Kwa wanaotaka nywele ndefu siri ni lishe na vyakula hivi

Ni ndoto ya wengi hasa akina dada kuwa na nywele ndefu na zenye afya lakini sio kila mmoja ana bahati ya kuzipata bila kutumia kemikali ama mafuta aina mbali mbali.
Lakini unaweza kutimiza ndoto hii kwa kuboresha lishe yako kwa vyakula hivi.
Nywele kavu ,laini na zenye mvuto bila shaka ni ishara ya afya njema na uzingativu wa lishe yako ni hatua muhimu sana ya kujihakikishia hilo .
Leo tunakupakulia siri ya umuhimu wa vyakula hivi katika kuhakikisha kwamba una nywele zenye ubora huo .
1. Mayai yanakupa protini
Kiungo kikubwa cha nywele ni protini na mayai yanayo protini ya kutosha .Iwapo hupati madhara kwa kuyala mayai au aina yoyote ya protini basi fahamu hilo .
2. Mboga za Spinach na nyingine zenye Iron
Iron ni kiungo muhimu katika seli za nywele yako na haya inafahamika kwamba uhaba wa iron unaweza kukufanya upoteze nywele .
Wakati mwili wako unapokosa Iron ,yamaanisha kwamba hewa ya oxygen na virutubisho havifiki katika mzizi wa nywele zako hatua inayodumaza ukuaji wa nywele zako.
3. Matunda ya familia ya chungwa na Vitamin C
Mwili wako unahitaji Vitamin C ili kuweza kunyonya iron na hivyo basi unahitaji matunda ya familia ya chungwa ili kupata vitamin hiyo .
Wataalam wa lishe wanasema ndimu au limau moja kwa siku linatosha kukupa dozi ya siku ya vitamin C .
Vitamin C pia inahitajika katika uzalishaji wa kiungo cha Collagen kinachoungainisha sehemu za nywele na ngozi yako kichwani na kupitisha virutubisho .
4. Njugu na nafaka za aside za Omega 3
Mafuta ya omega yanayotokana na aside nzuri zinasaidia nywele 'kunenepa' na kuwa nzuri.
Kwa sababu mwili wako hauwezi kutoa asid hizi za mafuta unahitaji kuzila .Vyakula vya mbegu kama vile njugu ,korosho ,njugu mawe na vingine pia vina mafuta hayo muhimu .

5. Nafaka nzima
Nafaka nzima zina wingi wa Biotin pamoja na iron, zinc na Vitamin B .Biotin ni kiungo muhimu sana katika kuunda amino acids -protini inayohitajika kusaidia katika ukuaji wa nywele .
6. Karoti zina wingi wa Vitamin A
Ukipata sharubati ya karoti kila siku basi utakuwa umejiokoa katika kuhakisha kwamba nywele zako zinakuwa kwa haraka .
Nywele zina tishu inayokuwa haraka sana mwilini na vitamin A inahitajika na seli kwa ukuaji huo .
7. Parachichi/Avocado ina Vitamin E
Vitamin E inaboresha kukimbia kwa damu na kusaidia pengo za mizizi ya nywele kufanya kazi vizuri na kusaidia ukuaji wa nywele . Pia vitamin E inasaidia kuhakikisha kuwa viwango vifaavyo vya PH .












