Coronavirus: Watanzania na Wakenya washinikiza serikali zao kutangaza 'lockdown'?

Mhudumu wa afya

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mataifa ya Afrika Mashariki bado hayajatangaza amri ya kukaa ndani''lockdown'' katika mataifa yao
    • Author, Na Dinah Gahamanyi
    • Nafasi, BBC News Swahili

Baadhi ya raia wa Tanzania na Kenya wamekua wakizitaka serikali zao zitangaze amri ya watu kukaa nyumbani ili kudhibiti maambukizi ya coronavirus. Lakini je marufuku hii ya ''lockown'' ina maana gani?

Nchini nyingi duniani zimelazimika kuweka amri ya kutokuwepo na mikusanyiko baina ya watu ''lockdown'', ili kudhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya corona yaliyowapata karibu watu 250,000 kote duniani na kusababisha vifo 9,900.

Amri ya kukaa nyumbani ''lockdown'' imekua ikiwekwa na nchi mbali mbali zilizokumbwa na mlipuko wa coronavirus duniani kwa kiwango tofauti kulingana na kiwango na mlipuko na kasi ya kusambaa kwa virus katika nchi husika.

''Lockdown'' imewafanya watu kubadili mtindo wao mzima wa maisha ili kuzingatia sheria.

Swali ni je Watanzania na Wakenya watarajie nini iwapo serikali zao zitatangaza ''lockdown?

Kuna aina mbili za ''lockdown'

Moja ikiwa ni amri kamili ya kukaa nyumbani ikimaanisha kuwa watu hawaruhusiwi kabisa kutoka majumbani mwao na nyingine ikiwa ni ile ambayo sio kamili ambapo baadhi ya shughuli za umma na matembezi ya watu hudhibitiwa kwa kiwango fulani.

Kwa mfano tarehe 23 Januari wakati Uchina ilipoweka amri kamili ya kukaa nyumbani dhidi ya wakazi wa jiji la Wuhan, lenye watu milioni 11, ambako virusi vya Covid-19 inadhaniwa kuanzia ilikua ni amri yamili ya kukaa nyumbani.

Amri hiyo iliwataka wakazi wa jiji hilo kutosafiri kuingia ama kutoka nje ya jiji hilo, hata wale waliokua na sababu za kimatibabu au kwa sababu za kibinadamu.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Raia wa Italia watiana moyo kwa nyimbo za kizalendo

Ndani ya jiji, usafiri wa umma ulizuiwa magari ya kibinafsi yalizuiwa kuendeshwa barabarani mara nyingi, isipokua pale yanapokua sehemu ya kampeni ya vita dhidi ya virusi vya corona.

Italia pia ilitangaza Amri kamili ya watu kukaa nyumbani baada ya kuwa na kasi ya maambukizi ya coronavoirus nyuma ya imekuwa ikifuata nyuma ya Uchina kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya coronavirus ikiwa na vifo 1,284 huku 4,440 wakiambukia virusi hiy, kulingana na data za Chuo Kikuu cha Hopkins.

''Lockdown'' ilianza kutekelezwa kwa mara ya kwanza kaskazini mwa nchi, kabla kutekelezwa kitaifa, na serikali imewataka watu milioni 60 wa Italia kubakia majumbani mwao pale inapowezekana.

Ufaransa, Pia imetangaza amri kamili ya kukaa nyumbanina. Kulingana na amri hiyo raia wanaotoka majumbani mwao lazima wabebe waraka unaoelezea ni kwa nini, huku nchi hiyo ikiwa imeweka faini ya €135 ($150; £123) kwa yeyote atakayekiuka amri ya kutoka bila sababu.

Rais Emmanuel Macron awali aliwaamuru watu kubaki majumbani mwao na waende nje tu pale wanapoenda kufanya majukumu muhimu

Chanzo cha picha, BBC

Maelezo ya picha, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron awali aliwaamuru watu kubaki majumbani mwao na waende nje tu pale wanapoenda kufanya majukumu muhimu

Rais Emmanuel Macron awali aliwaamuru watu kubaki majumbani mwao na waende nje tu pale wanapoenda kufanya majukumu muhimu. Bwana Macron alisema: "Tuko vitani... hatupambani na jingine lolote lile wala nchi yetu wenyewe. Lakini adui yuko hapa, haonekani, hawezi kuguswa ... na anasonga mbele."

Uingereza imetangaza haijatangaza ''Lockdown'' kamili licha ya kwamba imerekodi , vifo vya watu 71, lakini watu wamekua wakiambiwa waepuke matangamano ya kijamii, watu kufanyakazi nyumbani ikiwa wanaweza na kuepuka safari za kigeni zisizo muhimu.

Waziri Mkuu Boris Johnson Jumatatu aliwataka watu waepuke kwenda kwenye maeneo kama vile baa, vilabu vya pombe na migahawa.

Amri kamili ya hivi karibuni ya kukaa nyumbani imetolewa Alhamisi katika Jimbo la Californianchini Marekani, wakazi wake wakiagizwa "kukaa nyumbani" au ''lockdown'' huku likijaribu kudhibiti maambukizi ya coronavirus, yanayoongezeka mara dufu kila baada ya siku nne.

Amri itawaruhusu wakazi kuondoka majumbani mwao kununua mahitaji ya nyumbani au dawa, au pale wanapotembeza na mbwa au wanapofanya mazoezi ya mwili, lakini itawataka kuacha mikusanyika ya watu.

California Street, usually filled with cable cars, is seen empty in San Francisco, California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mitaa ya jiji la San Francisco jimboni California ambayo kwa kawaida hufurika magari kwa sasa ni mitupu

Pia italazimisha biashara ambazo sio za lazima kufungwa, huku ikiwaruusu wengine wanaofanya biashara za vyakula na mahitaji na bidhaa nyingine muhimu za nyumbani, maduka ya dawa, benki na vituo vya mafuta ya petroli kuendelea kufunguliwa.

Amri yake itawaruhusu wakazi kuondoka majumbani mwao kununua mahitaji ya nyumbani au dawa, au pale wanapotembeza mbwa au wanapofanya mazoezi ya mwili, lakini itawataka kuacha mikusanyika ya watu.

Itawalazimisha biashara ambazo zinaonekana si za lazima kufungwa, huku ikiwaruhusu wengine wanaofanya biashara za vyakula na mahitaji na bidhaa nyingine muhimu za nyumbani, maduka ya dawa, benki na vituo vya mafuta ya petroli kuendelea kufunguliwa.

Awali alikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 40 katika jimbo lake wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya Covid-19 katika miezi miwili ijayo.

Habari zaidi kuhusu coronavirus

Virusi vya corona tayari vimewaua watu 205 nchini Marekani huku watu 14,000 wakipata maambukizi, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Hopkins.

Ujerumani haijatangaza '' Lockdown''ambayo ina zaidi ya visa zaidi ya 6,000 na vifo 13, imezuia ibada za kidini na ikawambia watu wafute safari zao za ndani na nje ya nchi yao au safari za mapumziko y za kitalii.

Hata hivyo serikali imeweka masharti yanayowazuwia raia kukusanyika katika maeneo kama baa, burudani, hifadhi za wanyama na pia viwanja vya michezo vimefungwa. Shule pia zimefungwa na inatafakari uwezekano wa kuweka ''lockdown''.

Je nchi za Afrika Mashariki zinaweza kuwa chini ya ''lockdown''?

Ukweli ni kwamba nchi za Afrika Mashariki zimepata hivi karibuni visa vya maambukizi ya virusi vya corona ikilinganishwa na maeneo mengine ya dunia na idadi ya maambukizi bado ni ya kiwango cha chini, hali inayoyazuwia mataifa hayo kuchukua hatia ya kutoa amri ya kukaa nyumbani ''lockdown''

Hata hivyo kasi ya kuenea kwa maambukizi ya coronavirus imewatia hofu baadhi ya raia wa Tanzania na Kenya na kupitia mitandao ya kijamii wamezitaka serikali zao kuchukua hatua itakayowaamuru watu ''kukaa ndani'' kama njia wanayoiona kuwa ndiyo inayofaa ya kudhibiti maambukizi ya virus.

Mstari

Nchi za Afrika mashariki hazijatangaza ''lockdown'' kukabiliana na janga la coronavirus:

Kile kilichofanywa na mataifa kama Tanzania, Kenya, Uganda, na Rwanda katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona ni kutolewa kwa maagizo au melekezo kwa raia.

Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu amekuwa akitoa maelekezo juu ya coronavirus kwa Watanzania
Maelezo ya picha, Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu amekuwa akitoa maelekezo juu ya coronavirus kwa Watanzania

Tanzania yenye visa vitano kwa sasa, baada ya kutangaza kisa chake cha kwanza cha maambukizi ya coronavirus kwa mfano mfano iliwaagiza Watanzania kuzingatia kanuni ya 46 ya sheria ya afya ya jami na Waziri wa Afya ummy Mwalimu akatoa maelekezo yafuatayo:

  • Kwanza Watanzania wasiokuwa na safari za lazima wanashauriwa kwa sasa kusitisha safari zao kwenye nchi zenye maambukizi
  • Taasisi zote zikiwemo shule, hoteli, maduka ya biashara, nyumba za kulala wageni, makanisa, misikiti, ofisi za umma na binafsi, vituo vya kutolea huduma za afya, taasisi za fedha, vyombo vya usafiri pamoja na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile masoko, viwanja vya michezo na vituo vya abiria kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni au maji yenye dawa kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa mikono.
  • Kuweka maji yenye dawa ya chroline katika mageti ya kuingia katika hifadhi zote kwa ajili ya kusafisha mikono ya watalii na waongoza wageni.
  • Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono
  • Kukumbatiana, kubusu, kuepuka kushika pua, mdomo na macho.
  • Hospitali zote nchini za serikali na zisizo za serikali kuweka zuio la idadi ya watu ambao wanakwenda kuwaona ndugu zao. Kwa maelekezo ya waziri ni kwamba wageni wa kumuona mgonjwa wasizidi wawili kwa siku kwa kila mgonjwa mmoja.
  • Wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa vituo vya afya iwapo watamuona na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Covid- 19.

Katika hatua ya hivi punde ya kukabiliana na mlipuko wa coronavirus Serikali imetangaza kupiga marufuku kuwatembelea wafungwa...Tanzania yathibitisha kuwa na kisa cha kwanza cha corona

Hospitali na maduka ya jumla wametakiwa kuwa na kemikali za kuua vimelea, maji ya kunawa na kuhakikisha wanasafisha maeneo hayo ili kuepuka maambukizi ya coronavirus
Maelezo ya picha, Matumizi ya kemikali ya kusakasa mikono ni moja ya mambo yanayohamasishwa na serikali za Afrika mashariki tangu mlipuko wa coronavirus ulipoingia eneo hilo

Kwa upande wa Kenya ambayo sasa ina visa saba vya coronavirus hali si tofauti na Tanzania kwani baada ya ilipopata kisa coronavirus Wakenya walipewa maagizo, na katika jitihada za kudhibiti rais Uhuru Kenyatta akatoa maagizo mkiwemo akawaambia:

  • Waepuke mikusanyiko ikiwemo maeneo ya kuabudu
  • Wapunguze mikusanyiko ya kijamii mkiwemo harusi na mazishi, na masharti hayo yazingatiwe mara moja na wanafamilia
  • Waepuke maeneo yenye msongamano wa watu mkiwemo maduka ya jumla na maeneo ya burudani
  • Wapunguze mikusanyiko katika maeneo ya usafiri wa umma na kwingineko iwezekanavyo.
  • Kuwepo ukomo wa wageni wanaotembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali za umma na za kibinafsi... Visa viwili zaidi vya coronavirus vyatangazwa Kenya

Hatua zilizochukuliwa na Rwanda ni pamoja na kuzuwia mikusanyiko ya watu na kuhimiza usafi.

Waziri wa Afya rikali ya Rwanda imetangaza kuchukua hatua kadhaa za dharura kukabiliana na janga la coronavirus, saa kadhaa baada ya kutangaza kwamba raia mmoja wa India aliyewasili nchini humo Machi 8, kuwa na virusi vya corona.

Visa vya hivi karibuni vinaifanya Rwanda kuwa na jumla ya visa kumi na moja vya coronavirus

Chanzo cha picha, MINISTRY OF LOCAL GOVERNMENT, RWANDA/FACEBOOK

Maelezo ya picha, Visa vya hivi karibuni vinaifanya Rwanda kuwa na jumla ya visa kumi na moja vya coronavirus

Nchi hiyo ambayo imekua na idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya coronavirus katika Afrika mashariki kwa kiwango cha watu 11 imetoa maagizo kwa umma wa wanyarwanda mkiwemo:

  • Kufungwa kwa maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.
  • Hatua hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia hii leo, wamesema.
  • Shirikisho la Sola la Rwanda(FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.
  • Raia wametakiwa kunawa mikono yao mara kwa mara
  • Na katika hatua ya hivi safari za kuingia kuingia na kutoka nchini humo zimezuiwa kwa muda

Uganda haijapata kisa chochote cha virus

Licha ya kwamba bado haijaripoti kisa chochote cha maambukizi ya coronavirus Uganda imechukua hatua za kudhibiti maambukizi ya corona huku serikali ikitoa maagizo kwa raia inayoamini yatasaidia kudhibiti maambukizi ya virusi.

Serikali ya Uganda iliweka sera ya karantini ya lazima kwa wasafiri wanaowasili nchini humo kutoka mataifa 16 yaliyo katika 'hatari zaidi' ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Uingereza, Marekani na nchi kadhaa za Ulaya ni miongoni mwa mataifa yatakayoathiriwa na sera hiyo mpya ya usafiri nchini Uganda.

Awali serikali pia ilisema wasafiri wanaowasili katika uwanja wa kimataifa wa Entebbe watakuwa wakipuliziwa dawa.

Ni dhahiri kwamba visa vya coronavirus katika mataifa ya Afrika mashariki ni ndogo, ikilinganishwa na maeneo mengine ya dunia.

Licha ya kasi ya maambukizi kuangaliwa na baadhi ya wana Afrika Mshariki kuwa ni ya kutisha, huenda wakasubiri kwa muda kwa mataifa yao kutangaza amri ya kukaa nyumbani au''lockdown''

Nchi zilizozuwia safari