Uganda: Mchungaji Joseph Kabuleta akamatwa kwa ‘kumkashifu’ Museveni

Chanzo cha picha, Reuters
- Author, Ambia Hirsi
- Nafasi, BBC Swahili
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Mchungaji Joseph Kabuleta ni raia wa hivi punde wa Uganda kujipata mashakani kwa tuhuma za kumkashifu au kumkasirisha rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.
Bw Kabuleta, alikamatwa na maajenti wa usalama ambao hawakuwa na sare rasmi mwendo wa saa kumi na moja jioni, Ijumaa iliyopita mjini Kampala.
Maafisaa hao aidha hawakuwa na gari rasmi la kazi na wakati wa kumkamata mchungaji huyo hawakuoa sabababu yoyote ya kuchukua hatua hiyo.
Kabla ya kukamatwa kwake Bw. Kabuleta alikua akiendesha kampeini kali katika mitandao ya kijamii ambapo alikua akiikosoa Utawala uliyo madarakani na familia ya Rais.
Katika waraka wa hivi karibuni kwa jina "Mafia Empire and the Transition",ambao ulichapishwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook mnamo Julai 8, Bw. Kabuleta alielekeza lalama zake hususan kwa mwana wa kiume wa Rais Museveni na mshauri wa ngazi ya juu wa oparesheni maalum, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba. Alisema mpango mzuri ni kuhakikisha Jenerali Muhoozi hamrithi baba yake kama rais.

"Tayari Jenerali Muhoozi amekuwa akitumwa kumwakilisha baba yake kwa mikutano ya kimataifa na pia kukutana na mabalozi na viongoziwengine wa ngazi za juu na kuelezea katika mtandao wake wa kuhusu ziara hizo ," ilisema sehemu ya ujumbe wa Bw. Kabuleta.
Aliongeza kuwa: "Huenda Baba yake ana mpango wa kustaafu kimpango baada ya kuchakachua uchaguzi wa mwaka 2021 na kuchukua jukumu la kumshauri mwanawe huku akiendelea kundesha biashara ya kampuni ya familia inayofahamika kama Uganda.
"Au pengine mageuzi yakifanyika ndani ya chama cha NRM na taifa lianze mfumo wa utawala wa kibunge ambapo chama kilicho na wabunge wengi kunachukua uraisi."
N akumaliaza: "Mpango wowote walionayo, Lakini nahisi mambo huenda yakabadilika. Himaya ya Mafia imeanza kuporomoko na Uganda itarejea mikononi mwa Waganda."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Muda mfupi baada ya Kabuleta kukamatwa msemajiowa polisi mjini Kampala Patrick Onyango alinukuliwa na gazeti la New Vision, hana habari kuhusu ''kukamatwa kwake'' na kwamba atazitaarifu vyombo vya habari akipata maelezo kamili.
Baadae msemaji wa Idara ya upelelezi wa jinai Charles Twine,alithibitisha kuwa Bw.Kabuleta amekamatwa na kwamba anazuiliwa na polisi s arrest and detention.
"Amekamatwa na kushitakiwa kwa kiuka sheria ya mawasiliano na kwa sasa anazuiliwa," Bw Twinealiliambia gazeti hilo.
Mjadala mkali waibuka
Hatua ya kumkata Bw. Kabuleta imezua mjadala mkali, huku wengi wakilaani kitendo hicho.
Andrew Mwenda, Mmiliki wa jarida la kibinafsi, aliyepata umaarufu miaka ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa kukosoa utawala wa Rais Museveni kwa kukandamiza vyombo ya habari anasema Waganda wana haki ya kumkosoa rais.
Bw aliandika katika mtandao wake wa Twitter: "Kukamatwa kwa Joseph Kabuleta kwa "kumkasirisha Rais" ni ushamba na hatua iyo haina nafasi katika ulimwengu wa sasa! Waganda wana kila sababu ya kumkosoa Rais. Wamemchagua awahudumie. Wanatakiwa wawe huru kumwelezea kero lao ikiwa hawajaridhishwa na jinsi anavyoongoza nchi!"
Ameongeza kuwa: "Uganda ni nchi na wala sio ufalme, rais anachaguliwa na wananchi hatawazwi kuwa kiongozi wakati wa kuzaliwa; kwa hiyo rais amepewa mamlaka na watu kuongoza kwa niaba. Kwa misingi hiyo raia wana kila sababu ya kuelezea jinsi wanavyohisi kuhusu utawala wa kiongozi wao/Je wanahisi anatekeleza wajibu wake ipasavyo!"
Maoni ya Bw. Mwenda yanaegemea kesi ya kikariba iliyowasilishwa mahakamani mwaka 2005, na hatimae kuamiliwa mwka 2010, ambapo mahakama iliondoa katika Katiba kosa la kuwashawishi watu kupinga serikali.
Wakili James Nangwala, ambaye alimwakilisha Bw. Mwenda katika kesi hiyo wakati huo alihoji kuwa: "Nchini Uganda ambapo Rais anachaguliwa mienendo yake sharti ijadiliwe na wanainchi... Kiongozi hastahili kuwapuuza waliomchagua kwasababu wamempatia madaraka kuwaliko."
Kesi hiyo ilitokana na mashataka yaliyowasilishwa mahakamani dhidi ya Bw. Mwenda kufuatia matamshi aliyotoa katika kipindi cha KFM, kuhusiana na kifo cha aliyekuwa makamu wa rais wa zamani wa Sudan kabla ya taifa hilo kugawannywa mara mbili John Garang.
Katika baadhi ya kauli alizotoa Mwenda alisema: "Unawaona hawa marais wa Afrika. Mtu huyu amesoma hadi chuo kikuu, kwanini mienendo yake sio sawa na mtualiye na elimu? Kwa ninitabia zake ni za kishamba ?'
Sheria ya sasa
Kufikia sasa karibu watu 15 wamekamatwa kwa madai ya kumkasirisharais Museveni tangu mwaka uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Chanzo cha picha, AFP
Kando na kesi inayomkabili Bw. Kabuleta, kesi nyingine ambayo inahusiana na suala la kumkosea Rais heshima inamhusisha Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda Dr Stella Nyanzi, ambaye amekuwa akizuiliwa rumande tangu mwezi Novemba mwaka jana.
Amefikishwa mahakamani klakini amekata kwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana, akihoji kuwa hana haja ya kwenda nyumbani akiwa na hofu ya kuwa atakamatwa tena siku ifuatayo.
Dkt Nyanzi anashtakiwa kwa kutekeleza unyanyasaji wa mtandaoni pamoja na kutoa matamshi machafu swala ambalo linakiuka sheria nchini Uganda.
Hii ni mara ya pili maafisa wa polisi wanamtuhumu Dkt Nyanzi kwa madai ya kumtusi Museveni na familia yake.
Wengine waliokamatwa
Mwaka jana, Mbunge wa Manispaa ya Mukono MP Betty Nambooze alikamatwa na kuzuiliwa kwa kukiuka sheria ya kutumia vibaya mitando ya kijamii. Inadaiwa ujumbe aliyochapisha katika mitandao ya kijamii kabla na baada ya kupigwa risasi na kuuawa kwa mbunge wa Arua Ibrahim Abiriga na ndugu yake Saidi Butele Kongo ulikua wa kichocheza.
Watu wengine waliokamatwa ni pamoja na Raymond Soufa, maarufu Peng Peng, Nasser Mugerwa pamoja na Jane Kuli, ambao walizuiliwa na polisi kwa kukiuka sheria hiyo.
Januari 2019: Polisi katia wilaya ya Gomba walimkamata mtu wa miaka 19 kwa kumtusi Rais Museveni. Mamlaka zilisema,Joseph Kasumba, mkaazi wa Kanoni, alimtukana rais Museveni, majina ya kumdhalilisha.
Juni 18, 2019: Andrew Mukasa, ambaye pia anafahamika kama Bajjo, alishitakiwa kwa kuchochea ghasia thidi ya utawala wa rais Museveni na kuvunja sheria ya mawasiliano.
Novemba 2017: Wakurugezi watano wa na wahariri watatu wa gazeti la Red Pepper washitakiwa kwa makosa saba ikiwa ni pamoja na ukiukaji wa sheria ya utumizi wa kompyuta, kutia dosari sifa ya rais Museveni na kumsumua kiakili ndugu yake mdogo Jenerali Henry Tumukunde.














