Uchaguzi Tanzania 2020: Bernad Membe aendelea kuwania urais ACT licha ya viongozi wake kumnadi Lissu

"Mimi ni Mgombea wa urais wa chama chetu na ninakwenda kukipeleka kwenye uchaguzi mkuu"

Chanzo cha picha, MEMBE/TWITTTER

Maelezo ya picha, "Mimi ni Mgombea wa urais wa chama chetu na ninakwenda kukipeleka kwenye uchaguzi mkuu"

Mgombea urais wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT- Wazalendo Bernard Membe amejitokeza na kusisitiza kuwa yeye yungali kwenye mbio za kuwania urais wa nchi hiyo.

Membe amejitokeza baada ya ukimya wa takribani majuma mawili ambapo viongozi wakuu wa chama chake Zitto Kabwe na Maalim Seif Shariff Hamad wamekuwa wakimnadi mgombea wa Chadema, Tundu Lissu katika tiketi ya urais dhidi ya mgombea wa chama tawala CCM rais John Magufuli.

"Mimi ni Mgombea wa urais wa chama chetu na ninakwenda kukipeleka kwenye uchaguzi mkuu," Membe amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Unaweza kutazama mazungumzo yake na waandishi wa habari

Maelezo ya video, Mgombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Bernard Membe asema yeye ni mgombea

Kuhusu viongozi wake kumuunga mkono Lissu Membe amesema: "Sisi tupo wa moja waliosema ni individuals (watu binafsi) na tumeyamaliza, chama cha ACT tuna mgombea, na ni mimi. Wapo watu ndani ya Chadema hawatampigia Lissu kwa hiyo hata Zitto na Maalim ni ACT lakini wanaweza wasinipigie kura ila tunaamini watabadilisha maamuzi yao ila tupo pamoja."Kwa mujibu wa Membe, nadharia kwamba wapinzani wakiungana wanaweza kukiangusha chama tawala haijawahi kufanikiwa Afrika, japo kwa Tanzania anaamini wamefanikiwa kuleta mpasuko kwenye chama tawala CCM.

"Nilitaka kukabiliana na Rais aliyeko madarakani mimi peke yangu washukuru walinifukuza. Chama Cha Mapinduzi kimepasuka na kipindi chote cha ukimya wangu nimewapigia simu na bado liko wazi. Tunachotaka ni kukipasua Chama Cha Mapinduzi kwa kuwapa mlango wa heshima wa kutokea."

Maelezo ya sauti, ACT Wazalendo: CCM haitaondoka uongozini iwapo Tundu Lissu na Membe watagombea wakiwa mbal

Membe anaamini yeye na chama chake kina ushawishi: "Tutafunga bao la dakika ya 89 ACT Wazalendo hatuna matatizo. Chama hiki kiko imara na kitasima kama chama na sio kama tawi la chama kingine... tumefanya kazi huku chini sasa tunakuja juu watanzania niwaambie tunaenda kushinda."

Msimamo wa viongozi wa ACT Wazalendo ukoje?

Wakati Membe akitangaza kuendelea kuwania urais, viongozi wake wakuu Zitto na Maalim Seif wanatarajiwa kuwa katika mkutano wa kampeni wa Lissu mkoani Kilimanjaro hii leo.

Ijumaa ilopita Zitto alitoa tamko kuwa kura yake itaenda kwa Lissu na kuwataka wanachama wote wa chama hicho kufanya hivyo.

Wagombeaji urais Tanzania

  • Anawania awamu ya pili na ya mwisho madarakani.
  • Kampeni yake imejikita kati mafanikio yake kwenye sekta za madini, ujenzi wa miundombinu, elimu bure na mapambano dhidi ya rushwa.
  • Awamu yake ya kwanza pia imekosolewa kwa ukandamizaji wa haki za binadamu.
  • Ni mgombea wa chama tawala ambacho kipo madarakani toka uhuru, hivyo anatarajiwa kushinda uchaguzi huu.
  • Magufuli, 60, alichaguliwa Bungeni mara ya kwanza 1995 na kupata umaarufu akihudumu katika wizara ya ujenzi alipopata jina la utani la tingatinga.
  • Alimiminiwa risasi na wasiojulikana Setemba 2017, japo amenusurika shambulio hilo limemuacha na majeraha ya kudumu.
  • Alirejea Tanzania mwezi Julai 2020 baada ya miaka mitatu ya ughaibuni ili kugombea urais kupitia chama kikuu cha upinzani Chadema.
  • Kampeni yake imejikita kwenye kuheshimu haki za binadamu na kukuza uchumi wa watu.
  • Mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu alichaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 na 2015 na kuhudumu kama mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.
  • Alituhumiwa ndani ya CCM kuwa alikuwa na mipango ya ‘kumhujumu’ Magufuli kwenye uchaguzi wa ndani ya chama 2020.
  • Sasa ni mgombea wa ACT, ambacho kimeweza kukua kutoka kuwa chama kidogo mpaka moja ya mihimili ya upinzani kwa kipindi kifupi.
  • Kachero mstaafu, alihudumu kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya rais mstaafu Jakaya Kikwete toka 2007 mpaka 2015.
  • Mwanasiasa mwandamizi wa upinzani ambaye amegombea urais katika chaguzi zote kasoro mwaka 2015.
  • Alikuwa kinara wa upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 na 2005.
  • Ushawishi wake ndani ya upinzani umepungua baada ya migogoro ya ndani ya CUF iliyolazimisha kundi hasimu kwake kujitoa chamani.
  • Profesa Lipumba ni moja ya wasomi maarufu wa uchumi nchini Tanzania ambapo alisoma shahada zake za juu kutoka chuo kikuu maarufu cha Stanford, Marekani.

Anasema kamati ya Uongozi ya Chama chake cha ACT imeshauriana na kuona kuwa huu ni mwaka wa kihistoria kwa Watanzania, mwaka wa kuamua hatma ya Maisha yao.

"Kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe nitampigia kura kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai Lissu.

Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda mgombea wa chama tawala."

Zitto alisema hatua hii ya kumuunga mkono mgombea wa chama kingine imesukumwa na dhamira yake ya kuleta mabadiliko ya kumchagua Lissu.

Kabwe ameyaeleza hayo katika hotuba yake ya kampeni Bangwe, Kigoma na kuwataka wafuasi wa chama hicho pia kumpigia kura Lissu.

act

Mwezi Septemba Mwenyekiti wa ACT Maalim Seif Shariff Hamad, alitangaza kumuunga mkono Lissu kwenye kinyang'anyiro cha Urais.

ACT katika kinyang'anyiro cha urais imemsimamisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Benard Membe, ambaye mpaka sasa hajajitokeza hadharani kumuunga mkono Lissu.

act

Mara baada ya Maalim Seif kutangaza kumuunga mkono Lissu, Mmembe alisisitiza kuwa yeye ndiye mgombea halali wa ACT.

Chadema kwa upande mwengine kimetangaza kumuunga mkono Maalim kwenye kinyang'anyiro cha urais wa Zanzibar.

Hata hivyo, ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa vimeoynya juu ya ushirikiano wa vyama hivyo ikisema ni kinyume na sheria.