Je Tanzania itaiga mfano na kuondoa marufuku ya kutohudhuria shule kwa wasichana wajawazito?

Back of Fatu, the 13 year old girl who is pregnant after suffering sexual abuse

Chanzo cha picha, Waves

Maelezo ya picha, Fatu anakubali kuwa sio rahisi kuwa mjamzito kama unasoma lakini amedhamiria kumaliza masomo yake
Muda wa kusoma: Dakika 4

Serikali ya Tanzania ilipelekwa mahakamani mwezi uliopita kwasababu ya kupiga marufuku wasichana wa shule waliopata ujauzito na kina mama wadogo kuhudhuria shule. Ni moja ya nchi chache duniani ambayo inayotekeleza marufuku ya hiyo.

Mwaka mmoja uliopia mwezi kama huu, mahakama moja nchini Sierra Leone, iliagiza kubadilishwa kwa hatua ya marufuku ya wasichana wadogo waliopata ujauzito kuhudhuria shule iliyokuwa imeweka sawa na hatua iliyochukuliwa Tanzania.

Lakini je kubadilishwa kwa marufuku hiyo Sierra Leone kumebadilisha nini?

Fatu ambaye sio jina lake halisi, ana umri wa miaka 13 na ana ujauzito wa miezi minne. Ni miongoni mwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono.

Kama marufuku hiyo haingekuwa imebadilishwa hadi mwaka huu, ingemaanisha kuwa msichana huyo aache shule na kulazimika kuolewa, lakini sasa anaendelea kutimiza ndoto ya kwamba siku moja atakuwa daktari.

Mnamo mwezi Machi, Sierra Leone ilibatilisha marufuku yake ya wasichana wajawazito na kina mama wadogo kutohudhuria shule, miezi mitatu baada ya mahakama moja ya Jumuiya ya Kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi kutoa uamuzi kuwa hatua hiyo ni ubaguzi na ukiukaji wa haki ya mtoto ya kupata elimu.

Nchi hiyo kwa kipindi kirefu ilikuwa na tatizo la mimba za utotoni ambapo zaidi ya asilimia 35 ya wasichana chini ya umri wa miaka 18 walikuwa wamejifungua watoto mwaka 2013.

Na idadi hiyo iliongezeka hadi asilimia 65 katika baadhi ya sehemu wakati wa janga la Ebola mwaka 2014/2015 shule zilipolazimika kufungwa.

Jambo lililosababisha serikali nchini humo kuchukua hatua ya kutangaza rasmi sera ya kupiga marufuku wasichana waliopata ujauzito kurejea shuleni kwa misingi kuwa hilo lingehamasisha wasichana wengine kuona kupata ujauzito ni jambo la kawaida.

Takwimu rasmi zinaonesha kuwa mwaka 2015, wasichana wasiopungua 3,000 waliathirika na marufuku hiyo wengine wakisema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.

Ingawa vituo vya muda vya kusoma vilitengwa kwa ajili ya wasichana hao, walikutana mara tatu tu kwa siku kufundishwa masomo manne pekee; Mwaka 2019, mahakama hiyo ilisema kuwa vituo hivyo pia ni ubaguzi na kuagiza vifungwe mara moja.

Kubadilisha fikra za watu

Na mambo yamekuwa tofauti mwaka huu kwasababu serikali imelitambua hilo kama tatizo. Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio alitangaza ubakaji kama tatizo la kitaifa linalohitajika kushughulikiwa kwa dharura na kuahidi kuchukua hatua.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

1px transparent line

Kwa mara ya kwanza karibu wasichana wajawazito 1,000 walifanya mtihani wa kitaifa.

Back of Fatu, the 13 year old girl who is pregnant after suffering sexual abuse

Chanzo cha picha, Waves

Maelezo ya picha, Maoni yameanza kubadilika Sierra Leone huku wasichana wajawazito wakianza kurejea shuleni

Wazazi wa Fatu Francis na Iye wanafuraha kwasababu msichana wao anaweza kuendelea na masomo licha ya kwamba ni mjamzito.

Wanasema kuwa kuondolewa kwa marufuku hiyo kumebadilisha mtazamo wao na ni matumaini yao kwamba Fatu atapata elimu, lakini kama hilo lingetokea mwaka mmoja uliopita, hali ya mtoto wao ingemaanisha kumuoza tu.

Fatu mwenyewe anasema maisha yamekuwa magumu kidogo shuleni.

Anachoka mara moja na pia anakuwa na wakati mgumu wa kukaa darasani kwa muda mrefu, "Siwezi kukaa darasani muda wote".

"Marafiki hawanichagui tena katika michezo yao hasa wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana, kwasababu wanasema sitashiriki kikamilifu".

Lakini anaongeza: "Ningependa kuendelea kwenda shuleni nitakapojifungua kwa kuwa nataka kumaliza shule na kuelimika.

"Ninaimani siku zijazo nitakuwa muuguzi. Nikiwa mkubwa nataka kuwa mshauri wa wasichana wadogo na kina mama wenye umri mdogo."

Msimamo mkali wa Tanzania

Shirika la Equality Now, ambalo liliwasilisha kesi kupinga marufuku ya wasichana wajawazito kuhudhuria shule nchini Sierra Leone sasa limeanza kukabiliana na Tanzania.

Shirika hilo liliwasilisha kesi yake mwezi jana katika mahakama moja ya Afrika yenye kutetea haki za watoto, likiwa na matumaini ya kubadili uamuzi wa Tanzania.

Lakini kulingana na Judy Gitau wa shirika la Equlity Now, kesi ya Tanzania ni tofauti kabisa na Sierra Leone na hakuna uhakika wa kupatikana kwa matokeo sawa na hayo.

"Nchini Sierra Leone, sera hiyo ilikuwa ni ya kitambo na haikuwa inaungwa mkono wa uongozi," amesema Gitau.

"Lakini wakati nchi zingine zimekuwa zikipinga hatua kama hiyo, uongozi wa Tanzania umeamua kutekeleza sheria hiyo miaka ya hivi karibuni."

Anarejelea onyo lililotolewa na Rais John Magufuli mwaka 2017: "Maadamu mimi ndiyo rais… hakuna msichana mjamzito ambaye ataruhusiwa kurejea shuleni. Ukipata ujauzito, ndio mwisho wako".

Alipigiwa makofi aliposema katika mkutano mmoja nje ya Dar es Salaam: "Ikiwa ni turuhusu wasichana kurejea shuleni, siku moja tutaona wasichana wote wa darasa la kwanza wakienda nyumbani kunyonyesha watoto wao." Pia alitishia kifungo cha miaka 30 jela kwa wanaume wanaowatia mimba wasichana wadogo.

Students of Al-Haramain secondary school attend a class on their first day of re-opened school in Dar es Salaam, Tanzania, on June 1, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nusu ya wanafunzi 60,000 wanaoacha shule nchini Tanzania huwa ni wasichana

Tanzania ni moja kati ya nchi zenye idadi kubwa ya mimba za utotoni duniani.

Kulingana na UNFPA, mwaka 2016, mmoja kati ya wasichana wanne wenye umri wa miaka 15 - 19 ama alikuwa mjamzito au amejifungua.

Data ya serikali mwaka huo huo ilionesha asilimia 36 ya wanawake walikuwa wameolewa kabla ya kufika umri wa miaka 18, huku asilimia 5 pekee ya wavulana wakiwa wameona kati ya umri huo.

Benki ya dunia ambayo ilitoa dola milioni 500 kwa Tanzania kama mkopo mwaka huu, imesema nusu ya wanafunzi 60,000 wanaoacha shule kila mwaka ni wasichana ambapo 5,500 hulazimika kuacha shule kwasababu ya kupata mimba za utotoni.

Aidha Tanzania imekiri tatizo hilo na kuanzisha programu shuleni za kutoa elimu zaidi ya afya ya uzazi.

Shirika la UNFPA limeripoti kuwa Tanzania inaweza kupoteza hadi dola bilioni 5.22 kwa mwaka kwasababu ya idadi ya wasichana wadogo wanaocha shule.

Aidha, shirika la Equality Now, linasema limetafuta suluhisho kwa zaidi ya miaka mitatu kwa serikali ya Tanzania ili iweze kuondoa marufuku hiyo bila mafanikio yoyote na sasa kuwasilishwa kwa kesi hiyo katika Mahakama ya Afrika ndiyo tegemeo la mwisho.

"Mchakato wa kisheria unaweza kuchukua miaka kadhaa," amesema msimizi wa shirika la Equality Now Judy Gitau. "Tunalifuatilia hata kama itachukua muda mrefu, ingawa tunaimani kuwa mchakato huu hautachukua muda mrefu sana kwasababu ya wasichana."

Pia unaweza kusikiliza:

Maelezo ya sauti, Magufuli: Ukishapata mimba ni kwaheri shuleni