Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais wa Tanzania Dokta John Magufuli aongoza maelfu kumuaga Ruge
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza maelfu ya watanzania kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Mwili wa Ruge umeagwa leo katika uwanja wa Karimjee halfla iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali wakiwemo pia mawaziri,wabunge, wakuu wa wilaya halikadhalika viongozi wa dini.
Mwili wa Ruge Mutahaba unasafirishwa mpaka mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania kwa ajili ya kuzikwa.
Ilikua siku ya kawaida jua kali likiwaka lakini waombolezaji walionekana kutochoka wakisubiri kutoa salamu za Buriani
Ruge Mutahaba atakumbukwa sana kwa mchango wake katika tasnia ya Burudani kwani wasanii wengi wanaofanya vizuri wamepita mikononi mwake ambapo alikuwa akiwajengea uwezo kuvipa uthamani vipaji walivyonavyo.
Viongozi, wafanyakazi na wasanii walipata nafasi ya kutoa ushuhuda kuhusu maisha ya Ruge na mchango wake katika nyanja mbalimbali ikiwemo burudani, siasa, uchumi na tasnia ya habari kwa ujumla.