Mazishi ya Ginimbi: Familia ya Genius Kadungure yafanya mazishi yake alikozaliwa

Chanzo cha picha, BBC
Mazishi ya Genius Kadungure al maarufu Ginimbi yamefanyika katika mji alikozaliwa wa Domboshava, nchini Zimbabwe.
Familia na marafiki zake walifika kutoa heshima zao za mwisho kwa mfanyabiashara huyo maarufu.
Marehemu ambaye alikuwa maarufu sana nchini Zimbabwe, alifariki kutoka na ajali ya barabarani katika barabara ya Liberation Legacy Way tarehe 8 November, 2020 pamoja na watu wengine watatu.
gari la Ginimbi liliungua moto baada ya kugongana na magari mengine
Ratiba ya mzishi ya Ginimbi

Ibada ya wafu ilianza saa tatu unusu kwa saa za Zimbabwe, ka mujibu wa ratiba ya mazishi
Wakati wa mazishi watu wafuatao walitoa risala zao kuhusu uhusiano na maisha yao na marehemu na nyakati za uhai wa Ginimbi.
- Baba - Baba ya Ginimbi kumzungumzia mwanae
- Mama - Wakati wa hotuba kwa niaba ya mama yake Ginimbi ,lakini mfanyabiashara huyo Januari mwaka huu na hivyo mama yake mdogo alitoa hotuba kwa niaba yake
- Sekuru - Mjomba wake Ginimbi
- Ambuya - Bibi (nyanya) kuzungumza kumuhusu Ginimbi .
Orodha ya jinsi watu walivyotakiwa kufuatana kutoa hotuba zao katika mazishi ilikuwa kama ifuatavyo :
- Tete - Dada yake Ginimbi au shambazi
- Dada yake Ginimbi
- Mwana
- Munkuru
- Mukwesha
- Muroora
- Wafanyakazi wenzake
- marafiki
- Sahwira

Tunachofahamu kuihusu familia ya Ginimbi
Genius Kadungure aka Ginimbi alizaliwa tarehe 10 Oktoba 1984. Alizaliwa katika mji wa Domboshava katika familia ya watu wanne.
Mama yake Ginimbi Juliana Mubaiwa alifariki dunia Januari 2020 baada ya kuugua saratani . Kaka yake Andrew alifariki mwaka 2019.
Jumapili , baada ya kifo chake, Anderson Kudungure baba yake mfanyabiashara huyo maarufu alifanya mahojiano na gazeti la Daily mail na kusema kuwa walikuwa hawajaonana na Ginimbi , licha ya kwamba walikuwa ni majirani na eneo la Nyamande lililopo Domboshava ambako Genius alijenga nyumba yake.
"Alipenda kuendesha kwa kasi kubwa ,"alisema baba yake. "Niliposikia kuhusu ajali yake , nilijua hawezi kusurika, kutokana na ninavyomjua anavyoendesha gari ka kasi kubwa.
Tangu kifo chake kilipotokea, mwili wa Ginimbi umekuwa katika kasri lake lililopo Domboshava, ambalo baadhi ya watu wa familia yake wamekuwa wakisema panafaa kujengwa kujengwa kaburi kubwa kwa ajli ya mpendwa wao.

Chanzo cha picha, INSTAGRAM/MOANA_TY22
Awali marafiki zake walimtetea kuhusu chanzo cha utajiri wake
Baadhi ya watu walisema kuwa Ginimbi alikuwa na nyoka ambaye alikuwa akimtemea pesa; lakini baadhi ya marafiki wa Ginimbi wamejitokeza na kumtetea wakisema kuwa ni kwanini watu hawakujiuliza chanzo cha utajiri wake wakati alipokuwa hai?.

Chanzo cha picha, GENIUS GINIMBI KADUNGURE/INSTAGRAM
Mmoja wa marafiki wake, Ronald Muzambe amesema katika taarifa yake: "kila mtu anayemfahamu Ginimbi hadi alipofikia umri wa miaka 36 anamuelewa kuwa alikuwa na vyanzo vingi vya utajiri. Hakuna yeyote ambaye alishawahi kuuliza ni vipi alipata utajiri alipokuwa hai, ni kwanini wanaongea mambo tofauti kumuhusu wakati sasa amekufa ?"
Muzambe anasema watu wamuache marehemu afe kwa amani. Ninawashauri watu "wawe na hisia za kiutu angalau kidogo, ili kumuaga vizuri na kuonyesha heshima kwa rafiki zake na familia yake katika wakati huu mgumu ."
Ginimbi alikuwa mtu maarufu tangu alipokuwa na umri wa miaka 26 akiwa muuzaji wa gesi ya petroli (LP) . Tangu wakati huo alikuwa ni aliyependa kujifurahisha na marafiki zake kwa kufanya sherehe ndogo ndogo za mara kwa mwara wakati ule, kabla ya kuanza kufanya sherehe kubwa.
Magari ya Genius Ginimbi

Chanzo cha picha, GENIUS GINIMBI KADUNGURE/INSTAGRAM
Kulingana na gazeti la Times Live, miongoni mwa magari yake ambayo ameyaacha ni pamoja na :
- Rolls-Royce Ghost (2016 model)
- Rolls-Royce Ghost (2020 model)
- Rolls-Royce Wraith (ambalo alikufa akiwa analiendesha)
- Bentley Continental GT (2014 model)
- Bentley Continental GT W12 (2020 model)
- Bentley Bentayga
- Bentley Mulsanne
- Lamborghini Aventador S Coupe
- Ferrari 488 Spider
- Mercedes G Wagon Brabus (2016 model)
- Mercedes G Wagon G63 (2020 model)
- Range Rover Vogue Autobiography (2019 model)
- Range Rover Sport SVR (2019 model)
- Range Rover Sport Lumma (2017 model)
- Range Rover Sport (2018 model)
- Range Rover Velar (2018 model)
- Mercedes-Benz S Class (2014 model)
- Mercedes-Benz S Class (2019 model)
BBC Hata hivyo haikuweza kupata chanzo huru cha kuthibitisha taarifa zilizotolewa na gazeti la Times Live ingawa Ginimbi anatambuliwa kuwa alikuwa ni mtu aliyerkuwa na uraibu wa kununua magari.
Magari haya ni ya kifahari na alinunua mfano aina tofauti za BMW, Jaguar na Lexus.
Genius kanungre aka Ginimbi ni alikuwa nani ?
Genius Kadungure maarufu Ginimbi alikuwa mtu maarufu sana nchini Zimbabwe akiwa mlimbwende na mfanyabiashara.
Pia alikuwa mwanzilishi wa kampuni ya kuuza gesi ya Pioneer gases ambayo ina kampuni nchini Botswana , Afrika Kusini na Zimbabwe. Mnamo tarehe 8 mwezi Novemba 2020, Ginimbi aliaga dunia baada ya ajali ya gari .
Gari hilo aina ya Rolls Royce lilidaiwa kugonga gari jingine na kukosa mwelekeo na kugonga mtu kandokando ya barabara. Kufuatia hatua hiyo gari hili liliwaka moto na kuungua.

Chanzo cha picha, Kadungure/Instagram
Kulingana na mashahidi Ginimbi alidaiwa kutolewa akiwa hai lakini akafariki muda mchache baadaye. Abiria wengine wawili waliokuwa ndani walisalia ndani yake na kuchomeka hadi mauti yao.
Biashara
Kadungure alidaiwa kuanza biashara ndogo ndogo akiwa na umri wa miaka 17 huku akiwa wakala wa gesi .
Alianzisha kampuni ya gesi ya Pioneer ambayo ni miongoni mwa makampuni ya Kundi la biashara za Piko.
Kampuni hiyo inauza gesi , kwa wafanyibiashara , kwa umma na madukani.
Maisha yake ya kibinafsi
Mwaka 2014 alidaiwa kufunga ndoa na mfanyabiashara mmoja lakini kufikia mwaka 2018 alifichua kwamba yeye na mfanyabiashara huyo wamewachana. Hatahivyo waliendelea kufanya biashara pamoja.
Sherehe za kukata na shoka
Kadungure alikuwa maarufu kama kijana aliyependa kula 'bata' na kufanya shrehe za kukata na shoka .
Mwaka 2010 , alifanya sherehe iliogharimu US$17,000 .

Chanzo cha picha, Kadungure/Instagram
Sherehe hiyo ilivutia marafiki zake kutoka mji mkuu wa Harare huku wageni wakipewa mivinyo ya gharama ya juu kwa siku tatu mfululizo.
Miaka miwili baadaye 2012 alifanya sherehe nyengine ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa iliofanyika mjini Botswana .
Sherehe hiyo ilidaiwa kugharimu $32,000 wakati huo. Mwaka 2013, Kadungure alidaiwa kufanya sherehe nyengine ya siku tatu nyumbani kwao huko Domboshava ili kusherehekea jumba lake jipya katika eneo hil













