Mkenya Brigid Kosgei avunja rekodi za mbio za wanawake

Brigid Kosgei sets a new world record

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kosgei avunja rekodi katika umri mdogo

Brigid Kosgei ni msichana wa Kenya aliyeshinda mbio za wanawake duniani akiwa na umri mdogo wa miaka 16, na kuvunja rekodi ya muingereza Paula Radcliffe na leo ameweza kubaki katika nafasi yake ya kinara.

Msichana huyo mwenye miaka 25, ameshinda mbio katika saa 2 na dakika 14, ambapo bado anakuwa amevunja rekodi ya Radcliffe ambaye alishinda katika 2:15:25 katika mashindano ya mbio ya mwaka 2003.

Msichana huyo ameshangaza wengi katika ushindi alioupatia nchi yake na kuwa mshindi mdogo zaidi wa mashindano.

Mshindi aliyefuata ametokea Ethiopa's Ababel Yeshaneh, ndio mshindi wa pili wa mashindano ya mbio ya Chicago na alishinda katika dakika ya 6 na sekunde 47.

Presentational grey line

Hapo jana mkenya Eliud Kipchoge ameweka jina lake katika vitabu vya historia , akimaliza kilomita 42 za mbio za marathon kwa saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos nchini Austria Vienna.

Hata hivyo muda huo bora uliowekwa na bingwa huyo hautatambulika kama rekodi ya dunia.

Tofauti kati ya muda mpya wa dunia wa Brigid na Eliud ni kwamba Chicago marathon ni miongoni mwa mashindano ya mbio zinazotambuliwa rasmi na shirikisho la riadha duniani IAAF na huku aliyokimbia Eliud Kipchoge haitambuliwi na shirikisho hilo kwa sababu haikutimiza taratibu zao.