Virusi vya corona: Madagascar yaomba msaada wa dharura kukabiliana na corona

Rajoelina pia alisema kwamba yeye na familia yake wamekuwa wakinywa dawa ya mitishamba ya Covid Organics inayodaiwa kutibu virusi hivyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rajoelina pia alisema kwamba yeye na familia yake wamekuwa wakinywa dawa ya mitishamba ya Covid Organics inayodaiwa kutibu virusi hivyo

Wizara ya afya nchini Madagascar imetuma ombi la msaada wa dharura kwa mashirika na taaisi za Afya huku wagonjwa wa corona wakiongezeka.

Wizara ya Afya imesema kwamba ugonjwa huo katika wiki za hivi karibuni umesambaa kwa kiwango cha juu nchini Madagascar huku maeneo kadhaa yakirekodi milipuko hususan mji mkuu wa Antananrivo, kulingana na mtandao wa Actu Orange.

Kumekuwa na ripoti kwamba hospitali za umma nchini Madagascar zimejaa na zimekuwa zikiwalaza wagonjwa walio katika hali mbaya zaidi.

Katika hospitali moja mjini Antananarivo, mkurugenzi anasema kwamba tayari wanatibu wagonjwa 46 na kwamba wana nafasi ya wagonja wanne zaidi.

Maafisa katika baadhi ya hospitali katika mji mkuu wa Antananarivo, wanadai kwamba hospitali zimejaa kutokana na kuongezeka maradufu kwa wagonjwa wa corona.

Mwakilishi wa WHO nchini Madagascar ameonya kwamba hospitali zimejaa hata kabla ya mlipuko huo kufikia kilele chake nchini humo.

Taifa hilo kwa sasa lina takriban wagonjwa 7000 wa Covid-19.

Rais Andry Rajaolina mapema mwezi huu aliweka masharti ya kutotoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo kufuatia kuongezeka kwa maradhi hayo.

Mnamo mwezi Aprili, alizindua dawa ya mitishamba ya maradhi ya Covid-19 ambayo ilisambazwa nchini humo.

Mizigo kadhaa ya dawa hiyo ya Covid Organic pia ilitumwa kwa makumi ya mataifa barani Afrika.

Hatahivyo uwezo wa kinywaji hicho umepuuziliwa mbali na wataalam wa Afya nchin NIgeria na DR Congo mataifa ambayo yalifanyia majaribio dawa hiyo.

Rais aliwatajka watafiti kuja na tiba ambayo 'waliipata kwamuda muafaka'

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais aliwatajka watafiti kuja na tiba ambayo 'waliipata kwamuda muafaka'

Katikati ya mwezi Julai rais wa taifa hilo alitangaza kwamba wabunge wawili wamefariki kutokana na virusi vya corona huku wabunge wengine 25 wakiambukizwa virusi hivyo tangu kisa cha kwanza kilipothibitishwa katika kisiwa hicho mnamo mwezi Machi.

Rajoleina pia alisema kwamba yeye na familia yake wamekuwa wakinywa dawa ya mitishamba ya Covid Organics inayodaiwa kutibu virusi hivyo ambayo ilizinduliwa mwezi Aprili, licha ya onyo kutoka kwa shirika la Afya duniani kwamba haijaidhinishwa kutumika.

Ni kweli kwamba nimewasiliana na walioambukizwa . Nimeingia katika mahospitali yanayowatibu wagonjwa wa corona. Niko salama'', alisema.

Taifa hilo lina takriban wagonjwa 7000 wa corona

Chanzo cha picha, AFP

Sina virusi vya corona hata kidogo. Sina dalili. Namshukuru Mungu. Nafuata maagizo niliojiwekea, lakini zaidi ya yote mimi na wapenzi wangu mke wangu na watoto wangu, tunakunywa na kufuata maagizo ya dawa yetu ya mitishamba''