Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jacinda Ardern: Waziri mkuu wa New Zealand ahudhuria mkutano wa UN na mwanawe mchanga New York Marekani
Waziri mkuuu wa New Zealand, Jacinda Ardern ametoa hotuba yake ya kwanza katika kongamano la Umoja wa mataifa mjini New York.
Katika tukio ambalo si la kawaida kiongozi huyo aliingia ndani ya chumba cha mkutano wa shirika hilo la kimataifa akiwa na mtoto wake mchanga.
Japo ameandamana na mpenzi wake Clarke Gayford, Bi Ardern amechukua muda kumchezesha mwanawe mchanga kwa jina Neve Te Aroha, kabla ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa mataifa.
Kiongozi huyo kwa sasa anamnyonyesha bintiye Neve, ambaye ana miezi mitatu. Huu sio uamuzi wa kawaida kwa mwanamke yeyote, ikizingatiwa kuwa angemuacha nyumbani,
kwa siku sita ili aweze kuhudhuria mkutano huo muhimu wa kimataifa.
Arden ameliambia shirika la habari la New Zealanda kuwa mara nyingi yuko na mtoto wake kiiwa nchini New Zealand.
''Kwa kweli mwanangu Neve yuko nami kila mahali New Zealand''
Wakati huu anapohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa, Bwana Gayford atakua na jukumu la kumtunza mtoto Neve, kama ilivyoandikwa katika kadi inayotambulisha
rasmi uwepo wa mtoto huyo katika ukumbi wa mkutano.
Bi Ardern pia ameliambia gazeti la Herald nchini New Zealand,kuwa atagharamia usafiri na malazi ya mpenzi wake. "Yuko hapa kumtunza mtoto wetu".
Kiongozi huyo amerejea kazini kutoka likizo ya uzazi mapema mwezi Agosti.
Msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric, amesema "Waziri mkuu Ardern ni kielelezo chema kwa taifa lake na hatua yake ya kuhudhuria mkutano huu akiwa na mwanawe ni ishara wazi kwamba hakuna mwakilishi bora zaidi kwa nchi kuliko mama mchapa kazi''.
Bwana Dujarric, ameongeza kuwa viongozi wanawake duniani ni 5% kwa hiyo wanahitaji kujisikia huru kadiri ya uwezo wao.