Refilwe Ledabwe: Rubani mwanamke anayewafunza wasichana wa Afrika kuendesha ndege

Paballo au Pabi Leghotsa anatoka katika kiti cha rubani wa ndege ya viti vinne akifurahia

''Ni ajabu. Nilihisi kana kwamba nina udhibiti kamili, unaelewa?'' Anasema,akizunguka kwa furaha. Kuchukua udhibiti wa ndege ni kitu ambacho kijana huyo kutoka mji wa Soweto viungani mwa mji wa Johannesburg , alikuwa na ndoto yake tangu alipokuwa msichana mdogo.

Amesimama katika barabara ya ndege katika uwanja wa ndege wa Grand Central akiwa na furaha isiokuwa na kifani , huku maneno ya furaha yakimtoka

''Kuendesha ndege ya Zulu Sierra Papa Whiskey ilikuwa raha sana . Nilifurahia sana''

Mwanamke aliyesababisha raha hiyo ni Refilwe Ledabwe, mwanamke wa kwanza mweusi kuwahi kuwa rubani kikosicha hudma za polisi Afrika kusini

Pia ni mwanamke wa kwanza mweusi wa taifa hilo kuwa rubani wa ndege aina ya helikopta.Na hiyo haijafika hata nusu ya mafanikio yake.Relifwe ndiye mwanzilishi wa wakfu wa kusawasaidia wasichana wadogo barani afrika kwa jina Girl fly Programme in Afrka GFPA, shirika linalowawezesha vijana wa kike kuchukua masomo ya teknolojia, uhandisi na hesabati shuleni.

Kila mwaka anaandaa , kambi ya mafunzo ya urubani , ambapo hujifunza kuhusu robotiki, maneno ya siri na safari za angani.Na baadaye kila msichana anapata mafunzo ya bure ya kuendesha ndege wakati mmoja wa mwaka.

Akiwa amevalia sare za rubani wa ndege, akiwatazama wasichana hao wakiendesha ndege hizo mmoja baada ya mwengine anasema: 'Nataka wasichana hawa wafanikiwe.sio chaguo la kuwa marubani bali kuwa wasichana wenye ujasiri wa kuweza kutoa mchango wao katika jamii, uchumi na kusadia jamii.'

Hamu yake yake ya kuwa rubani ni kuwafunza wengine na ni maono hayo ambayo yanamshinikiza kutaka kuafikia ndoto yake ya kutaka kuendeleza vizazi vijavyo vya kike nchini Afrika kusini kuwa wataalam wa angani, na viongozi wa sayansi katika siku zijazo barani Afrika

Akisimama katika barabara ya ndege, marubani wengine wanasimama na kumuita jina lake , wakimpungia mkono ,kumsumbua na kumuomba ushauri kuhusu maswala kadhaa ya usafiri wa angani.

Anatabasamu akijibu maswali yao mbali na kuendelea kupanga kambi ya mafunzi ya takriban wasichana 100 walio kati ya mrui wa miaka 14 hadi 18 kutoka Afrika kusini na botswana katika eneo lenye milima la Magaliesburg.

Refilwe ambaye alikulia katika nyumba yenye mzazi mmoja na ndugu sita mjini Limpopo, hakuweza kuwa karibu na ndege hadi alipofikia umri wa miaka 17

Alikuwa na ndoto ya kuwa daktari hadi wakati alipokuwa chuo kikuu alipopanda ndege kuelekea Johanesburg kutoka Cape Town na kugundua kwamba ndege hiyo ilikuwa ikiendeshwa na rubani mwanamke.

Ndoto yake iliendelea hadi alipoanza kufanya kazi kama mfanyikazi wa ndege wa shirika la ndege la Afrika kusini.Alianza kuchukua mafunzo ya kuendesha ndege ya kibinafsi Lakini baada ya muda mfupi akagundua kwamba alihitaji njia nyengine ya kutafuta fedha.

Niliandika takriban barua 200 kwa kila kampuni iliokuja akiliini mwangu nchini Afrika kusini,alisema. Kampuni tatu zilijibu ikiwemo huduma ya polisi ya Afrika Kusini ambao waliamua kunilipia mafunzo ya kuendesha ndege aina ya helikopta na kumsaidia kupata leseni ya rubani wa ndege za biashara.

Refilwe amewacha kazi ya polisi na sasa anatumia muda wake mwingi kuwa mwalimu, huku akilenga kuwatafuta wasichana walio na hamu ya kuingia katika sekta ya usafiri wa ndege.

Saa mbili kaskazini mwa Johannesubrg, katika milima iliojaa vumbi, wasichana wanaanza kuwasili katika kambi ya mafunzi ya urubani ya Refilwe ambayo ndio ya nne na kubwa zaidi kufikia sasa

Wao ni wasomi katika sekta zao, wote wakijipata alama za juu katika masomo ya hesabu na sayansi. Hatahivyo hapa ndipo ambapo tofauti yao inaishia

Hawana ni wasichana kutoka vijijini, wasichana kutoka shule kuu za kibinafsi na wasichana ambao hawajapata rafiki mweusi ama mweupe hapo nyuma kutokana na jamii zilizogawanyika

Siku za kambi hiyo zimejaa mashine za kufunza kuendesha ndege, utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki na maswali yanarushiwa wageni wahamasishaji walioalikwa. Nyakati za usiku za kambi hiyo zimejaa nyimbo, densi moto uliowashwa kutoa baridi na kujenga urafiki

Profesa Debra Meyer, muhadhiri mkuu wa kitivo cha sayansi katika chuo kikuu cha Johannesburg anasema kuwa ni muhimu kwa wanafunzi kukuwekeza katika masomo ya sayansi, teknolojia, Uhandisi na hasa barani Afrika hususan wanafunzi wa kike.

"Ni muhimu kuwahimiza wasichana wadogo kufanya masomo ya sayansi na teknolojia lakini pia kuendelea na masomo hayo. Hatuoni wasichana wa kutosha wakifanikiwa katika masomo ya sayansi na hilo linafaa kubadilika

"Wanawake weusi hubaguliwa na ikiwa ni wachache waliopo katika sekta hii, tunahitaji kuwahimiza wasichana zaidi kuwasilisha maombi na kuwasaidia kupata ufanisi", anasema.

Matamshi hayo yanaungwa mkono na rubani Sakhile Nyoni-Reiling, mwanamke wa kwanza kuwa rubani nchini Botswana ambaye ameshikilia nyadhfa za juu katika shirika la ndege la Botswana Air na sekta ya usafiri wa ndege ya Afrika Kusini.

Anasema kuwa sekta ya usafiri wa ndege ilikuwa sekta ambayo wasichana walikuwa hawasikiki, akiongezea ni muhimu kwamba wasichana katika kambi hiyo walipata mafunzo ya kupambana na hali ngumu iliopo mbele yao.

Maandalizi

Deta iliyokusanywa na shirika la marubani wanawake inaonyesha kuwa ni asilimia 5 pekee ya wanawake dunia ni marubani.

Na ijapokuwa Refilwe ni mfano mzuri kwa wasichana hao, anamsifu mamake kuwa kiungo kikuu cha ufanisi wake.

Lakini ni nini haswa kinachomfanya kuendelea?

''Wanawake ni asilimia 50 ya idadi ya watu duniani. Iwapo hutawaandaa wanawake kwa kazi kama hizo katika siku za usoni basi tumepotea''.

"Ni muhimu kwamba hatuangazii usafiri wa ngani pekee bali masomo ya STEM kwa jumla kwa sababu hatua hiyo itawafanya wasichana kujimudu katika kupigania kazi za siku zijazo.pengine watarudi na kuzisaidia jamii zao kukabiliana na tatizo la umasikini

"Katika siku za usoni pengo lililopo kuhusu ukosefu wa usawa wa kijinsia pengine litapungua kiasi.

"Hiyo ndio sababu tunafanya tunachokifanya".

Kipindi hiki kiliandaliwa kupitia wakfu wa Bill & Melinda Gates