Dennis Itumbi: Ahojiwa kuhusu barua ya njama ya kumuua naibu rais wa Kenya William Ruto

Chanzo cha picha, AFP Contributor
Aliyekuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya kidijitali katika ikulu nchini Kenya Dennis Itumbi amezuiwa na polisi kuhojiwa kuhusu barua ya njama ya kumuua naibu rais William Ruto.
Itumbi amekamatwa na wapelelezi wanaochunguza tuhuma za njama ya kumuua naibu rais William Ruto.
Anazuiwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi mjini Nairobi, linaripoti gazeti la The Standard.
Anakamatwa siku kadhaa baada ya taarifa kwamba chanzo cha barua hiyo ghushi kimetambulika - barua iliyozusha tuhuma za kutaka kuuawa Ruto.
Wakili wake, Moses Chelanga, anasema bado wanasubiri kuambiwa Itumbi anazuiwa kwa mashtaka gani lakini ameeleza waandishi habari leo kwamba linahusiana na barua hiyo kuhusu njama ya kuuawa kwa naibu rais William Ruto.
Chelanga ameeleza kwamba Itumbi amenyimwa kuachilia kwa dhamana na anazuiwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga mjini Nairobi na anasubiri kufikishwa mahakamani kesho Alhamisi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Wiki iliyopita, mawaziri kadhaa nchini Kenya walikana kupanga njama za kumuua Naibu Rais William Ruto.
Waziri wa biashara wa Kenya Peter Munya amekana shutuma za kupanga mauaji ya Naibu Rais William Ruto, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Waziri Munya alikuwa akizungumza nje ya makao makuu ya ofisi ya Mkurugenzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai (DCI) ambako aliitwa , sambamba na mawaziri wengine, kuhojiwa kuhusu shutuma kuwa walimtishia bwana Ruto, Gazeti la the Standard limeripoti.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Wameshutumiwa kufanya vikao vya siri,the Standard limeongeza, lakini bwana Munya amewaambia waandishi wa habari kuwa hawajapeleka taarifa polisi kwa kuwa bwana Ruto hajapeleka malalamiko rasmi.
Daily Nation la Kenya lilimnukuu waziri akisema kuwa Naibu Rais Ruto alidai kuwa mawaziri hao walikuwa wakifanya vikao vya siri na maafisa wengine.
Naibu Rais Ruto ana mipango ya kuwania urais mwaka 2022.














