Mambo matano unafaa kuyafahamu kuhusu anga za juu: Kiumbe wa kwanza anga za juu alikuwa nani na jua huwa na nini?

Jua huwa na joto sana, kwa hivyo linafaa kuwa na moto mkali. Wanaosafiri anga za juu huwa wako mbali sana na Dunia, kiasi kwamba huwa hawahisi nguvu mvuto zozote. Ni kweli?

La hasha.

Hapa tunaangazia baadhi ya mambo matano ambayo huenezwa sana na watu lakini si ya kweli.

1. Jua ni bonge la moto

Jua

Chanzo cha picha, NASA

Huwa na joto la kiwango cha juu sana (nyuzi 15 milioni katika kitovu chake), lakini je huwa ni bonge moja kubwa la moto? La hasa. Huwa limeundwa kwa gesi.

Kwa uzani, huwa ni haidrjeni asilimia 75 na asilimia 25 helium. Huwa kuna madini kadha ya chuma lakini huwa ni chini ya asilimia 0.1 ya uzito wake.

Joto lake hutokana na shughuli ya kemikali karibu sawa na inayotumiwa kuzalisha kawi katika baadhi ya vinu vya nyuklia, kwa Kiingereza 'nuclear fusion'. Atomu za haidrojeni hugongana kwa nguvu na kasi sana na kuzalisha atomu za helium.

2. Utalipuka ukisafiri anga za juu bila vazi maalum

Mwanaanga

Chanzo cha picha, NASA

Ni uvumi unaoenezwa, hasa kupitia filamu za kale, Kwamba naitrojeni kwenye mwili wako inaweza kupanuka na ufure kiasi kwamba mwishowe unalipuka na kufariki. Ngozi yako huwa na nguvu sana kiasi kwamba hauwezi kulipuka kutokana na hilo.

Hata hivyo kuna hatari nyingine huko zikiwemo kiwango cha joto na miali nururishi hivyo ni lazima uvalie vazi kama hilo.

3. Kiumbe wa kwanza kuzuru anga za juu alikuwa mbwa

Nzi na mbwa

Chanzo cha picha, HISANI

Laika, mbwa koko aliyepatikana katika barabara za Moscow, alikuwa mbwa aliyependwa sana urusi baada yake kusafiri anga za juu akiwa kwenye chombo cha Sputnik mwaka 1957. Hata hivyo, hakuwa kiumbe wa kwanza kusafiri anga za juu. Mwenye rekodi hiyo ni nzi wa matunda.

Nzi kadha walitumwa anga za juu na wanasayansi kutoka Marekani mwaka 1947 kuwasaidia kufahamu kuhusu athari za miali nurusishi.

4. Wana anga za juu huelewa kutokana na kuwa mbali na Dunia?

Mwananga

Chanzo cha picha, NASA

Huyu ni Mae C. Jemison, aliyepigwa picha mwaka 1992 akiwa kwenye chombo cha anga za juu kwa jina Endeavour.

Pengine umezitazama video za wana anga kama vile Tim Peake wakielewa angani katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS), na huenda ulifikiria kwamba hilo linatokana na hali kwamba wako mbali sana na nguvu mvuto ya Dunia.

Hata hivyo, asilimia 90 ya nguvu hizo za Dunia hufika ISS. Hivyo basi mbona wanaelea? Ni kwa sababu ya jambo linalofahamika kama 'free fall'. Hii huwa na maana kwamba kwenye eneo ombwe au tupu (lisilo na chochote) vitu huanguka kwa kasi sawa, bila kujali uzito wake. Wana anga hao kwa hivyo huwa wanaanguka kuelekea kwenye Dunia kwa kasi sawa na chombo walichomo ndani yake, lakini chombo hicho huwa kinasonga hivyo wanasonga pia. Ndio maana huwa wanaonekana kama wanaelea.

5. Kuna sehemu ya Mwezi yenye giza

Mwezi

Chanzo cha picha, NASA

Ni kweli, kuna sehemu ya Mwezi ambayo huwa ni giza totoro. Hata hivyo, si kweli kwamba sehemu hiyo huwa na giza wakati wote. Mwezi huwa na mchana na usiku sawa na inavyofanyika duniani kwa kila sehemu, ingawa tofauti ni kwamba mchana na usiku kwenye Mwezi huwa ni kipindi cha wiki mbili hivi.

Mwana huu, China ilituma chombo cha kupeleleza yanayotoea sehemu ya mbali zaidi ya Mwezi ambayo huwa na giza. Picha za kwamba zilizoonyesha kwamba kuna sehemu ya mwezi huwa na giza zilipigwa mwaka 1959.