Rais wa Urusi ameonya kuhusu mipango ya upanuzi wa jeshi la wanahewa wa Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais Putin amesema kwamba Marekani inaimarisha jeshi lake la wanahewa kwa kasi tayari kwa operesheni ya angani akiongezea kwamba Urusi inahitaji kuimarisha jeshi lake la wanahewa zaidi.
Katika mkutano na maafisa wa ulinzi, Bwana Putin aliweka wazi kwamba upanuzi wa jeshi la wanahewa la Marekani ni tishio kwa maslahi ya Urusi.
Mnamo mwezi Agosti rais Trump alizindua kitengo kipya cha ulinzi kitakachoangaizia vita angani. Marekani, Urusi, na China zote zinaaminika kujaribu silaha zake zinazoweza kuharibu setlaiti iliopo angani.
Uhasama wa kiubabe wa kivita
Mwaka uliopita, viongozi wa Marekani walionyesha hamu yao ya kuwa na jeshi la angani , wakitangaza tawi la sita la wanahewa wake ambao watakuwa wakiangazia vita vya angani.
Rais Trump alionya kuhusu hatua za kijeshi zilizopigwa na maadui zake. Nimeona vitu ambavyo hungetaka hata kuviona, alisema.
Makamu wa rais Mike Pence alisema kwamba China na Urusi zimekuwa zikitengeza leza za angani pamoja na makombora yanayoweza kuharibu Setlaiti zilizopo angani ambayo yanahitaji kukabiliwa.
'Mazingra ya angani yamebadilika katika kizazi kilichopita' , alisema bwana Pence.
Kile ambacho kilikuwa na amani na kisichodhibitiwa sasa kimejaa upinzani. Kwa mfano mataifa yenye uwezo mkubwa duniani yametumia anga kijeshi kwa mawasiliano ama hata upelelezi kwa miaka mingi.

Chanzo cha picha, AFP
Ushindani miongoni mwa mataifa yenye uwezo mkubwa duniani
Kuna operesheni za kijeshi na zile za kiraia angani, lakini zinaweza kupishana. Teknolojia ya kutumia setlaiti katika GPS ilianzishwa na jeshi la Marekani kabla ya raia kuruhusiwa kuitumia.
Watu hawajui kwamba anga tayari ni mazingira ya kijeshi, alisema Alexandria Stickings, mtaalamu wa usalama wa angani katika taasisi ya Royal United Rusi.
Anga imetumika kijeshi tangu miaka ya 60. Wakati wa vita baridi, Marekani na Usovieti hawakuwa wakipigana angani, lakini zilitumia Setlaiti ili kupelelezana.
China, Urusi na Marekani zote zimejaribu silaha ambazo zina uwezo kuharibu Setlaiti, kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la Secure World Foundation ambalo hurekodi uwezo wa kijeshi angani.
Haya ni makombora ambayo hurushwa kutoka ardhini moja kwa moja yakilenga setlaiti ilio angani.
Kuna silaha ambazo hujulikana kama co-orbitals ambazo ni setlait zilizoshikana na makombora ama roketi inayorushwa kutoka angani.
Setlait hiyo hujiondoa kutoka kwa kombora lililorushwa na kwenda katika mduara wa setlait inayolengwa kwa kuikamata ama kugongana nayo.
"Katika kipindi cha kati ya miaka 10 na 15 iliopita, kumekuwa na ongezeko la maslahi katika utengenezaji wa silaha za angani ambazo zinaweza kutumika kukabiliana angani, anasema Brian Weeden mkurugenzi wa Wakfu wa Secure World Foundation.
Mengi yanafanywa na Urusi pamoja na China lakini Marekani pia inatengeza makombora kadhaa.

Sababu moja kuu ya jeshi kutaka kutetea kile kilichopo angani ni kwasababu Setlaiti zinategemewa sana duniani.
Marekani pamoja na makampuni yake ama serikali inamiliki setlaiti nyingi zaidi ya taifa jengine lolote duniani kulingana na Muungano wa Wanasayansi walio na hofu, shirika linapopigania maswala ya wanayansi .
China kwa sasa ina setlaiti zaidi ya Urusi na zilizosalia zinatoka kutoka kwa mataifa tofauti.
Idadi ya setlaiti za kijeshi za China angani imekua ikiongezeka huku Urusi pia ikijenga setlait zake ya kijeshi ambazo zilitoweka baada ya kuvunjika wa Muungano wa Sovieti mbali na matatizo ya kifedha.
Malengo mapya ya Marekani
Uzinduzi wa jeshi la Marekani la angani huenda lengo lake kuu ni kuijibu Setlaiti za China na mipango ya uundaji wa silaha ambazo sasa zimeanza kutoa matokeo mazuri, kulingana na Belddyn Bowen , mtaalam wa maswala ya angani kutoka chuo kikuu cha Leicester.
Mwaka 2007 China ilifanyia majaribio kombora lake la kuharibu setlaiti ambalo liliharibu Setlaiti yake ya hali ya hewa ambayo ipo zaidi ya maili 500 angani.
Licha ya ukosefu wa habari madhubuti, Marekani na Urusi zote zinaaminika kutengeneza kombora la kuharibu Setlaiti ambalo linaweza kurushwa kutoka ardhini ama kutoka kwa ndege likiwa na uwezo wa kuharibu sensa ya setlaiti.















