Vitu saba ambavyo unahitaji kuvisikia kuhusu sauti yako

Chanzo cha picha, Getty Images
Kila mtu anazaliwa na sauti ya kipekee.
Unaweza kuwa mtu ambaye unaongea sana, muimbaji au mcheshi lakini ni kwa kiasi gani unaifahamu sauti yako hiyo ambayo ni nzuri na inayostahajabisha?
Kipindi cha BBC kinachohusu masuala ya sayansi kimeangazia utafiti ambao umefanywa kuhusu udadisi wa sauti na kubaini vitu ambavyo vinashangaza sana.
1. Ulikuwa na lafudhi yako tangu umezaliwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Watoto huwa wanaakisi lafudhi za wazazi wao wakati wakiwa bado tumboni
Watafiti waliwachunguza watoto waliozaliwa Ufaransa na Ujerumani na kubaini kuwa kile kilio ambacho huwa wanakitoa wakati wanazaliwa huwa ndio lugha mama yao.
Wameonyesha pia namna ambavyo inawezekana kujua watoto hawa wametoka mataifa tofauti kwa namna ambavyo wanalia.
2. Je sauti yako ikoje ndani

Chanzo cha picha, Getty Images
Sauti yako inaanzia kutoka ndani, ukiwa unahema taratibu huwa inaendeshwa na sanduku linalohifadhi sauti.
Vipande viwili vya tishu, hutikisika kwa kwenda mbele na kurudi nyuma wakati ambapo hewa inapita mdundo wa sauti unatengenezwa.
Hivyo mdomo, taya, ulimi pamoja na ngozi laini ya nyuma ya koo lako uunda sauti yako.
3. Kwa nini sauti yako inaweza kuongezeka sana

Chanzo cha picha, Getty Images
Sauti ya wanaume waliobalehe , sanduku la sauti ya kiume huwa inatokea chini ya koo na huanza kutoka kama anaunguruma. Sauti hiyo inajulikana kama "Adam's apple".
Utofauti wa umbali kati ya sanduku la sauti na mdomo huwa ni kubwa.
Ndio maana sauti za wanaume huwa ni kubwa.
Wanawake pia huwa wanapitia mfumo wa aina hiyo ingawa kuna utofauti mdogo, mchakato wake unaweza kuwa tofauti wakati wa kumaliza na sauti yao inaweza kuwa chini.
4. Sauti yako inaweza kuwa huru zaidi kwa watu unaowafahamu

Chanzo cha picha, Getty Images
Unapompenda mtu zaidi ndio kunaweza kukufanya uweze kuongeza sauti yako au kutaka sauti yako ifanane kama yao.
Hivyo kama mwanaume anampenda mwanamke basi mara kwa mara ataongeza sauti yake wakati anaongea na mwanamke huyo.
5. Sauti yako inazeeka pia

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtu unapozeeka, huwa inapokea hewa kutoka nje wakati unapoongea hivyo inaifanya sauti yako iwe inasikika kama unahema sana.
Hii inamaanisha kwamba mtu huyo anakuwa hawezi kuongea sentensi ndefu kwa sababu utaishiwa pumzi.
Lakini vilvile sauti inaweza kuwa ya juu wakati wa umri wa uzee.
6. Sauti yako inaweza kubaki kuwa ya kijana kwa muda

Chanzo cha picha, Getty Images
Habari njema ni kuwa ,sauti yako huwa inazeeka taratibu zaidi ya kiungo chochote cha mwili wako.
Kama unataka kukisia umri wa mtu kwa kusikiliza sauti yake ,huwezi kwa sababu utasema watu hao kuwa wadogo zaidi ya umri wao.
7.Ni namna gani unaweza kutunza sauti yako

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni kama ilivyo kwa mwili wako, sauti yako pia inahitaji matunzo hivyo kwa kuimba na kuzungumza na watu kutasaidia kutunza sauti yako.












