Mzozo wa Irael na Palestina: Je mkataba wa amani kati ya Israel na UAE utamaliza mzozo

Picha za Benjamin Netanyahu na Mtawala wa Abu Dhabi Mwna Mfalme Mohammed bin Zayed Al Nahyan

Chanzo cha picha, Reuters/Getty Images

Maelezo ya picha, Benjamin Netanyahu na Mwana Mfalme Mohammed Al Nahyan walifikia mkataba huo chini ya usaidizi wa Marekani

Saa kadhaa baada ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu,(UAE) kufikia mkataba utakaofanya kuwa rasmi uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya Israel kukubali kusitisha mpango wenye utata wa kuzifanya kuwa makazi ya Kiyahudi maeneo ya ukanda wa magharibi yanayokaliwa na Wapalestina.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alisaidia nchi hizo kufikia mkataba huo aliutaja kuwa wa "kihistoria" na mafanikio makubwa kuelekea upatikanaji wa amani.

Mpaka sasa Israel haina uhusiano wowote wa kidiplomasia na nchi za Ghuba na Uarabuni.

Lakini changamoto ya pamoja kuhusu Iran imechangia kuwepo kwa mawasiliano yasiyo rasmi kati ya nchi hizo mbili.

Viongozi wa Palestina wameripotiwa kushangazwa na hatua hiyo. Msemaji wa Rais Mahmoud Abbas amesema mkataba huo ni "uhaini", na kwamba balozi wa UAE anarudishwa nyumbani.

Rais Trump ameutaja mkataba wa maelewano kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Mwanamfalme mtawala wa Abu Dhabi Mohammed Al Nahyan kuwa "kihistoria halisi". Hatua hiyo Inaashiria mpango wa tatu wa amani wa Israeli na Waarabu tangu kutangazwa kwa Israeli uhuru mnamo 1948, baada ya Misri na Jordan.

"Kufuatia hatua hii natarajia Waarabu na chi za Kiislam kufuata mkondo wa Muungano wa Milki za Kiarabu," aliwaambia wanahabari katika ofosi yake ya Oval, akiongeza kwamba kutakua na hafla ya kutia saint mkataba duo Katina Ikulu ya White House wiki zijazo.

Awali, Rais aliweka tangazo la kufikiwa kwa mkataba huo katika Twitter yake, na kuandika Bw.Netanyahu kwa kiyahudi: "Siku ya Kihistoria."

Je huu ni ushindi wa sera ya kigeni?

Katika hotubba ya televisheni kwa taifa Bwana Netanyahu alisema kuwa "amechelewesha" mpango wa kuyafanya makazi ya Waiyahudi maeneo ya Ukanda wa Magharibi, lakini mpango huo bado unasalia "mezani". Hatua hiyo utatambua rasmi Ukanda wa Magharibi kuwa sehemu ya Israel.

"Sijafanyia mabadiliko mpango wangu kuhusu makazi ya ukanda wa magharibi kwa ushirikiano na Marekani. Inimejitolea kutimiza lengo hilo. Mpango huo haujabadilika. Nawakumbusha kwambi ni mimi niliyeleta suala kuhusu Judea na Samaria mezani. Na suala hilo bado lipo mezani," alisema.

Ramani

Bwana Netanyahu amesema kuwa Israel itashirikiana na UAE kutengeza chanjo dhidi ya virisi vya corona na pia kushirikiana Katina masala ya kawi, maji, uhifadhi wa mazingira na mambo mengine mengi.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema mkataba huu huenda ukawa ushindi wa sera za kigeni kwa Rais Trump, ambaye anagombea mutual wa pili wa Urais katika uchaguzi mkuu mwezi Novemba, na kumpatia ufanisi wa kibinafsi Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye anakabiliwa na mashitaka kuhusiana na madai ya ufisadi.

Uungwaji mkono wa viongizi wote wawili umeshuka kutokana na jinsi walivyoshughulikia janga la corona. Na nchini Israel, baadhi ya watu wanaotaka ukanda wa magharibu kutambuliwa rasmi kuwa makazi ya Kiyahudi wameelezea kughadhabishwa kwao na na tangazo hilo.

Balozi wa UAE nchini Marekani, Yousef Al Otaiba, amesema makataba kati ya nchi hiyo na Israel ni "ni ushindi wa kidiplomasia mashariki ya kati'', na kuongeza: "Ni maendeleo makubwa katika uhusiano wa Waarabu na Wayahudi hatua ambayo itapunguza mvutano na kubuni uhusiano mpya utakaoleta mabadiliko chanya".

Misri ilitia saini mkataba wa maelewano na Israel mwaka 1979, na Jordan in 1994. Mauritania pia ilifikia mkataba wa kidiplomasia na Israel mwaka 1999, lakinn ikisitisha makubaliano hayo yakasitishwa 2009.

Nini kilichofikiwa katika mkataba huo?

Katika wiki cache zijazo wajumbe wa Israel na UAE watakutana kutia saini mkataba kuhusu uwekezaji, utalii, safari ya ndege ya moja kwa moja, usalama, mawasiliano, teknolojia, kawi, afya , utamaduni, mazingira na kufunguliwa kwa ubalozi pande zote mbili miongoni mwa masuala mengine yatakayonufaisha nchi hizo."Kuwa na ushirikiano wa moja kwa moja kati ya nchi mbili zilizo na uwezo Mashariki ya Kati kutaimarisha uchumi na ni hatua ambayo italeta pamoja jamii eneo hili," taarifa ya pamoja ilisema.

Israeli pia "itasimamisha kutangaza umiliki wa maeneo yaliyoainishwa" katika ruwaza ya Rais Trump ya Amani kati ya Israeli na Wapalestina, ambamo aliunga mkono mpango wa Israeli wa kuzifanya makazi ya Kiyahudi katika maeneo ya Ukanda wa Magharibi pamoja na bonde la Jordon.

Wapalestina wameonya kwamba hatua kama hiyo itaharibu matarajio yao ya serikali huru ya uhuru na kukiuka sheria za kimataifa - msimamo unaoungwa mkono na jamii kubwa ya kimataifa.

Maelezo ya video, Coronavirus: Israel wanavyotumia Intelijensia kuwakamata wagonjwa wanaotoroka

Waziri wa mambo ya nje wa UAE, Anwar Gargash, amesema hatua ya nchi hiyo kutambua Israel "ujasiri mkubwa" ya kukomesha " zozo hatari" endapo Israel itayachukua makazi ya Ukanda wa magharibi.Alisema UAE ilifanya hivyo "kokomesha mpango huo, sio kuusitisha".

Alipoulizwa kuhusu ukosoaji wa Palestina dhidi hatua ya UAE, alitambua kuwa eneo hilo linakumbwa na uhasama mkubwa sana na kwamba anatarajia kusikia "kelele za kawaida". "Tulisumbuka juu ya hili," alisema, lakini mwishowe tuliamua "tuifanye".

Taarifa ya pamoja inasema Israel "sasa itaangazia juhudi za kupanua uhusiano na nchi zingine za uarabuni na ulimwengu wa Kiislam", na kwamba Marekani na UAE zitafanya kazi pamoja kufikia lengo hilo.

Muungano wa Milki za kiarabu na Israel pia zitaungana na Marekani kuzindua "Ajenda maalum ya Mashariki ya Kati", huku viongozi wa nchi hizo tatu wakiafikina kwamba "wana mtazamo sawa katika juhudi za kuleta amani na utulivu mashariki ya kati kupitia ushirikiano wa kidiplomasia, ujumuishaji wa uchumi, na uratibu wa karibu wa usalama ".

Nchi zingine zimepokeaje hatua hiyo?

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema "ilikuwa ombi langu kuwa mpango wa kuzifanya makazi ya kiyahudi maeneo ya ukanda wa magharibi hautaendelea na leo makubaliano ya kusitisha mpango umefikiwa katika hatua ambayo itakuwa mwanzo wa kuleta amani Mashariki ya Kati".

Rais wa Misri Egyptian Abdul Fattah al-Sisi amekaribisha mkataba huo huku waziri wa mambo ya nje Jordan Ayman Safadi, akisema makubaliano hayo huenda yakasaidia kupeleka mbele mashauriano ya amani yaliyokwama.

Lakini afisa wa ngazi ya juu wa Palestina, Hanan Ashrawi, amelaani makubaliano hayo, akisema UAE " imejitokeza hadharani kuonesha ushirikiano wa kisiri ama kufanya rasmi uhusiano kati yake na Israel" na kumwambia Mwana Mfalme Mohammed: "Natumai 'marafiki' zako hawatakusaliti."

Shirika la habari la Iran Tasnim, lililo na ufungamano na jeshi la ulinzi wa Iran, lilitaja mkataba huo kama "fedheha". Na mjini Gaza, kundi la wanamgambo wa Hamas liliutaja mkataba huo kama "usaliti dhidi ya watu wetu."

2px presentational grey line