Rais wa Tanzania Dokta John Magufuli aongoza maelfu kumuaga Ruge

Rais wa Tanzania John Magufuli
Maelezo ya picha, Rais Dokta Magufuli akiigia ndani ya ukumbi wa Karimjee kutoa heshima za mwisho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza maelfu ya watanzania kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Mwili wa Ruge umeagwa leo katika uwanja wa Karimjee halfla iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali wakiwemo pia mawaziri,wabunge, wakuu wa wilaya halikadhalika viongozi wa dini.

Mwili wa aliyekua mkurugenzi wa uzalishaji na vipindi uliwasili siku ya Ijumaa kutoka Afrika Kusini
Maelezo ya picha, Mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ukiwasili Karimjee

Mwili wa Ruge Mutahaba unasafirishwa mpaka mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania kwa ajili ya kuzikwa.

Waombolezaji wakiwa kwenye viwanja wakifuatilia kwenye Skrini kinachojiri ndani ya ukumbi
Maelezo ya picha, Waombolezaji wakiwa kwenye viwanja wakifuatilia kwenye Skrini kinachojiri ndani ya ukumbi

Ilikua siku ya kawaida jua kali likiwaka lakini waombolezaji walionekana kutochoka wakisubiri kutoa salamu za Buriani

Diamond Platnumz alihudhuria halfa ya leo
Maelezo ya picha, Watu mbalimbali maarufu wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho

Ruge Mutahaba atakumbukwa sana kwa mchango wake katika tasnia ya Burudani kwani wasanii wengi wanaofanya vizuri wamepita mikononi mwake ambapo alikuwa akiwajengea uwezo kuvipa uthamani vipaji walivyonavyo.

Peter Msechu na Christian Bella wakiwa jukwaani
Maelezo ya picha, Wanamuziki mbalimbali walitumbuiza wakati wa hafla hiyo

Viongozi, wafanyakazi na wasanii walipata nafasi ya kutoa ushuhuda kuhusu maisha ya Ruge na mchango wake katika nyanja mbalimbali ikiwemo burudani, siasa, uchumi na tasnia ya habari kwa ujumla.

Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Tanzania
Maelezo ya picha, Viongozi mbalimbali walijitokeza kutoa heshima za mwisho