Virusi vya corona: Je, dawa za mitishamba zina nafasi katika mapambano dhidi ya corona?

tiba asilia

Chanzo cha picha, Getty Images

Dawa ya asili ya Covid-19 ambayo imetengenezwa nchini Madagascar na kutangazwa na rais Andry Rajoelina imezua mijadala kuhusu matumizi ya dawa za mitishamba barani Afrika.

Dawa hiyo ya asili ya kutibu corona imetengenezwa na mmea ambao umedhibitishwa kutengeneza dawa za malaria.

"Hali ya wagonjwa ambao wanatibiwa corona kwa kutumia dawa hiyo ya mitishamba wanaonekana kuwa na nafuu baada ya siku saba na kupona kabisa baada ya siku kumi," Rais Rajoelina alisema, kwa mujibu wa ripoti ya Mei Mosi.

Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwa hakuna tiba ya virusi vipya vya corona . Hata hivyo inaziunga mkono dawa za asili ambazo zimethibitishwa kisayansi.

Licha ya dawa hiyo kutokuwa na udhibitisho, Mamlaka ya kisiwa cha bahari ya hindi imejichukulia maamuzi ya kuhalalisha dawa hiyo ya mitishamba na kutangaza kuanza kujaribu kuwatibu watu wenye maambukizi ya corona tangu Mei Mosi.

Jeshi limesambaza dawa hiyo ya mitishamba ya Covid-19 na wanafunzi wamesisitizwa kutumia kabla hawajaanza masomo.

Ukosoaji mkubwa umejitokeza kuhusu ubora wa dawa hiyo na hakuna udhibitisho unaodhibitisha kuwa kinywaji hicho ni kinga.

Mkubaliano ya kimataifa kuhusu afya

dawa

Chanzo cha picha, Getty Images

Dawa hiyo ya mitishamba imesambazwa katika mataifa kadhaa barani Afrika, ikiwemo Equatorial Guinea, Niger, Gabon, visiwa vya Comoro, Guinea-Bissau ,Ghana na Tanzania.

Sudan Kusini na Afrika Kusini ambayo ina wagonjwa wengi wa corona barani Afrika wameonyesha nia ya kupata bidhaa hiyo.

"Imeonekana wazi kuwa rais Andry Rajoelina, amekuwa akishawishi mataifa ya Afrika," tovuti moja ya Madagascar ilisema.

Maendeleo ya dawa hiyo yalipelekea umoja wa Afrika kuwa na mkutano wa simu, kuzungumzia suala hilo mwezi Aprili.

Kituo cha kukabiliana na magonjwa cha Umoja wa Afrika kimeanza mazungumzo na Madagascar ili waweze kutoa takwimu za ubora wa dawa hiyo na usalama wake.

Madagascar imekataa madai ya Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS ambayo ilidai kutakakibali cha kuuza dawa na kusema kuwa taifa hilo limetuma bidhaa hizo kama dawa.

Umaarufu wa matumizi ya dawa za mitishamba

Maelezo ya video, Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona?

Taarifa kuhusu ugonjwa wa Covid-19 katika mataifa kadhaa barani Afrika zimerudiha watu katika bara hilo kuona umuhimu wa kutumia tiba za kienyeji .

Nchini Cameroon, Askofu mkuu wa kanisa katoliki la Douala, Samuel Kleda, alitangaza dawa ya mitishamba ambayo inayoweza kuwaweka huru watu wagonjwa wa corona.

"Nilifahamu kwanza mmea uliotumika na kutokana na dalili za virusi vya corona.Nilichanganya dawa hiyo ambayo anapewa mtu ana maambukizi ya virusi vya corona na walipata nafuu", alisema hayo kwenye kipindi cha Televisheni.

Mwenyekiti wa jumuiya ya dawa za mitishamba, Sao Tome alitangaza hivi karibuni dawa hiyo ya kunywa kuwa inatibu virusi vya corona.

Nchini Nigeria, kiongozi wa dawa asili wa Yoruba bwana Ooni of Ife, alisema kuwa jitihada za kupata tiba ya corona ziko ukingoni.

Coronavirus

Usimamizi wa dawa za jadi

Barani Afrika, waatalamu wa tiba asilia na wataalamu wa afya wanashirikiana. Ingawa katika kipindi hiki cha mlipuko kumekuwa na uangalizi mkubwa zaidi wa dawa zinazotengenezwa na hata taasisi inayotengeneza dawa.

Hatahivyo hali ya mlipuko wa ugonjwa wa corona inaongeza uhitaji wa usimamizi wa tiba za jadi.

Afrika Kati , Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na wanafanya utafiti wa tiba ya mitishamba inayotibu ugonjwa wa corona.

Utafiti uliofanyika nchini China umebainisha kuwa mmea huo wa Pakanga unaweza kutibu hata virusi vya Sars vilivyotokea 2005.

Ghana, Nigeria na Kenya pia wanaangalia kwa kina tiba hizi za mitishamba kutona kama zinaweza kutibu virusi.

Guinea imewahamasisha waganga wa dawa za asilia kushirikiana na serikali katika kutengeneza tiba ya ugonjwa huo.

Msukumo wa kupata suluhisho la mlipuko uliopo

corona

Chanzo cha picha, Getty Images

Mataifa ya Afrika yanakabiliana na msukumo mkubwa wa kupambana na ugonjwa wa corona, huku hatua zilizochukuliwa mpaka sasa ni kuepo kwa amri za kutotoka nje jambo ambalo limeathiri uchumi kwa kiwango kikubwa.

Ingawa haijawa wazi kuwa dawa hizi za asili zinasaidia kwa namna yeyote, kama ni tiba zinazoweza kufanya kazi sahihi au haziaminiki tu.

Dawa iliyotangazwa Madagascar kuwa inatibu ugonjwa wa Covid 19 imeonekana kupingwa vikali na kunaidwa kuwa hiyo ni njia potofu ambayo inaweza kusababisha maambukizi kuleta athari zaidi.

Katika hali hiyo , tiba asilia au za mitishamba zinaonekana kuvutia sera za watunga sheria wa barani Afrika.