Fahamu mpango wa Israel kuhusu eneo la Ukingo wa Magharibi

Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa anapanga kuchukua kwa ufanisi baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi- (West Bank) hatua itakayokua ya utata wa hali ya juu.
Ukingo wa Magharibiunaozungumziwa ni upi?
West Bank au Ukingo wa Magharibi, ni sehemu ya ardhi inayopatikana - kama jina linavyoeleza katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan na inapakana na Israel upande wa Kaskazini, Magharibi na Kusini. Mashariki kuna Jordan.
Ukingo wa Magharibi umekuwa chini ya uvamizi wa Israel tangu mwaka 1967 katika vita vya Mashariki ya Kati, lakini miongo ya mazungumzo magumu baina ya Israeli na Wapalestina -ambao wote wana haki ya eneo hilo-imesababisha suala la umiliki kutotatuliwa.
Kati ya Waarabu wa Palestina milioni 2.1 na milioni 3 (kulingana na vyanzo tofauti) wanaishi katika eneo la West Bank wakiwa na mamlaka machake ya kujitawala na wakiwa chini ya utawala wa jeshi la Israeli.
Ukingo wa Magharibi (ambayo haijumuishi Yerusalemu Mashariki) pia ni nyumbani kwa Wayahudi wa Israeli wapatao 430,000 wanaoishi katika makazi (na maeneo mengine 124 madogo) yaliyojengwa chini ya uvamizi wa Israeli.
Wengi miongoni mwa jamii ya kimataifa wanachukulia makazi hayo kama makazi yaliyojengwa kinyume cha sheria, chini ya sheria ya kimataifa, ingawa Israel na Marekani chini ya utawala wa Trump zinapinga hayo.
Je mpango wa "kuchukua eneo " ni nini? Na ni kwanini ni muhimu kuufahamu?
'Annexation' kama unavyoitwa ni neno linalotumiwa wakati taifa linapotangaza kuwa na mamlaka juu ya eneo lingine. Inazuiwa na Sheria ya Kimataifa. Mfano wa hivi karibuni ni Urusi kuifanya rasi ya Crimea ya Ukraine mwaka 2014.

Chanzo cha picha, AFP
Bwana Netanyahu amekwishasema mpango huo "sio wa kutwaa eneo Jingine", ingawa unahusisha kutekeleza mamlaka ya Israeli katika maeneo yanayopakana na Ukanda wa Magharibi (West Bank) ambayo yana makazi ya Wayahudi pamoja na eneo tambarare lililoko kando ya Ukanda wa Magharibi linalofahamika kama Bonde la Jordan.
Hatua hiyo inaweza kusababisha takriban 4.5% ya Wapalestina wanaoishi katika Ukingo huo wa Magharibi kujipata wakiwa ndani ya eneo litakalotwaliwa na Israeli.
Bwana Netanyahu amesema kuwa mamlaka ya nchi yake hayatatumiwa kwa Wapalestina wanaoishi katika Bonde la Jordan, na taarifa zinasema pia kwamba Wapalestina wengine wanaoishi katika maeneo yaliyochukuliwa na Israeli hawatakuwa chini ya sheria za Israeli.
Eneo lililopangwa kuchukuliwa na mamlaka ya Israeli (kulingana na ramani inayochorwa na Israeli pamoja na Marekani) linaweza kuwa ni 30% ya West Bank, kwa mujibu wa ripoti.
Bwana Netanyahu huenda akaanza kwa kutwaa makazi tu, ambayo yatakua ni 3% ya West Bank(Ukingo wa Magharibi). Asilimia 27% itakayosalia huenda isichukuliwe hadi Israeli itakapofanya maafikiano na serikali ya Marekani .
Lakini, Wapalestina wanataka eneo lote la West Bank - ambalo wanadai ni lao kihaki na kihistoria-kwa ajili ya taifa lao huru siku za usoni, pamoja na Ukanda wa Gaza.
Hatua yoyote ya Israel kuyafanya maeneo hayo kuwa sehemu yake, kutawaacha Watu wa Palestina na ardhi ndogo kwa ajili ya nchi yao wenyewe.
Kama mpango una utata sana, kwanini Israeli inataka kuutekeleza?
Israel inadai kuwa ina haki za kihistoria na kwa West Bank kama ardhi ya mababu ya Wayahudi. Pia inadai ina uwepo wake pale-hususan katika Bonde la Jordan-ni eneo muhimu ya kimkakati kwa ajili ya ulinzi wake.
Inasema kuwa makazi sio kikwazo cha amani na hilo litabaki kuwa sehemu ya Israeli chini ya mpango wowote wa amani na Wapalestina, iwe maeno hayo yametwaliwa au la.
Bwana Netanyahu kwa muda mrefu amekua akiongoza ujenzi wa makazi kupitia mpango wa kuchukua maeneo hayo anataka kuondoa hofu yoyote juu ya hatma yao, kitu ambacho kinamjenga katika ngome yake ya kisiasa.
Ni kwanini hili linazingumziwa sasa?
Hadi hivi karibuni, Bwana Netanyahu angekabiliwa na upinzani mkubwa miongoni mwa jamii ya kimataifa kwa hatua ya aina hiyo.
Hatahivyo, mpango wa Donald Trump wa amani baina ya Israeli na Wapalestina, uliofichuliwa mwezi Januari, unairuhusu Israeli "kujumuisha" makazi- ambayo ni hatua kali ikilinganishwa na misimamo ya awali ya Marekani juu ya mpaka wa amani baina ya pande mbili

Chanzo cha picha, AFP
Inawezekana kwamba Bwana Netanyahu anataka mpango wake wa kuchukua maeneo ya Ukingo wa Magharibi (West Bank) ukamilike kabla ya uchaguzi wa urais wa Marekani kufanyika mwezi Novemba ili itakapotokea kwamba mpinzani wa Trump Joe Biden anayeupinga atakaposhinda asirudishe nyuma sera ya Marekani.
Ni nini kitakachobadilika iwapo maeneo ya West Bank yatakua chini ya mamlaka ya Israel ?
Kwa mfano ikitokea( Israeli na Marekani bado wanajadili ni linin a ni vipi ), makazi na maeneo yanayoyazingira yatakua sehemu ya kudumu ya Israeli( walau kutokana na msimamo wa Israeli), .
Kubadilisha uamuzi huu kutahitaji uungaji mkono mkubwa wa walio wengi miongoni mwa Wabunge wa Israeli, jambo ambalo huenda lisiwezekane.
Kwa kawaida, sheria za Israeli tayari zinashughulikia suala la walowezi, ingawa si kwa Wapalestina, ambao wanafuata sheria za jeshi la Israeli tu na sheria ya Wapalestina, kwahiyo kutakua na mabadiliko madogo yatakayoshuhudiwa kutokana na hilo .
Moja ya tofauti muhimu zitakazosababishwa na kuchukuliwa kwa maeneo haya ni katika ujenzi wa makazi - moja ya maeneo yanayosababisha uhasama mkubwa baina ya Israeli na Wapalestina.
Kwa sasa, ujenzi na kuweka maeneo katika West Bank inahitaji idhini ya waziri wa usalama wa Israeli na waziri Mkuu, na inaweza kuchukua miezi au hata mwaka kupata idhini hiyo. Kufuatia Israeli mpango wa Israeli kuyafanya maeneo hayo kuwa ni yake , litakua ni suala la kieneo na itakua ni rahisi kwa Israeli kujenga huko.
Nje ya maeneo yanayotaka kuchukuliwa na Israeli, jeshi la Israeli litaendelea kuyadhibiti - jambo ambalo baadhi ya Wapalestina wanasema limenyima kizazi chao haki zao za kimsingi za kiraia
Je dunia inasema nini kuhusu mpango wa Israeli?
Kwa kiasi kikubwa, Israeli imekua ikionywa na rafiki sawa na mahasimu wake kwamba isiendelee na mpango wake wa kuyaweka maeneo yanayokaliwa na Wapalestina chini ya mamlaka. Kuna hofu kwamba hatua ya aina hiyo itaufanhya mpango wa amani baina ya Israeli na Wapalenstina kuwa mbali sana kufikiwa
Wapalestina wanatoa wito wa kuwepo kwa shinikizo la ndani ya nchi ili kuivunja mipango ya Netanyahu, na Waziri wao mkuu amesema wanaweza kujitangazia uhuru wao kwa eneo lote la Ukingo wa Magharibi iwapo Israel itachukua ardhi pale.

Chanzo cha picha, Reuters
Moja ya tofauti muhimu zitakazosababishwa na kuchukuliwa kwa maeneo haya ni katika ujenzi wa makazi - moja ya maeneo yanayosababisha uhasama mkubwa baina ya Israeli na Wapalestina.
Kwa sasa, Currently, ujenzi na kuweka maeneo katika West Bank inahitaji idhini ya waziri wa usalama wa Israeli na waziri Mkuu, na inaweza kuchukua miezi au hata mwaka kupata idhini hiyo. Kufuatia Israeli mpango wa Israeli kuyafanya maeneo hayo kuwa ni yake , litakua ni suala la kieneo na itakua ni rahisi kwa Israeli kujenga huko.
Nje ya maeneo yanayotaka kuchukuliwa na Israeli, jeshi la Israeli litaendelea kuyadhibiti - jambo ambalo baadhi ya Wapalestina wanasema limenyima kizazi chao haki zao za kimsingi za kiraia
Je dunia inasema nini kuhusu mpango wa Israeli?
Kwa kiasi kikubwa, Israeli imekua ikionywa na rafiki sawa na mahasimu wake kwamba isiendelee na mpango wake wa kuyaweka maeneo yanayokaliwa na Wapalestina chini ya mamlaka. Kuna hofu kwamba hatua ya aina hiyo itaufanhya mpango wa amani baina ya Israeli na Wapalenstina kuwa mbali sana kufikiwa.
Wapalestina wanatoa wito wa kuwepo kwa shinikizo la ndani ya nchi ili kuivunja mipango ya Netanyahu, na Waziri wao mkuu amesema wanaweza kujitangazia uhuru wao kwa eneo lote la West Bankiwapo Israel itachukua ardhi pale.

Ni nini kitakachobadilika iwapo maeneo ya West Bank yatakua chini ya mamlaka ya Israel?
Kwa mfano ikitokea( Israeli na Marekani bado wanajadili ni linin a ni vipi ), makazi na maeneo yanayoyazingira yatakua sehemu ya kudumu ya Israeli( walau kutokana na msimamo wa Israeli), .
Kubadilisha uamuzi huu kutahitaji uungaji mkono mkubwa wa walio wengi miongoni mwa Wabunge wa Israeli, jambo ambalo huenda lisiwezekane.
Kwa kawaida, sheria za Israeli tayari zinashughulikia suala la walowezi, ingawa si kwa Wapalestina, ambao wanafuata sheria za jeshi la Israeli tu na sheria ya Wapalestina, kwahiyo kutakua nkutakua na mabadiliko madogo yatakayoshuhudiwa kutokana na hilo .
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema kuwa anapanga kuchukua kwa ufanisi baadhi ya maeneo ya Ukingo wa magharibi- (West Bank) hatua itakayokua ni kitendo cha utata wa hali ya juu.
Ukingo wa Magharibi ni nini?
Ni sehemu ya ardhi inayopatikana - kama jina linavyoeleza katika ukanda wa magharibi wa mto Jordan na inapakana na Israel upande wa magharibi, magharibi na kusini. Mashariki kuna Jordan.
Ukingo wa Magharibi umekuwa chini ya uvamizi wa Israel tangu mwaka 1967 katika vita vya Mashariki ya Kati, lakini miongo ya mazungumzo magumu baina ya Israeli na Wapalestina -ambao wote wana haki ya eneo hilo- yamesababisha suala la hadhi yake kuhusu umiliki kutotatuliwa.












