Mwanamfalme Latifa: Binti wa mtawala wa Dubai aliyetoweka

Princess Latifa bint Mohammed Al Maktoum and Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum

Chanzo cha picha, Getty Images / Princess Latifa

Taarifa za kutatanisha za binti wa mfalme zimejitokeza kuhusiana na utekaji nyara usio wa kawaida na kuzuiwa katika sehemu ya siri.

Ni miezi mingi tangu mara ya mwisho Tiina Jauhiainen alipomuona rafiki yake.

Binti mfalme Latifa, alifungiwa huko Dubai baada ya kujaribu kutoroka, alikuwa anaendelea kuwasiliana naye kwa muda kwa kutumia simu aliyokuwa nayo kisiri.

Lakini ghafla, mawasiliano yakakatika.

Short presentational grey line

Mara ya mwisho Tiina kumuona Latifa, walikuwa wamelala kwenye mashua huku wakiwa wanatazama juu na kufurahia miale ya jua, wakati wanasafiri katika bahari Hindi.

Ilikuwa ni Februari 2018, wakiwa wamepanga safari hatari ya kumtorosha Latifa kutoka Dubai na kuanza maisha mapya nje ya nchi hiyo.

Binti mfalme huyo ni mmoja kati ya watoto 25 wa Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum, mtawala wa Dubai.

Sheikh amebadilisha mji mzima na kuufanya unaong'aa, eneo ambalo watu wanamiminika kufanya biashara na eneo muafaka la mapumziko.

Lakini kwa wanawake wa Dubai, sheria na utamaduni vinaweza kufanya maisha kuwa yenye masharti magumu sana.

Dubai skyline and beach

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pwani ya mji wa Dubai

"Siruhusiwi kujiendesha, Siruhusiwi kusafiri wala kuondoka Dubai kabisa," Latifa amesema katika video iliyorekodiwa kabla tu ya kutoroka.

"Sijawahi kutoka nje ya nchi hii tangu mwaka 2000. Nimekuwa nikiuliza maswali mengi kuhusu kusafiri tu, au kwenda kusoma, ama kufanya kitu kingine chochote kile cha kawaida. Lakini hawataki kuniruhusu. Nataka kuondoka."

Akiwa ameketi katika makazi ya Tiina, Latifa alizungumza kwa ucheshi juu ya kile kinachotarajiwa kujitokeza.

"Nina matarajio makubwa juu ya hatma yangu. Sijui nitahisi namna gani nikiamka asubuhi na kuona kwamba naweza kufanya chochote ninachotaka kwa siku hiyo. Yaani nasubiri sana siku hiyo."

Binti mfalme huyo hakuwa na pasipoti yake na pia alikuwa chini ya ulinzi kwa hiyo waliondoka Dubai kimyakimya na kuendesha gari hadi pwani ya Oman.

Iliwachukua saa kadhaa kuondoka katika maji ya eneo hilo.

Na kufikia jioni walifikia dau ambalo lilikuwa linatakiwa kuwa chanzo cha kuwapeleka eneo watakakokuwa uhuru.

Princess Latifa and Tiina Jauhiainen on the first leg of their journey in 2018

Chanzo cha picha, Tiina Jauhiainen

Maelezo ya picha, Binti mfalme Latifa na Tiina Jauhiainen wakiwa wameanza safari yao mwaka 2018

Katika ujumbe wa Whatsapp kwa rafiki yake, Latifa alitangaza: "Sasa niko huru".

Walikuwa wamepanga kuanza safari ya Bahari Hindi, na kisha wakasafiri hadi Marekani ambako Latifa anaweza kuanza kutafuta hifadhi kwasababu za kisiasa.

Lakini siku nane baadaye, wakati wanakaribia pwani ya bahari Hindi, safari ya kutoroka kwao kukaenda mrama na mambo yakabadilika ghafla.

Wanaume waliokuwa na silaha walivamia boti walilokuwa wanasafiria. Rafiki zake wakajificha kwenye chumba cha kuoga hadi walipolazimika kutoka kwasababu ya moshi ya guruneti iliyokuwa imerishwa.

"Latifa alikuwa anapiga kelele na kurusha mateke. Alikuwa anasema 'musiniregeshe UAE. Niueni tu hapa'," Tiina alisema. Hiyo ndio mara ya mwisho alimuona rafiki yake.

Baadaye katika video ambazo zimejitokeza muda huu, Latifa anaonesha wazi madhila aliyokumbana nayo.

"Nilikuwa ninapigana, na huyu kijana akaja na pochi, akatoa sindano na kunidunga mkononi."

Latifa anasema kisha akaingizwa katika meli ya kijeshi iliyokuwa Bahari ya Hindi.

"Makomando wakanibeba na kunipitisha kwenye ushoroba, kunipeleka hadi kwenye chumba kikubwa na mbele yangu kukawa na majenerali kama wanne au watano.

"Nikirejelelea maneno haya mbele yao 'Jina langu ni Latifa al Maktoum'.

"Sitaki kwenda Dubai, Nataka kutafuta hifadhi kwingineko. Nilikuwa katika sehemu ya maji ya kimataifa, munastahili kuniacha niende zangu."

Lakini maombi yake yalikuwa hayafiki kokote, na anasema kwamba akakabiliwa na komando wa Emirati.

"Alinishika. Akaninyanyua. Akanipiga mateke alikuwa mkubwa kuniliko. Nguo yake ikapanda juu na nikamuona mikono. Nikaamua kumpiga kwa nguvu kadiri ya uwezo wangu na kutikisa kichwa changu huku akipiga kelele."

Anasema alidungwa sindano na kurejeshwa Dubai.

Sheikha Latifa bint Mohammed Al Maktoum with Dubai skyline behind

Chanzo cha picha, Getty Images

"Nilihisi vibaya kweli. Nilihisi juhudi zangu za miaka mingi kuhakikisha ninapata uhuru wangu nilihisi zimegonga mwamba. Na nimekuwa hapa peke yangu. Nikiwa nimefungiwa. Siwezi kupata matibabu, si shitakiwi, si funguliwi mashitaka, yaani hakuna chochote kinachoendelea."

Short presentational grey line

Tiina alirejeshwa UAE kwa kutumia dau ambako alizuiliwa kwa wiki mbili. Kisha akaanza kuelezea simulizi yake kwa vyombo vya habari vya kimataifa.

Alianzisha kundi la kampeni lengo likuwa ni Latifa kuachiwa huru na kupeleka kesi ya binti huyo wa mfalme Umoja wa Mataifa.

Lakini kadiri miezi ilivyokuwa inaendelea kusonga, hakuwahi kusikia lolote kutoka kwa Latifa.

Siku moja, 2019, wakati anatembelea familia yake huko Finland, alipata ujumbe kutoka kwa mtu asiyemjua.

Kwanza alilazimika kujibu maswali ya kiusalama. Miaka michache iliyopita, Tiina alikuwa amemfunza Latifa capoeira, sanaa ya kupigana ya Brazil. Na sasa mtu huyo asiyemjua alitaka kujua jina la utani la Latifa capoeira.

Na muda mfupi baada ya hapo, Tiiina akafanikiwa kuwasiliana na binti mfalme moja kwa moja.

"Mara ya kwanza kusikia sauti yake, nililia. Sikuweza kujizuia. Nilikuwa na hisia kali kweli."

Tiina Jauhiainen
Maelezo ya picha, Tiina Jauhiainen

Latifa alifanikiwa kujirekodi video yenye ujumbe, Na kile walichokibaini kiliwashutua.

Binti mfalme, ambaye sasa hivi ana umri wa miaka 35, alionekana akiwa kwenye kona ya bafu akizungumza kwa sauti ya chini.

"Najirekodi video hii nikiwa bafu, kwasababu hii ndio sehemu pekee yenye mlango ninaoweza kuufunga. Nimeshikwa mateka. Mimi siko huru. Nimefungiwa katika gereza hili. Sina udhibiti wa maisha yangu."

Akionekana aliyepauka, alikuwa amekaa kwa miaka mitatu bila kupata jua vizuri.

"Niko katika nyumba hii ya kifahari, ambayo imebadilishwa kuwa gereza. Madirisha yote hayafunguki. Kuna polisi watano nje na polisi wawili wa kike ndani ya nyumba hii. Na siwezi hata kwenda nje kupata hewa safi."

Nyumba hii ipo mita chache tu kutoka ufuoa wa bahari.

"Tusidhanie tu kwamba kwasababu ni nyumba ya kifahari, basi kila kitu kiko sawa", Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, Ken Roth, amesema.

"Huyu mwanamke amefungiwa. Ni eneo alilofungiwa akiwa peke yake isipokuwa kwa walinzi wake. Kufungiwa kwa namna hiyo kunachukuliwa kuwa aina ya mateso."

Hofu ni vile Latifa anavyosikika kwenye video. Sauti yake inaashiria hali ya dharura na kutojua la kufanya.

"Kila siku nina wasiwasi juu ya usalama na maisha yangu. Sina uhakika kama nitawahi kunusurika hali hii. Polisi wamenitishia kwamba nitakuwa gerezani kwa kipindi chote cha maisha yangu na sitawahi kuona jua tena. Kwahiyo, hapa siko salama."

Licha ya hatari kwamba atapatikana na simu hiyo aliyonayo kisiri, alianza kuonesha utulivu na kuanza kusimulia simulizi yake ya kipekee.

Short presentational grey line

"Kwangu ni rahisi tu, ni kama, niko huru au siko huru? Sawa. Dunia itajua kwamba siko huru. Yeyote anayejali atajua kwamba mimi siko huru na sitakubali propaganda zao. Hivyo ndivyo nilivyo."

Sheikh amesema anachukulia kurejea kwa Latifa Dubai kama uparesheni ya uokozi.

Desemba 2018, baada ya Latifa kutojulikana alipo kwa miezi 9, UAE ilipata shinikizo kali sana. Umoja wa Mataifa ulikuwa umetaka uthibitisho wa kwamba yuko hai - la sivyo itaanza kupaza sauti na kuonesha wasiwasi wake kwamba huenda binti mfalme huyo amefariki dunia.

Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum at Royal Ascot , 21 June 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum akiwa amevaa vazi la kifalme, Juni 2019

Latifa alitembelewa na mama yake wakambo mke wa mfalme Haya.

Haya alimuomba kula naye chakula cha mchana.

"Alisema kwangu mimi itakuwa kama mtihani, kuona utakavyokuwa mbele za watu baada ya kuwa gerezani kwa kipindi kirefu," anasema Latifa katika moja ya video. "Na ikiwa utaonesha tabia nzuri, utakuwa huru siku chache zijazo."

Latifa asijue kwamba, mama yake wakambo Haya alikuwa amejipanga kusema uongo kumhusu kwamba ana tatizo la kubadilika badilika kwa hisia na kwamba ni rahisi kwake kuwa katika hatari ya kudhulumiwa. Kusaidia kuthibitisha kwa Umoja wa Mataifa kwamba Latifa yuko sawa, Haya alimpigia rafiki yake simu, aliyekuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika shirika la kutetea haki za binadamu Mary Robinson.

Desemba 15, mwaka 2018, Mary Robinson alisafiri hadi Dubai na kusema kuwa Haya na maafisa wake walimtaarifu juu ya ugonjwa wa Latifa, "kimatibabu". Na akakubali kutoa usaidizi wake kwa kuwasiliana na Umoja wa Mataifa.

Wakati huo, Latifa, alikuwa hajui kinachoendelea. Wakati wa chakula cha mchana walizungumza juu ya mazingira yake, kuruka angani kwa mwavuli na pia juu ya kitabu ambacho Mary Robinson alitarajia kuchapisha.

Princess Latifa bint Mohammed Al Maktoum has lunch with Mary Robinson, a former United Nations High Commissioner for Human Rights and former president of Ireland - picture released December 2018

Chanzo cha picha, UAE government handout

Maelezo ya picha, Binti mfalme Latifa akiwa na Mary Robinson

"Hatukuwahi kujadiliana kunihusu. Hatukuzungumzia kesi yangu kabisa," Latifa amesema. Hakujua kwamba Robinson aliwahi kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayesimamia masuala ya haki za binadamu.

Mary Robinson alituambia kwamba hakumhoji Latifa kuhusu video au kutoroka kwake, au kutaka kuonana nae moja kwa moja.

"Sikujua kuzungumza na mtu mwenye tatizo la kubadilika badilika kwa hisia. Yaani sikutaka kabisa kuzungumza naye na kuongeza maumivu aliyokuwa anapitia katika chakula kile cha mchana kilichotarajiwa kuwa jambo la kufurahisha."

Lakini baadaye, Robinson aliruhusu Latifa kupigwa picha alizozituma kwa Umoja wa Mataifa. Robinson anasema aliamini kwamba hizi ni picha za kibinafsi na alishutuka baada ya kuona nchi ya UAE imezitoa kwa umma siku tisa baadaye.

Baada ya chakula cha mchana Latifa alirejeshwa gerezani kwake. "Yaani ulikuwa mtego. Ni kama walinilaghai," Latifa anasema. Hakuna kilichobadilika kwa Latifa asiyejulikana alipo.

Lakini kwa mama yake wakambo haya, kulikuwa na mendeleo yasio yakawaida.

"Muda mfupi baadaye," Robinson anakumbuka, "Nilipigiwa simu na Haya, akisema 'Mary, niko London. Nimekuja London na watoto wangu wiwili. Nimevaa nguo zilezile nilizokuwa nimevaa kwasababu nilikuwa na hofu sana. Tulikuwa tumekosea. Nimebaini mengi tu.'"

Baadaye, Haya alisema kwamba Sheikh hakutaka kusikia chochote cha Latifa na badala yake aliendelea kuwa mkatili wake.

Na kufikia Aprili 2019, anasema anaamini kwamba maisha yake nchini Dubai hayakuwa salama. Aprili 15, alitorokea Uingereza.

Princess Haya bint Al Hussein arrives at Royal Courts of Justice in London, July 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mke wa mfalme Haya akiwa London, Julai 2019

Sasa akiwa anakabiliwa na kutoroka kwa mmoja wa wake zake na watoto wawili zaidi, Sheikh alianza kwa kufungua kesi katika mahakama ya juu akitaka kurejeshewa watoto wake Dubai.

Lakini alichopata ikawa ni mengi zaidi ya aliyokuwa anapigania.

Machi 2020, uamuzi wa mahakama ya juu ukabaini kuwa maelezo ya kina zaidi kuhusu matibabu ya wasichana wake wakubwa. Miaka 18 awali, binti yake wa pili, Shamsa, alitekwa nyara Uingereza na kurejeshwa Dubai, ambako amekuwa akishikiliwa mateka tangu wakati huo.

Umauzi huo uliangazia simuli hiyo kwa ujumla, kwa mara ya kwanza ukazungumzia vile maafisa wa Sheikh walikuwa wamemfuatilia hadi Cambridge na kumrejesha nyumbani.

Pia jaji alibaini kuwa Haya ametishiwa maisha na Latifa ametekwa nyara na kufungwa gerezani - na kuwa Sheikh hakuwa mkweli mahakamani.

Short presentational grey line

Kwa Tiina, huu ulikuwa kama ufunguo kwake. "Nilifikiria kwamba hatua hiyo ingeharakisha kuachiwa kwa Latifa."

Lakini kwa mara nyingine tena, hakuna kilichobadilika kwa Latifa katika suala la kufungiwa gerezani Dubai.

"Nikawa najiuliza, ni kipi kinachohitajika ili aachiwe huru? Inasikitisha. Inasikitisha sana," Tiina amesema.

Akiwa peke yake, kwenye gereza alilofungiwa Dubai, Latifa alifuatilia kesi hiyo na kuendeleza mawasiliano na rafiki yake pamoja na binamu yake Marcus na mwanzilishi mwenza wa kampeni inayoshinikiza Latifa aachiwe huru ya 'Free Latifa' David Haigh.

Latifa alikuwa katika mwaka wake wa tatu akiwa amefungiwa gerezani.