Tupolev -160: Ndege za kuangusha mabomu za Urusi zatua Venezuela na kuighadhabisha Marekani

Tupolev Tu-160 ikiwa uwanja wa ndege wa Maiquetia, Simón Bolívar kaskazini mwa Caracas, Desemba 10, 2018

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ndege aina ya Tupolev Tu-160 iliyotua uwanja wa Simón Bolívar Jumatatu
Muda wa kusoma: Dakika 3

Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini.

Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.

Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumattau katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kitendo hicho ni sawa na "serikali mbili fisadi kufuja mali ya umma."

Serikali ya Urusi imesema maneno yake hayo "hayafai hata kidogo."

Ruka YouTube ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa YouTube ujumbe

Ndege hizo mbili za kivita zenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefu bila kutua zilitua katika uwanja wa ndege wa Simón Bolívar viungani mwa mji mkuu wa Venezuela, Caracas, zikiandamana na ndege nyingine mbili za Urusi.

Venezuela na Urusi zimekuwa marafiki kwa muda mrefu na ndege hizo mbili za kivita ziliwahi kutumwa tena taifa hilo mwaka 2008, zikiwa pamoja na manowari moja yenye uwezo wa kurusha makombora.

Ndege hizo zilifika tena Venezuela mwaka 2013.

The arrival of two Russian Tupolev Tu-160 strategic long-range heavy supersonic bomber aircrafts at Maiquetia International Airport, just north of Caracas, on December 10, 2018.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waziri wa ulinzi wa VenezuelaVladimir Padrino (wa pili kushoto, mstari wa mbele) aliwalaki Warusi hao

Kitendo cha sasa kimetokea siku chache tu baada ya rais Maduro kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow.

Waziri wa Ulinzi wa Venezuela Vladimir Padrino alisema ndege hizo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Venezuela na mshirika wake Urusi.

"Hili tunalifanya kwa pamoja na marafiki zetu, kwa sababu tuna marafiki duniani ambao hutetea na kuheshimu uhusiano wa usawa."

Presentational grey line
Map showing emigration routes
Maelezo ya picha, Njia zinazotumiwa na raia wa Venezuela baada ya kuondoka nchini mwao
Presentational grey line

"Tunajiandaa kuilinda Venezuela hadi hatua ya mwisho ikilazimu," alisema waziri huyo akionekana kurejelea tuhuma za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ya nchi hiyo kwamba yapo mataifa yanayotaka kupindua serikali ya nchi hiyo.

Rais Maduro alisema Jumapili kwamba kuna juhudi zinazoendelea kwa sasa "zikiratibiwa moja kwa moja kutoka White House (Marekani) za kuvuruga maisha ya kidemokrasia Venezuela na kutekeleza mapinduzi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kikatiba, kidemokrasia na iliyo huru ya taifa letu."

Bw Pompeo alishutumu kitendo cha kutumwa kwa ndege hizo za Urusi kwenye Twitter.

Pompeo

Chanzo cha picha, TWITTER

Presentational white space
Presentational white space

Msemaji wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, Dmitry Peskov, amesema tamko la Pompeo si la kidiplomasia hata kidogo.

Bw Pompeo hakuwa afisa pekee wa Marekani aliyeshutumu kitendo hicho cha Urusi.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Kanali Rob Manning alisema hivi majuzi, Marekani ilituma meli ya jeshi la wanamaji inayotumiwa kama hospitali Amerika Kusini kutoa msaada wa kimatibabu kwa mamilioni ya raia wa Venezuela ambao wameikimbia nchi yao kutokana na mfumko mkubwa wa bei ya bidhaa na huduma na uhaba mkubwa wa bidhaa, chakula na dawa nchini mwao tangu mwaka 2014.

A Venezuelan woman who has emigrated carries a bag along the Pan-American highway

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maelfu ya raia wa Venezuela wamekuwa wakiyakimbia maisha magumu nchini mwao

"Hii ni tofauti sana na Urusi, ambao hatua yao kutatua mgogoro huu wa kibinadamu Venezuela ni kutuma ndege za kuangusha mabomu badala ya msaada wa kibinadamu," amesema Kanali Manning kwa mujibu wa kituo cha habari cha NBC.

Lakini Urusi siyo pekee iliyotuma ndege za kivita katika taifa au mataifa mengine.

A Russian Air Force pilot is pictured at Maiquetia International Airport, just north of Caracas, on December 10, 2018.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mmoja wa marubani wa kijeshi waliosafiri na ndege hizo za Urusi

Marekani pia ilituma ndege za kivita nchini Ukraine, moja ya washirika wake, baada ya uhusiano wake na Urusi kudorora hasa baada ya Urusi kumega eneo la Crimea mwaka 2014.

Urusi ilichukulia hatua ya Marekani na mataifa ya Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato) ya kujenga ushirikiano wa karibu na Ukraine kwama tisho kwake.

Presentational white space

Ndege aina ya Tu (Tupolev)-160 ni za aina gani?

A Russian Tu-160 bomber near Caracas, Venezuela. Photo: 10 December 2018

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

  • Hufahamika kama White Swans nchini Urusi (lakini zimepewa jina la utani la Blackjacks na Nato)
  • Ni ndege zenye mabawa yanayoweza kuyumba-yumba na zinaweza kwenda kwa kasi mara mbili zaidi ya kasi ya sauti
  • Ndege za kwanza zilizinduliwa mwaka 1981, lakini zikaboreshwa miaka ya 2000
  • Zinaweza kusafiri umbali wa 12,000km (maili 7,456) bila kutua
  • Zinaweza kubeba makombora na mabomu ya nyuklia
  • Zilitumiwa na Urusi katika vita Syria kuanzia mwaka 2015

Unaweza kusoma pia

Presentational white space