Wananchi waombwa utulivu kukabiliana na majanga mawili ya mlipuko DRC

Chanzo cha picha, EPA
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo imethibitisha uwepo wa visa vipya vya ugonjwa wa Ebola.
Waziri wa afya nchini humo Dkt. Eteni Longondo amethibitisha kuwa chanzo cha vifo vya watu wanne waliofariki Mei 18, huko magharibi mwa mji wa Mbandaka, ambao una idadi ya watu wapatao milioni moja.
Utafiti wa maabara kuu umethibitisha kuwa watu hao walifariki kutokana na Ebola.
Na sasa Kongo imeripoti kuwa na kesi 11 za Ebola.
Gavana wa jimbo hilo alianza kuonya serikali ya Kongo tangu katikati ya mwezi Mei juu ya mlipuko wa Ebola. Na ameomba sasa baada ya kuthibitishwa kwa kesi hizo , anawaomba raia kutulia na kuendelea kufuata hatua za usafi haswa kunawa mikono, kutoshikana nmikono, wasishikane mikono au kugusa wagonjwa wanaotoka damu.
Ni zaidi ya kilomota 1,000(karibu maili 600 ) kutoka kituo ambacho kina mlipuko wa corona kwa sasa huko mashariki mwa taifa hilo.
Vilevile wahudumu wa usalama na afya wataenda katika jamii waliopoteza ndugu zao kwa ajili ya kupuliza dawa eneo hilo ambalo wagonjwa walipatikana.

Chanzo cha picha, EPA
Mwishoni mwa mwezi April, DRC ilikuwa inalenga kutangaza kuisha kwa mlipuko mkubwa wa pili , lakini maambukizi mapya yakajitokeza.
Watu zaidi ya 2,000 walifariki kutokana na ugonjwa huo tangu mwaka Agosti 2018.
Taifa hilo sasa linakabiliana na milipuko miwili ya virusi, DRC imethibitisha kuwepo kwa zaidi ya maambukizi 3,000 ya corona.
Rekodi ya mwisho ya mlipuko wa Ebola mjini Mbandaka,ilikuwa mwaka 2018, wakati watu 33 walifariki katika mji huo.












