Netanyahu ajiandaa kuongoza tena Israel kwa muhula wa tano

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ana matumaini kuiongoza tena Israel
Muda wa kusoma: Dakika 2

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akatetea nafasi yake katika muhula wa tano

Chama chake Likud na washirika wake wa mrengo wa kulia wanatarajiwa kujizolea viti 65 kati ya 120 vya bunge, vyombo vya habari nchini humo vimeeleza.

Waziri Mkuu huyo mwenye miaka 69 anakabiliwa na shutuma za rushwa

Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi yana maana kuwa atakuwa waziri kuu aliyekaa madarakani kwa muda mrefu, akimzidi baba wa taifa hilo David Ben-Gurion.

Netanyahu amesema ''Nimeguswa sana kwa namna watu walivyoniamini kwa mara ya tano, na kuahidi kunipa kura nyingi kuliko kura zilizopita''

''Nina nia ya kuwa waziri mkuu wa wananchi wote wa Israel.Wa mrengo wa kulia, kushoto, wayahudi, wasio wayahudi.Raia wote.''Alisema Netanyahu.

Kampeni zilivyofanyika

Netanyahu ametoa ujumbe mzito kuhusu masuala ya usalama kabla ya kupiga kura, suala lililogeuka kuwa moja kati ya masuala muhimu katika uchaguzi huo.

Alitoa tangazo muhimu katika siku za mwisho za kampeni, akieleza kuwa serikali mpya itaondoa makazi ya wayahudi kwenye ukingo wa magharibi

Makazi hayo yanatajwa kuwepo kinyume cha sheria, chini ya sheria za kimataifa, ingawa Israel imekua ikipinga hilo.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Luteni Jenerali mstaafu Benny Gantz

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Luteni Jenerali mstaafu Benny Gantz

Katika hatua nyingine upinzani umekishutumu chama cha Likud kwa kupeleka waangalizi 1,200 wanaodaiwa kuwa na Kamera za siri ndani ya vituo vya kupigia kura,katika maeneo ya jamii za kiarabu.

Muungano wa jamii ya kiarabu,Hadash-Taal,umesema kuwa kitendo hicho ni kinyume cha ''sheria'' ambacho kina nia ya kuwatisha waarabu, lakini chama cha Likud kimesema kilitaka kuwa na uhakika kuwa ''kura halali'' zinapigwa,

Mpinzani mkuu wa Netanyahu Benny Gantz, ni Luteni Generali mstaafu, aliyeanzisha chama cha bluu na nyeupe mwezi Februari, akiahidi kuiunganisha nchi ambayo anadai ''imepoteza mwelekeo''.

Netanyahu anakabiliwa na mashtaka gani?

Mwishoni mwa mwezi Februari, wakili wa serikali Avichai Mandelblit alimfahamisha Bwana Netanyahu kuwa ana mpango wa kumfungulia mashtaka rasmi kuhusu shutuma za rushwa,udanganyifu na kuvunja uaminifu.

Waziri mkuu anadaiwa kupokea zawadi kutoka kwa wafanyabiashara matajiri na kutoa hongo ili aweze kupata sifa nzuri kwenye vyombo vya habari.Netanyahu amekana kufanya makosa hayo na kusema kuna njama za kisiasa dhidi yake.

Tarehe ya kusikilizwa mara ya mwisho, ambapo waziri mkuu na mawakili wake watapata muda wa kujitetea, bado haijatangazwa.Bwana Mandelblit amesema Mahakama kuu itaamua kama bwana Netanyahu aondoke madarakani au la, kwa vile anashtakiwa.

Kumekuwa na ripoti zinazosema kuwa Netanyahu anajaribu kupenyeza hoja kwa washirika wake wa kisiasa kupitisha sheria ambayo itampa kinga ya kutoshtakiwa akiwa madarakani

Majuma ya hivi karibuni kumekua na msuguano kati ya wanamgambo wa Israel na Palestina katika ukanda wa Gaza, na Rais wa Marekani,Donald Trump anatarajiwa kutangaza mpango wake wa kutatua mzozo wa muda mrefu kati ya Israel na Palestina hivi karibuni.

Hata hivyo ,mchakato wa amani haukua jambo la kipaumbele katika mjadala wa kuelekea uchaguzi.Raia wengi wa Israeli hawana matumaini makubwa kufikia suluhu ya mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe