Uchaguzi wa Seychelles : Jinsi kasisi alivyopanda na kuwa rais

katika jaribio lake la sita Wavel Ramkalawan, kasisi wakanisa la Kianglikana, amekuwa rais wa Seychelles na kumaliza miongo ya upinzani, lakini Tim Ecott anaripoti kuttoka visiwa hivyo vilivyomo katika Bahari ya Hindi kwamba atatakiwa kuliunganisha taifa.

"Baada ya miaka 43 tumepata demokrasia, barabara imekuwa ndefu na sasa tutavuna matunda yake ."

Kulikua na maneno machache ya kuelezea sifa zake katika hotuba ya kuapishwa kwa Wavel Ramkalawan alipokuwa akionekana kujikita zaidi katika kuwakaribisha wananchi na wageni wa heshima waliokuwa wameketi katika viwanja vya Ikulu.

Kuchaguliwa kwake ni mwanzo wa mabadiliko kwa visiwa hivyo, ambako urais umekuwa ukitawaliwa na chama kimoja tangu mwaka 1977.

Mbele ya jengo la kifahari la ukoloni la Victoria na gwaride la heshima la jeshi, Wavel mwenye umri wa miaka 58 aliapishwa na jani mkuu Jumatatu.

Rais mpya ni mchungaji aliyetawazwa wa kanisa la Kianglikana, na haishangazi kwamba ujumbe wake wote ulikua ni wa amani, uvumilivu na wa kuwaomba Waseychelles kufanya kazi pamoja kwa ajili ya umoja wa taifa, na kuzuwia mgawanyiko wa miaka mingi sana wa mzozoz wa kisiasa.

Akimshukuru rais anayeondoka madarakani Danny Faure kwa kuyaweka wazi mazungumzo ya kisiasa kwa miaka michache iliyopita, Bw Ramkalawan alisisitizia haja ya kuvumiliana miongoni mwa watu wa seychelles na akatoa wito wa kile alichokiita kurejea kwa utu miongoni mwa jamii ambapo kila mtu anamsalimia mwenzake habari za asubuhi na ambapo tofauti za asili na kijamii nina wekwa kando.

"Seychelles," alisema rais mpya , "inapaswa kuwa mfano wa kuvumiliana kwa dunia nzima. Sisi ni visiwa 115 vidogo katika bahari ya India, lakini hatuna uhusiano mzuri.

"Tutaimarisha mahusiano ya urafiki na nchi zote, na kukaribisha msaada kutoka kwa washirika wetu wa kimataifa wowote watakavyokua ."

Nyuma ya hisia za kikristo alizozionesha rais mpya kuna chuma cha siasa.

'Mwanasiasa wa madhabahuni'

Hili lilikuwa ni jaribio lake la sita, safari ambayo aliianza wakati alipogombea kwa mara ya kwanza wadhifa huo 1998.

Aliingia siasa miaka kadhaa mapema, na alikosolewa na serikali kwa kufanya kile walichokiona kama taarifa ya kisiasa kutoka madhabahuni wakati wa enzi ya chama kimoja.

Alikuwa akikaribia kupata ushindi wa urais mara kadhaa, na mwaka 2015 alishindwa na James Michel kwa kura 193 tu katika awamu ya pili ya upigaji kura.

Akielezea kuhusu miaka yake katika upinzani , na kushindwa kwake mara tano katika uchaguzi wa urais, Bw Ramkalawan alitumia nukuu ya Nelson Mandela: "Mshindi ni muotaji ambaye hakati tamaa ."

Licha ya ujumbe mzuri katika hotuba yake ya kuapisgwa, bado kuna migawanyiko ndani ya jamii ya Waseychelles.

Ni miaka 43 tangu visiwa hivyo vilipokabiliwa na ghasia za mapinduzi ya Albert René, ambaye alipindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia James Mancham, mtu aliyeongoza visiwa hivyo kupata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1976.

Wakati akitoa wito wa amani na utulivu, Rais Ramkalawan alitembelea mchoro wa Gerard Hoarau, mpinzani wa René aliyeuawa mjini London mwaka 1985, na ambaye wauaji wake hawajatambuliwa.

Katika historia zake zote za miongo tangu uchaguzi, Seychelles yenye idadi ya watu 97,000-kwa sasa inakabiliwa na changamoto.

Uchumi wake unategemea kwa kiasi kikubwa utalii, ikitrembelewa na watalii takriban 350,000 kila mwaka wakiliingizia 65% ya pato la ndani ya nchi -GDP.

Covid-19 imepunguza idadi ya watalii wanaowasili , na uchumi umekwishapungua kwa karibu 14%.

Zaidi ya hayo, shirika lisilo la kiserikali linakadilia kuwa kati ya 10% ya watu anaofanya kazi , 6,000 kati yao wana uraibu wa mihadarati aina ya heroin, na wengi wanaitegemea serikali kwa mpango wa matibabu.

Pamoja na kushinda urais, chama cha Bw Ramkalawan, Linyon Demokratik Seselwa (LDS), kimeshinda wingi wa viti vya wabunge katika bunge la taifa.

Watakuwa na viti 25 katika bunge la 10 la United Seychelles . Hatahivyo , aliwatahadharisha wabunge wake dhidi ya kuwa watu walioridhika na kusahau kufuatilia masuala muhimu ya kitaifa.

" Hatuwezi kukaa tu eti kwasababu tumeshinda tu ," alisema. "Tunahitaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kutekeleza kile ambacho watu wet wanastahili ."

Ameahidi kwamba chini ya urais wake "hakuna yeyote atakayekuwa juu ya sheria ".

Hata kama mfumo wa chama kimoja ulivunjwa zaidi ya miaka 25 iliyopita, idadi ndogo ya Waseychelles wasomi wamekua wakishikilia nyadhifa muhimu na watu wamekua wakiteuliwa kwa misingi ya ufuasi wa chama kuliko uwezo wa mtu kikazi.

Kimataifa rais mpya huenda pia akakabiliwa na changamoto ya mazungumzo tata ya siasa za kijiografia za mataifa ya bahari ya Hindi.

Siku moja tu baada ya uchaguzi alirejelea kusema kwamba hadhi ya visiwa sio ya kuuzwa.

Uhasama wa India na China

Alikuwa akielezea kuhusu mkataba uliofanywa kati ya Rais Faure wa kuchukua udhibiti wa kisiwa kilichopo mbali na katika bahari yaIndia kama ngome ya jeshi lake la majini.

Bw Ramkalawan amekataa kushawishika kuwa hili litaendelea

Hatahivyo, katika miaka ya hivi karibun kanda hiyo limekuwa ni eneo la uhasama wa kidiplomasia kati ya India na China.

India ilikuwa na matumaini ya kutumia kisiwa cha Seychelles cha Assumption kukabiliana na uhasama wa ngome ya jeshi ya China iliyopo Djibouti.

Kwa pamoja China na India zimetoa misaada mikumbwa kwa Seychelles, ingawa mdhamini mkarimu zaidi ni Milki za kiarabu -UAE -hasa Abu Dhabi.

Hatahivyo, ujusiano mpya wa kidiplomasia huenda ukaimarika zaidi kati ya Ramkalawan na India hasa kwasababu babu yake ambaye alimia Seychelles akitokea India katika jimbo la Bihar.

Ushindi wa LDS umepokelewa kwa amani katika visiwa vya Seychelles, na watu wengi wanaamini kuwa ni wakati wa filozofia mpya katika Ikulu.

Rais Ramkalawan alisema wazi kwamba nia yake ni kuleta maridhiano ya kitaifa na kwa vyama vyote kujiunga katika kuwasaidia vijana kupata maisha bora ya siku zijazo.

"Tuwe katika chama chochote kile" alisema , "sasa tunapaswa kuweka juhudi zetu sasa katika kuwa Waseychelles pamoja."