ya aina yake tangu kumalizika kwa vita baridi , kwa mujibu wa FAS - ikionyesha dalili za mabadiliko.
Kukua kwa nguvu zake
Kwa mujibu wa FAS, ujnezi huo mpya unafanyika kilometa 380 ulipo ujenzi mwingine uliogunduika mwezi uliopita, ambao uko katika hatua za mwanzo mwanzo.
Kama miundo mbinu iliyoibuliwa awali, umewekwa katika eneo la jangwa lenye ukubwa wa mita za mraba 800.
Kila mnara upo kilometa 3 kutoka mwingine na mengine imefichwa kwa mfuniko mkubwa, ukifuata utaratibu wa vinu vingine vya atomiki vilivyopo sehemu mbalimbali za China.
Marekani imeguswa na hatua hiyo ya China na kupitia Idara yake ya Ulinzi imeonyesha wasiwasi wake kuhusu hilo.
"Hii n mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili kwamba umma unabaini kile kilichokuwa kinasemwa kwa muda mrefu kuhusu vitisho viavyoongezeka duniani na usiri unaozunguka mipango hiyo," anaandika.
Kwa miaka mingi, Beijing imekuwa ikiendesha zaidi ya vinu 20 kuhifadhi kile wanachokitaja ni DF-5s.
Hata hivyo, kwa mujibu wa tathimini iliyofanywa sasa kupitia picha za satelaiti, inaonekana kwamba itajenga mara 10 zaidi.
Kuongeza uwezo wake
Kwa mujibu wa Zhang, kwa miongo kadhaa sasa nyuklia haikuwa miongoni mwa vipaumbele vya China.
"Kumiliki nyukilia ni gharama sanana nahitaji miundo mbinu na vinu vya teknolojia ya hali ya juu," alisema.
"Kwa nchi kama Urusi na Marekani ilikuw arahisi kwao kumiliki nyuklia kwa sabababu ya uwezo wao na imekuwa ikimiliki mitambo ya nyuklia kwa muda mrefu, lakini tofauti na China, ndo kwanz aimeanza kujiingiza kwenye sekta hiyo katika miongo ya hivi karibuni," alisema.

Chanzo cha picha, FAS/PLANET LAB INC
Kwa mujibu wa kituo cha kimataifa cha Utafiti cha Stockholm Marekani ina mabomu ya nyuklia karibu 5,550 yanayoweza kurushwa kwa mfano na roketi huku Urusi ikiwa na 6,255.
Marekani inakadiria kwamba kwa mwaka jana China ilikuwa na mabomu 200, huku kituo cha utafiti cha Stockholm kinakadiria kuwa 350. Hata hivyo idadi hiyo imeongezeka kutoka 145 yaliyokadiriwa na kituo hicho mwaka 2006.
Mapema mwaka 2021, Mmoja wa viongozi waandamizi wa jeshi Marekani, Charles Richard, alisema kwamba "Silaha za nyuklia za China zinatarajiwa kuwa mara mbili zaidia kama sio mara tatu au mara nne katika kipindi cha muongo mmoja ujao."
China has notably boosted its nuclear weapons capabilities in recent years with the development of mobile road missile launchers or the recent nuclear-capable H-6N bomber launched from submarines.
Kilichoko nyuma ya pazia
Kwa mujibu wa Zhang, moja ya swali kubwa lisilo na majiu kwea sasa kuhusu ujenzi huo wa miundombinu ya nyuklia ni kwamba nini hasa lengo la China na kwa nini sasa?
"Kwa eneo wanalozungumza kichinia, kwa sasa mjadala mkubwa ni kama China inapeleka ujumbe kwamba inaongeza akiba zake na kupeleka ujumbe kwa Marekani kwamba kwa miaka mingi imekuwa ikiichukulia poa uwezo wa China kwenye sula la nyuklia ", anasema.
Taarifa zingine zinasema, China inashughulikia kutengeneza silaha nyingine ambayo haifahamiki bado.

Chanzo cha picha, Reuters
Outside the negotiations
Kugundulika kwa vinu hivyo nchini China kunakuja wakati nchi mbili kubwa zinazomiliki silaha za nyuklia, Marekani na Urusi zikijiandaa kufanya mazungumzo ya namna ya udhibiti wa silaha hizo.
Mkutano baina ya Marekani waliowakilishwa na Wendy Sherman na Urusi iliyowakilishwa na naibu waziri wa masuala ya kigeni, Sergei Ryabkov unaonekana ni hatua ya kwanza ya kuibua mazungumzo yaliyokwama kwa muda sasa kuhusu kupuguza umiliki wa nyuklia.
China, hata hivyo imekuwa ikigoma kwa mika sasa kukaa chini na kuzungumza kuhusu nyuklia zake. h













