Ufalme wa Zulu: Jinsi waasi wa ufalme na wanawafalme wanavyopigania uongozi

Mfalme Zwelithini mekuwa uongozjni 7kwa miaka 50

Chanzo cha picha, Sowetan/Getty

Maelezo ya picha, Mfalme Zwelithini amekuwa uongozini kwa miaka 50

Ufalme wa Zulu nchini Afrika Kusini umezongwa na utata, kufuatia kifo cha Mfalme Goodwill Zwelithini na wiki chache baadaye - mrithi wake.

Hali hiyo imesababisha mvutano wa uongozi katika ufalme huo - huku wahusika wakipambana mahakamani , na kurushiana matusi hadharani mbali na kusambaza uvumi kuhusu kutiliwa sumu kwa wapinzani.

Mwanahabari wa BBC Pumza Fihlani anatazama baadhi ya watu muhimu katika tukio hilo la ufalme.

Baba wa taifa : Mfalme Goodwill Zwelithini

Alizaliwa tarehe 14 mwezi Julai , 1948, alikuwa mfalme wa nane wa taifa la Zulu.

Kabla ya kuchukua madaraka kutoka kwa baba yake mwaka 1971, alilazimishwa kwenda mafichoni kwa miaka mitatu kufuatia vitisho vya kuuawa.

Isilo Samabandla Onke, ikitafsiriwa Mfalme wa wafalme wa Zulu , kama alivyoitwa , alikuwa mrithi wa moja kwa moja wa Mfalme Cetshwayo , kiongozi wa taifa la Zulu wakati vita vya mwaka 1879 dhidi ya jeshi la Uingereza.

Kwa wengi , baba huyo wa Watoto 28 kutoka kwa wake sita, aliheshimu sana utamaduni wa enzi hizo. Makala ya utawala wake ni ufufuzi wa densi ya Reed mwaka 1991.

Sherehe hiyo iliohudhuriwa na wanawake wengi ambao hawajaolewa kutoka kwa taifa la Zulu hulenga kusherehekea ubikira, lakini mfalme Zwelithini alisema kwamba ilifanyika ili kukuza hamasa ya virusi vya ukimwi katika jimbo la Kwa Zulu Natal , mkoa ulio na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini humo.

Densi ya ubikra hufanyika kila mwaka katika kasri la Enyokeni Royal Palace

Chanzo cha picha, Sowetan/Getty

Maelezo ya picha, Densi ya ubikra hufanyika kila mwaka katika kasri la Enyokeni Royal Palace

Mfalme Zwelithini alifariki tarehe 12 mwezi Machi katika hospitali ambapo alikuwa akitibiwa ugonjwa wa sukari .

Alikuwa mfalme aliyehudumu kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 50.

Baada ya kuzikwa, wasia wake ulisomwa katika mkutano wa ufalme huo.

Lakini urithi wake umezua utata katika familia hiyo ya kifalme , huku baadhi ya wanafamilia wakisema kwamba wasia huo ni bandia.

Mtawala wa ufalme: Malkia Mantfombi Dlamini-Zulu

Kulingana na wasia, mfalme huyo alichagua kuwa mrithi wa taifa hilo lenye watu milioni 11.

Malkia Dlamini Zulu alitarajiwa kusimamia utawala huo katika kipindi cha miezi mitatu maana alitarajiwa kumtaja mrithi wa mfalme huyo.

Lakini alifariki kabla ya kufanya hivyo.

Malkia wa Zulu Mantfombi Dlamini Zulu

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Malkia wa Zulu Mantfombi Dlamini Zulu

Alikuwa dada yake mfalme Mswati wa eSwatini 111, na aliolewa na mfalme wa Zulu mwaka 1977.

Kwasababu anatoka katika ufalme, malkia Dlamini ndiye aliyekuwa mke mkuu.

Alijaliwa watoto wanane na mfalme marehemu .

Ukilinganisha na wake wengine wa mfalme huyo mahari yake ya ng'ombe 300 ililipwa na taifa la Zulu kufuatia ukusanyaji katika jamii hiyo.

Wanahistoria wanasema kwamba hatua hiyo ilimfanya kuonekana mtu mkubwa katika familia hiyo ya kifalme.

Uteuzi wake kuwa mrithi ulizua madai kwamba mwanawe mkubwa wa kiume , aliyesoma nchini Marekani, Mwanamfalme Misizulu Zulu atakuwa mfalme mpya ijapokuwa familia hiyo ya kifalme haikuthibitisha hilo.

Malkia huyo mwenye umri wa miaka 65 alifariki kutokana na ugonjwa usiojulikana miezi kadhaa baada ya kuchukua hatamu kama mrithi.

Kifo chake mwezi Aprili kiliwacha maswali mengi na kuzua uvumi wa njama ya mauaji.

Katika kipindi cha miaka michache iliopita alikuwa akitumia wakati wake mwingi huko eSwatini ili kuangaliwa afya yake.

Wakati mmoja Mfalme Zwelithini akielezea kutokuwepo kwake katika taifa la Zulu alisema kwamba alipewa sumu.

Mfalme huyo alizungumza kabla ya mamia ya watu mwezi Disemba 2017 wakati tulipokutana kusherehekea maadhimisho ya kuapishwa kwake.

Mbele ya watu hao wote mfalme huyo alisema , malkia alisema Mnemtanenkosi amepewa sumu.

Hiyo ndio sababu hayuko nasi hapa, alikumbuka waziri mkuu wa Zulu Mangosuthu Buthelezi katika taarifa wiki hii.

Hakuna maelezo zaidi yaliopo kuhusu madai hayo ya sumu kutoka 2017, lakini inaeleweka kwamba amekuwa hospitalini mara kwa mara tangu wakati huo.

Malkia Mantfombi, mapme mwaka 1970s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia Mantfombi, mapme mwaka 1970s

'Haijulikani alivyofariki'', Buthelezi alisema kwamba ukaguzi wa chanzo cha kifo chake ulifanyika kubaini chanzo na matokeo yake yaliotarajiwa katika kipindi cha wiki chache zijazo''.

''Nilipotangaza kuhusu kifo cha mrithi wa mfalme , nilizungumza na Kizulu, nikielezea kwamba madaktari hawakutaka kumfanyia upasuaji kutokana na sumu katika ini lake. Hii ilihitaji matibabu ya antibiotics ili kupunguza maambukizi''.

Haijulikani ni vipi utata huo wa uongozi utatatuliwa na ni lini mfalme mpya atachaguliwa ,lakini kuna shinikizo kwa familia ya kifalme kufanyika kwa amani na kwa njia ya heshima. Ufalme huo una tamaduni za karne kadhaa na zinaheshimiwa na Wazulu.

Malkia: Sibongile Dlamini

Mke wa kwanza wa mfalme Zwelithini , alienda mahakani ili kugawiwa nusu ya mali ya mume wake , inayoshirikisha mali kadhaa , ardhi kubwa katika mkoa wa KwaZulu Natal ambayo mfalme huyo alikuwa mdhamini wake.

Haijulikani ni kiwango gani cha pesa zilizoachwa na mfalme huyo. Serikali ya KwaZulu inaupatia ufalme huo jumla ya $4.93m kama fedha za matumizi.

Mwanamfalme aliyeuawa: Lethukuthula

Kwa miaka kadhaa kulikuwa na uvumi kwamba mfalme angemchagua mwanawe mkubwa mwanmfalme Lethukuthula, kama mrithi wake . Mwanamfalme alikuwa mwana wa mke wa mfalme , kulingana na gazeti la Afrika kusini la South Africa's City Press.

Lakini mwamfalme huyo alifariki mwezi Novemba katika hali ya kutatanisha . Baadhi ya waliopo katika ufalme huo huenda walijaribu kumzuia kuchukua uongozi lakini hilo halijathibitishwa.

Mwanamfalme Lethukuthula

Chanzo cha picha, KwaZulu-Natal government/Twitter

Maelezo ya picha, Mwanamfalme Lethukuthula

Waasi wa ufalme huo: Mwanamfalme Mbonisi na Bintimfalme Thembi

Siku kadhaa baada ya kifo cha mfalme huyo , Mwanamfalme Mbonisi na Bintimfalme Thembi walituhumiwa kwa kufanya mikutano ya siri katika kasri la ufalme huo. Imedaiwa kwamba walikuwa hawapendelei uteuzi wa malkia Manftombi kama kaimu kiongozi.

Habari za mkutano huo wa siri zimezua hali ya tumbo joto kwa baadhi katika familia hiyo ya kifalme ambao wanaamini wataleta mgawanyiko mkubwa.

Chifu Buthelezi

Tangu kifo cha mfalme Zwelithini, Chifu Buthelezi amekuwa akizungumza kuhusu yanayoendelea ndani ya ufalme huo.

Anaonekana kama waziri mkuu wa kitamaduni wa marehemu mfalme huyo na amechukua jukumu kuu katika kutangaza kifo cha mfalme na mrithi wake na kuelezea umma kuhusu maandalkizi ya mazishi.

Mfalme wa Zulu Zwelithini na Chifu Buthelezi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfalme wa Zulu Zwelithini na Chifu Buthelezi