Tamasha la Met Gala, tukio lenye faida kwa Taasisi ya mavazi -Costume Institute at the Metropolitan Museum ya Art in New York, hutajwa kama moja ya tukio kubwa kabisha duniani la fasheni.
Linafahamika kwa orodha yake ya majina ya wageni maarufu wanaoalikwa , kushiriki ni gharama kubwa na zaidi ya yote nguo zinazovaliwa ni za ghali mno kulingana na mada ya mwaka.
Mwaka huu, mada hiyo ilikuwa ni Camp: Waraka kuhusu mitindo ya mavazi - inayoendana na onyesho lijalo katika katika Met, picha zilipigwa kwa kuzingatia inshailiyoandikwa na mpigapicha Susan Sontag mwaka 1964 iliyofahamika kama - Notes on Camp.
Hivyo basi Mavazi ya mwaka huu , sawa na onyesho yatazingatia "iujasiri, uchekeshaji , mtindo wa uandishi wenye vichekesh vya vibonzo , sanaa ya mtu mwenye kuigiza utunzi wa mwtu mwingine , kitu ambacho si halisi, maigizo na kuonyesha mambo kwa mtindo wa kupita kiasi ".
Na kumuonyesha kila mshiriki jinsi mambo yanavyopaswa kufanyika mwanzo kabisa alikuwa ni muimbaji Lady Gaga, aliyewasili akiwa ametinga gauni la rangi ya waridi linalopeperuka haikuonekana hivyo alipoingia.
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Lady Gaga, mmoja wa washereheshaji wa tukio ,akiwasili akiwa ametinga gauni lake la rangi ya waridi linalopepea
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Ambalo lilifungua kufichuliwa kwa gauni jeusi, vazi lake la pili ...
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ambalo pia lilifuatiwa na vazi la tatu la waridi iliyokolea lililoubana mwili wake
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, ...Ambayo aliitoa kuonyesha vazi lake la mwisho
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Serena Williams, ambaye alikuwa mshereheshaji mwenza, aliwasili katika vazi hili la rangi ya manjano lenye maua lililoshabihiana na raba zamazowezi za Nike
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ni kwanini uvae kofia moja, unaweza kuvaa nne kama Janelle Monae
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mchezaji Filamu wa Kenya Lupita Nyong'o akitabasamu mbele ya kamera
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mchezaji filamu Michael Urie aliamua kuwa na mionekano miwili kwa wakati mmoja
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wakati huo huo muigizaji filamu Ezra Miller, alionyesha sanaa ya vipodozi ya aina yake iliyowashangaza wengi
Maelezo ya picha, Familia inayoonyesha maisha yake halisi kwenye TV ya Kardashiansiliingia kwa kishindo kwenye tamasha la mwaka huu
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Hawa ni wanandoa wapyaPriyanka Chopra na Nick Jonas, ambao wanasemekana kuwa mara ya kwanza walikutana kwenye tukio kama hili la Met Gala mnamo 2017
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Walifuatiwa kwenye zullia jekundu na kaka mkubwa wa Nick Joe na mkewe mpya, ambaye ni nyota wa filamu ya Game of Thrones Sophie Turner
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mchezji filamu nyota katika Bollywood Deepika Padukone ''alitokelezea'' na gauni hili la mtindo wa Barbie la rangi ya waridi
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Laverne Cox aliingia ukumbini na gauni jeusi la hariri na vipodozi vilivyokolezwa
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mshereheshaji wa tatu ni Harry Styles, ambaye alivalia vazi hili jeusi lenye suruari inayopandishwa juu