Ndoa ya Kiyahudi: Wanawake ambao hawana uhuru wa kuachana na waume zao

Rifka Meyer alikuwa na miaka 32 alipoolewa kulingana na desturi ya Wayahudi na kuwa sehemu ya ndoa ya kidini.
Miaka miwili na nusu baadae, aliachwa kama 'mke aliyefungwa minyororo' katika familia ya Kiyahudi ya Orthodox.
Alikuwa katika ndoa ya kidini na mwanamume ambaye alikataa kumpa talaka.
Akizungumza na BBC, Rifka anasema- "Nilendelea kuhisi upweke na kukosa matumaini, nilikuwa nahisi kana kwamba napiga kelele lakini hakuna anayenisikiliza." Iliwachukua takriban miaka 10 kuachana.
Kiongozi wa cha Labor Jonathan Mendelson anasema wanawake 100 wa jamii ya Kiyahudi ya Haredi nhini Uingereza bado wamenaswa katika ndoa ya kama hiyo ya kidini ijapokuwa wanataka kujiondoa.
Jonathan ni mwanachama wa kamati ya bunge iliyobuniwa kuwasaidia wanawake kama hao.
Chini ya sheria ya Wayahudi wa Orthodox, mwanamke nachukuliwa kuwa ameolewa hadi mume atakapompa (hati) maalum inayothibitisha wameachana hata kama ameachwa kisheria
Wanawake hunaswa katika ndoa kama hizo za kidini zinazofahamika 'Agnaut' au 'Mke wa Chand'.
Marekebisho ya sheria Uingereza na kupigwa kwa Wayahudi
Rifka Meyer anasema kuwa hawezi kuwa katika mahusiano mengine hadi apte hati hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Anasema, "Unakwama huwezi hata kupata mpenzi mwengine mpya, sikuweza kuendelea na maisha yangu.
Nilikuwa katika hali ngummu, nisijue la kufanya wala pa kwenda. Hakuna mazungumzo na msaada ambao utakuonyesha njia.
Unakuwa mpweke na kukosa utulivu, alafu uunajipata ukikabiliana na hali hiyo peke yako.
Ni vigumu kiasa gani kuachana
Meyer, ambaye anaishi London hatimaye alipata hati ya kuachana na muwe wake mwaka jana baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Sasa ameamua kuanzisha shirika la 'Get Out' ili kuwasaidia wanawake walio katika hali kama iliyomkabili
Uingereza imefanyia marekebisho kifungu cha sheria kuhusu unyanyasaji wa nyumbani ili kumwajibisha kisheria mume akikataa kutoa talaka ya Kiyahudi, kumnyanyasa mke wake au akipatikana na makosa hayo.
Akipatikana na hatia kuna sehemu ya sheria hiyo inayopendekza afungwe jela.
Mawaziri wa Uingereza wanaamini hatua hii itawaaezesha wanawake kuwasilisha malalamishi rasmi wakishindwa kujiondoa katika ndoa ya kidini.
Lakini Shirikisho la Sinagogi, kikundi kinachowakilisha Wayahudi wa Orthodox, kinasema talaka hiyo litakuwa batili chini ya sheria ya Kiyahudi ikiwa itatolewa katika mazingira ya mateso, hofu ya kifedha au hofu ya kwenda gerezani.
'Hata baada ya talaka kutolewa kwa njia hiyo, bado mume na mke watachukuliwa kuwa bado hawajaachna.'

Hoja za Wayahudi wa Orthodox
Eli Spitzer ni mwalimu na mwanachama wa jamii ya Wayahudi wa Orthodox.
Anasema kuwa wataalam wengine wa Kiyahudi wanaamini kwamba kutafuta msaada wa wanawake chini ya sheria hii mpya "kutaanza mchakato ambao hatutaweza kubadilishwa zaidi."
Pia anahoji kuwa, "baada ya sheria hii kufanyiwa marekebisho, mume hataweza kumpa talaka mkewe kwa hiari yake, bila shaka atatoa talaka kwa kuhofia kushtakiwa na ndio sababu wataalam wa dini wanaamini kuwa itakuwa kinyume na dhana nzima ya talaka ya Kiyahudi, Kusudi lake ni kutoa talaka kwa hiari.
Lakini Bwana Mendelson, ambaye mwenyewe ni Myahudi, anapinga msimamo huo wa wataalam wa dini.
Akihoji lengo lao, anasema, "Hawa watu wenyewe wanaleta ubishi wakati hakuna kitu kama hicho, nashuku wanafanya hivyo kwa sababu wanaonekana kupoteza udhibiti katika mchakato wote.
Lakini chini ya hali yoyote, katika demokrasia ambayo watu wachache wa kidini wanaishi, inahitajika pia kudhibiti mambo kama hayo. Lazima waelewe kuwa hii ni Uingereza na hii ni Uingereza ya 2021.
Meyer anasema marekebisho ya sheria ya unyanyasaji wa nyumbani yangewasaidia wanawake , lakini "kufanya kazi na viongozi dini ya Kiyahudi " ni muhimu.
"Wanawake wanahisi kukata tamaa na watafanya kila wanaloweza kupata njia ya kujiondoa," Maisha ya hawa wanawake hukwama katika ndoa ''iliyokufa'', anasema.












