Jacob Zuma: akabiliwa na pingamizi kuhusu albamu ya muziki

Wimbo maarufu wa kupigania uhuru ulioimbwa na jacob Zuma ni ile ya Umshini Wami

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wimbo maarufu wa kupigania uhuru ulioimbwa na jacob Zuma ni ile ya Umshini Wami
Muda wa kusoma: Dakika 2

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekumbwa na mzozo mwengijne wa kisiasa - baada ya kusaini mkataba na kampuni ya kurekodi muziki.

Jimbo la Ethekwini lilikubali kufadhili albamu ya nyimbo za kupigania uhuru zilizoimbwa na Zuma, ambazo viongozi walisema zingehifadhi sehemu ya urithi wa kitamaduni.

Lakini chama cha upinzani cha Afrika Kusini, Democratic Alliance (DA), kimetaja hatua hiyo kuwa uharibifu mkubwa wa rasilimali.

Bwana Zuma mara nyingi huimba wimbo wake unaojulikana wa 'Nirudishie bunduki yangu' katika mikutano ya kisiasa.

eThekwini inashirikisha mji wa pwani wa Durban na miji ya jirani ya KwaZulu-Natal, na jimbo la nyumbani kwa Zuma ambako ndiko kuna wafuasi wake wengi.

Kiongozi Zwakele Mncwango wa chama cha DA alisema kuwa rasilimali za serikali za eneo hilo zinatakiwa kutumika kusaidia vijana kujiajiri katika sekta ya muziki.

"Sisi tunataka kukuza utamaduni na urithi. Tatizo letu ni wakati manispaa inapoteza pesa kwa rais wa zamani ambaye anajaribu bahati yake kwenye sekta ya muziki, wakati tuna wasanii chupikizi wanaohitaji msaada," chombo cha habari cha eNCA kimesema.

Mshauri wa DA Nicole Graham alisema chama hicho "kitapigana kwa hali na mali ," akisema: "Haiwezekani kwamba mtu yeyote mwenye busara ataamini kuwa rais wa zamani na mtu aliyekuwa mfisadi na mwenye aibu ataimba nyimbo za kupigania uhuru na kutoa faida yoyote kwa watu wa eneo la Ekwethini

Bwana Zuma, 76, alilazimishwa kwa nguvu kuachia mamlaka mwezi Februari 2018 na chama chake mwenyewe, African National Congress (ANC).

Anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa yanayohusishwa na mpango wa kununua silaha mwaka 1990. Amekan makosa hayo.

'Ana kipaji na anaelewa historia'.

Wakati wa vita dhidi ya uongozi wa wakoloni waliokuwa wachache nchini Afrika Kusini, nyimbo zilitumika sana kuimarisha uungwaji mkono na kuimarisha motisha ya waandamanaji.

Chifu wa bustani ya Thembinkosi Ngcobo alisema kuwa idara hiyo ilipendekeza kutia saini na bwana Zuma baada ya kukosa nyimbo za kupigania uhuru.

Ruka YouTube ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa YouTube ujumbe

Presentational white space

"Tulikuwa tukiwatafuta wasanii na kujaribu kufufua nyimbo kama hizi. Ilikuwa vigumu'' , alisema.

Tulijaribu kutafuta nyimbo zilizohifadhiwa ambazo zilikuwa na video ama hata sauti zozote lakini hatukuweza kupata chochote katika jumba la makumbusho.

Wakati huo waligundua kwamba bwana Zuma alisikika mara kwa mara akiimba nyimbo hizo.

''Ana kipaji na anelewa historia ya muziki'', bwana Ngcobo alisema.

''Alikuwa akiimba nyimbo hizo miaka ya 80 na 90 na hata kabla ya miaka hiyo. Wengi wa vijana katika chama tawala cha ANC hawajui.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Mnamo mwezi Disemba mahakama ya Afrika Kusini iliamuru kwamba bwana Zuma anafaa kulipa fedha alizopewa ili kusimamia kesi yake baada ya kukabiliana na kesi kadhaa za tuhuma za ufisadi.

Inakadiriwa kuwa serikali imelipa kati ya $1m na $2.2m kusimamia kesi yake.

Rais huyo wa zamani pia alijiunga na mtandao wa Twitter mwezi uliopita na kuchapisha ujumbe akisema .

''Nimeamua kuendelea mbele na kujiunga na mazungumzo haya muhimu kwasababu nasikia kwamba watu wengi wanazungumza kuhusu mimi huku wengine wakijiita Zuma. Nimeona ni muhimu kujiunga na kuwa katika mazungumzo haya''.