Jacob Zuma: Rais wa zamani wa Afrika Kusini apinga kuwa 'mfalme wa ufisadi'

Maelezo ya video, Jacob Zuma: Nimeonewa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameliambia jopo la mahakama linalochunguza madai ya rushwa dhidi yake kuwa ''kuna njama'' inayolenga kumuangamiza kisiasa.

Alikuwa anafika mbele ya jopo hilo kwa mara ya kwanza huku wafuasi wake wakimshangilia alipoingia katika jengo hilo.

Bw. Zuma, 77, alilazimishwa kujiuzulu wadhifa wa urais wa mwezi Februari mwaka 2018.

Wakati akijitetea, Zuma amesema kuwa madai hayo ya ufisadi ni njama ambayo imekuweko kwa muda mrefu ili kumharibia jina, mpango ambao umetekelezwa na wasimamzi wa chama cha ANC ili kumuondoa kwenye siasa za Afrika Kusini.

Alipoulizwa ni kwa nini anatoa madai hayo, alisema kuwa wanaompiga vita walidhani kuwa huenda ana habari dhidi ya watu fulani, ambazo zikifichuka zitawazuia kupata nafasi za juu katika chama hicho.

Jacob Zuma

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jacob Zuma

Nafasi yake ilichukuliwa na aliyekuwa makamu wake wakati huo Cyril Ramaphosa, ambaye aliahidi kukabiliana vikali na suala la rushwa nchini Afrika Kusini.

Bw. Ramaphosa alielezea utawala wa miaka tisa ya Zuma kama "kupoteza muda".

Mashitaka dhidi ya Zuma yanaangazia uhusiano wake na familia yenye utata ya Gupta, ambayo inatuhumiwa kwa kutumia vibaya uhusiano wao na Zuma kuingilia uteuzi wa mawaziri na kujipatia kandarasi za serikali kwa njia za kifisadi.

Pia anakabiliwa na tuhuma ya kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya Bosasa, ambayo inamilikiwa na familia ya Watson.

Bw. Zuma amekanusha madai hayo yote.

"Nimeonewa na kutuhumiwa kuwa mfalme wa watu wafisadi,"Zuma aliliambia jopo hilo linaloongozwa na jaji Ray Zondo.

"Watu wamenibandika majina ya kila aina na sijawahi kujibizana nao kuhusiana na suala hilo," aliongeza.

Zuma kuhusiana na 'hujuma' dhidi yake

Alielezea kwa kina- na kwa hasira - kile alichotaja kwa miongo kadhaa ya hujuma dhidi yake.

Alidai kuwa mataifa ya Uingereza na Marekani - bado ni washirika wa - sehemu ya mpango wa kumkosoa japo amejaribu kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini Afrika Kusini.

Accreditation badges for supporters of former South African President Jacob Zuma gather outside the Commission of Inquiry into Allegations of State Capture, Johannesburg, South Africa, 15 July 2019.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wafuasi wa Jacob Zuma waliokuwa wamevajia beji zilizokuwa na ujumbe wa kimuunga mkono

Bw. Zuma alidai kuwa waziri wa zamani wa serikali Ngoako Ramatlhodi, aliyetoa ushahidi wa kumdhalilisha ni sehemu ya njama hiyo.

Maajenti wengine wa kigeni walijaribu kumtilia sumu, alisema Zuma, bila kuwataja majina.

Usiku wa kuamkia siku ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake Zuma alikuwa mwenye tabasamu.

Aliweka katika mtandao wa Twitter video inayomuonesha akicheka akiimba "Zuma must fall!"

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Zuma na familia ya Gupta

Alisema aliona familia hiyo ya wazaliwa wa kihindi walikuwa ''marafiki zake''.

"Sikufanya jambo lolote kinyume cha sheria nao. Walikuwa marafiki zangu tu, sawa na jinsi walivyokuwa marafiki wa watu wengine," Bw. Zuma alisema, akiongeza kuwa walikuwa marafiki wa rais wa kwanza wa nchi hiyo Nelson Mandela na Thabo Mbeki.

Alipinga madai kuwa aliruhusu familia hiyo kuingilia kati uongozi kwa "kuteka nyara" na kuipiga mnada nchi hiyo.

"Nilipiga mnada Table Mountain? Je nilipiga mnada jiji la Johannesburg?"alisema.

line

Uchambuzi wa Pumza Fihlani, Mwandishi wa BBC Afrika Kusini.

Kitu kimoja kinachojitokeza katika ushahidi uliyowasilishw ana Bw. Zuma kufikia sasa - ikiwa ataporomoka, basi hatakubali kwenda peke yake.

Ametoa taswira ya picha anayodai kuwa kuna njama ambayo imekuwa ikipangwa dhidi yake kwa zaidi ya miongo miwili.

"Nimechokozwa," alisema, huku akitishia kutaja majina ya wale anadai kuwa majasusi wailohujumu harakati za uhuru wa watu weusi nchini Afrika Kusini na ambao anasema bado wanaendelea kumhujumu.

Wakati mmoja Bw. Zuma alikuwa kiongozi wa upelelezi wa chama chaAfrican National National Congress (ANC), vugu vugu la zamani la kupigania uhuru ambalo limekuwa madarakani tangu uta wala wa weupe ulipoondolewa madarakani mwaka 1994.

Akiamua kufichua siri kama alivyotishia, huenda akatikisa siasa za Afrika Kusini, halia mbayo ukasababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama cha ANC.

Lakini hali itakapotulia, bilashaka watu wa Afrika Kusini wanataka kujua ikiwa alihujumu kiapo cha ofisi yake ilipongia madarakani mwaka 2004 kwa kujihusisha na sula la ulaji rushwa kwa kiwango kikubwa.

Hilo ndilo swali ambalo Tume hiyo inajaribu kuthibitisha - na Bw. Zuma anapigania uhai wake wa kisiasa .

Presentational grey line