Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bobi Wine: ''Utawala hauamini kuwa mtu anaweza kuzungumza na watu bila kuwarushia pesa''
Mwanamuziki na mbunge nchini Uganda, Bobi Wine amemkejeli rais Yoweri Museveni, kwa kutoa mchango wa dola 26,000 kwa vijana katika eneo bunge lake mjini Kampala.
Kwa mujibu wa ripoti katika televisheni ya NTV Uganda, Bobi Wine amesema ''Kwa kuwa serikali haina la kuwaambia watu, sasa imegeukia kuwanunua-wakiona hamtishwi na risasi wanawarushia pesa''
Bobi pia amesema kuwa ''Utawala hauamini kuwa mtu anaweza kuzungumza na watu bila kuwarushia pesa''
Mwanasiasa huyo anadai kuwa serikali ilijaribu kuipatia pesa familia ya dereva wake aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agost 13.
Gazeti la Daily Monitor pia limeangazia madai hayo likisema familia ya dereva huyo aliyeuawa ilikataa kupokea pesa hizo.
Bobi Wine pia alidai kuwa ni yeye aliyekuwa analengwa katika kisa cha kupigwa risasi na kuuawa kwa dereva wake
Bobi Wine, ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na kupigwa mawe msafara wa Rais Yoweri Meseveni wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo.