Kwanini kikosi cha Sars kinachukiwa Nigeria?

A demonstrator holds a banner during a protest against alleged police brutality, in Lagos, Nigeria

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 3

Maandamano yaliotanda kote nchini Nigeria kwa sababu ya kikosi maalum cha polisi cha kukabiliana na wizi wa mabavu (Sars)

ni ishara kwamba vijana wanapaza sauti yao wakidai mabadiliko katika nchi hiyo maarufu barani Afrika ambayo imekumbwa na sifa ya utawala mbaya tangu ilipopata uhuru wake miaka 60 iliyopita.

Licha ya kumlazimisha rais kuvunja kikosi hicho cha polisi, bado wanadai mabadiliko kamili katika kikosi kizima cha polisi na maafisa waliotekeleza dhulma wakabiliwe na mkono wa sheria.

Lakini ni zaidi ya madai hayo kwa sababu wimbi hilo la maandamano limetoa fursa kwa vijana wengine kote nchi humo kuonesha kutoridhika kwao na serikali.

A demonstrator stands atop a vehicle and shouts slogans as others carry banners while blocking a road leading to the airport, during a protest over alleged police brutality, in Lagos, Nigeria October 12, 2020.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waandamanaji wamefunga njia mjini, Lagos

Mitaani, wanaoandamana ni vijana ambao wengine wametia nywele rangi, wako waliotoboa masikio na hata kuchora tattoo mwilini.

Ni kundi ambalo ni rahisi sana kwa maafisa wa usalama kulipachika jina la wahalifu, lakini ukweli ni kuwa hawa ni vijana wanaofanyakazi kwa bidii ambao hawategemei serikali.

Wengi wao wana umri wa kati ya miaka 18 na 24 na katika maisha yao hawajawahi kuwa na umeme thabiti, hawakupata elimu ya bure nchini mwao huku masomo yao chuo kikuu yakirefushwa kwasababu ya wahadhiri kushiriki maandamano ya mara kwa mara.

Matatizo wanayopitia mikononi mwa polisi kunaakisi yale ambayo vijana wa taifa hilo wanayapitia kwa ujumla.

"Ni kipi ambacho nimenufaika nacho tangu nimezaliwa katika nchi hii ?" Victoria Pang, 22, aliyehitimu ameuliza, aliyeshiriki moja ya maandamano katika mji mkuu wa Abuja - na mmoja kati ya wanawake ambao wamekuwa mstari wa mbele katika maandamano.

Policeman talking to protesters

Chanzo cha picha, Reuters

"Wazazi wetu wanasema kuna wakati mambo yalikuwa mazuri lakini sisi hatujawahi kushuhudia hilo," alisema.

Kwanini kikosi cha Sars kinachukiwa?

Maafisa wa polisi nchini Nigeria kwa ujumla wana sifa ya ufisadi, kutenda unyama na kutojali haki za binadamu lakini watu hapa wanahisia kali dhidi ya kundi la Sars ambalo limekuwa na tabia ya kutesa vijana.

Vijana wanaosemekana kujiweza kifedha, yaani wenye gari nzuri, kipakatalishi au waliochora 'tattoo' au kufuga 'dreads' hufuatwa sana na maafisa wa kikosi cha Sars.

"Kuna wakati watu wa mahali ninapoishi waliita mafisa wa polisi kunikamata kwasababu tu kila wakati nilikuwa nyumbani na ninaishi maisha mazuri," Bright Echefu, 22, mtaalamu wa utengenezaji tovuti aliyeungana na waandamanaji amesema katika mazungumzo na BBC huko Abuja.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kwa kipindi kirefu michoro ya tattoo, nywele za dreadlocks, kutoboa masikio na mitindo ya maisha inayosemekana kinyume na maadili kumechukiliwa kama kushindwa kujukumika kwa familia, mashirika ya kidini, jamii na hata shule.

"Kuchora tattoo kwenye mkono wangu kunanihusisha vipi na uhalifu?" ameuliza Joy Ulo, raia mwenye shahada aliyeandamana.

Demonstrators hold banners during a protest against alleged police brutality, in Lagos, Nigeria

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vijana ni wengi zaidi Nigeria

Rais Muhammadu Buhari, 77, ambaye siku za nyuma aliwahi kuelezea raia wa Nigeria kama "wavivu" kwa hadhira ya kimataifa hivi majuzi alishauri wale walioathirika na janga la virusi vya corona kiuchumi kugeukia kilimo kwasababu bado wana nguvu.

Ingawa kwa kiasi fulani maandamano yanayoendelea yanaonekana kupangwa, watu wanaoonekana kuratibu hatua kuchukuliwa kwenye mtandao ya kijamii hawataki kutambulika viongozi.

Wameonekana kuratibu kupatikana kwa maji, chakula, mabango hadi namna ya kuachiliwa kwa dhamana kwa waliokamatwa.

Pesa imepatikana kupitia mchango - baadhi ni ufadhili kutoka nje ya nchi hasa makampuni ya teknolojia na habari ambao wanaweza kulengwa kiurahisi na maafisa wa usalama.

Woman holding a bell

Chanzo cha picha, Reuters

Wanaoratibu ambao hawatambuliki rasmi wamekataa kuchagua viongozi wa vuguvugu hilo na kusema kwamba hawataki majadiliano yoyote na serikali.

Lakini ukweli ni kwamba kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa maandamano hayo kumetokana na watu mashuhuri na washawishi katika mitandao ya kijamii hass Instagram, Snapchat na Twitter.