Jacinda Ardern: Waziri mkuu wa New Zealand ahudhuria mkutano wa UN na mwanawe mchanga New York Marekani

Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve tangu alipozaliwa Juni 21

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve, tangu alipozaliwa Juni 21
Muda wa kusoma: Dakika 2

Waziri mkuuu wa New Zealand, Jacinda Ardern ametoa hotuba yake ya kwanza katika kongamano la Umoja wa mataifa mjini New York.

Katika tukio ambalo si la kawaida kiongozi huyo aliingia ndani ya chumba cha mkutano wa shirika hilo la kimataifa akiwa na mtoto wake mchanga.

Japo ameandamana na mpenzi wake Clarke Gayford, Bi Ardern amechukua muda kumchezesha mwanawe mchanga kwa jina Neve Te Aroha, kabla ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Kiongozi huyo kwa sasa anamnyonyesha bintiye Neve, ambaye ana miezi mitatu. Huu sio uamuzi wa kawaida kwa mwanamke yeyote, ikizingatiwa kuwa angemuacha nyumbani,

kwa siku sita ili aweze kuhudhuria mkutano huo muhimu wa kimataifa.

Arden ameliambia shirika la habari la New Zealanda kuwa mara nyingi yuko na mtoto wake kiiwa nchini New Zealand.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

''Kwa kweli mwanangu Neve yuko nami kila mahali New Zealand''

Wakati huu anapohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa, Bwana Gayford atakua na jukumu la kumtunza mtoto Neve, kama ilivyoandikwa katika kadi inayotambulisha

rasmi uwepo wa mtoto huyo katika ukumbi wa mkutano.

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern akihutubia mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern akihutubia mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa
Mpenzi wake Clarke Gayford,ambaye ni mtangazaji wa televisheni, kwa sasa anamsaidia jukumu la ulezi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mpenzi wake Clarke Gayford,ambaye ni mtangazaji wa televisheni, kwa sasa anamsaidia jukumu la ulezi

Bi Ardern pia ameliambia gazeti la Herald nchini New Zealand,kuwa atagharamia usafiri na malazi ya mpenzi wake. "Yuko hapa kumtunza mtoto wetu".

Kiongozi huyo amerejea kazini kutoka likizo ya uzazi mapema mwezi Agosti.

Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve tangu alipozaliwa Juni 21

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve, tangu alipozaliwa Juni 21

Msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric, amesema "Waziri mkuu Ardern ni kielelezo chema kwa taifa lake na hatua yake ya kuhudhuria mkutano huu akiwa na mwanawe ni ishara wazi kwamba hakuna mwakilishi bora zaidi kwa nchi kuliko mama mchapa kazi''.

Bwana Dujarric, ameongeza kuwa viongozi wanawake duniani ni 5% kwa hiyo wanahitaji kujisikia huru kadiri ya uwezo wao.