Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Luka Modric ateuliwa mchezaji bora wa kiume Fifa, Deschamps kocha bora
Kiungo wa kimataifa wa Croatia Madrid Luka Modric,ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Fifa wa kiume katika shughuli ya utoaji tuzo iliyofanyika usiku huu London Uingereza.
Modric mwenye miaka 33, amewapiga kumbo mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, anayechezea Juventus, kwa sasa pamoja na winga wa Liverpool Mohamed Salah.
Kwa upande wa wanawake mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Orlando Pride, Marta Vieira a Silva, ndie aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Fifa na kuwa ni tuzo yake wa sita ya uchezaji bora akiwazidi Dzsenifer Marozsan na Ada Hegerberg.
Kocha wa mabingwa wa kandanda duniani Ufarasansa Didier Deschamps ameibuka kidedea kuwa ndie kocha bora na kuwapiku Zinedine Zidane na kocha wa timu ya taifa ya Croatia Zlatko Dalic
Mohamed Salah ametwa tuzo ya goli bora(Puskas) goli ambalo alilifungwa dhidi ya Everton mwezi Desemba.Kipa wa zamani wa Chelsea Thibaut Courtois ametajwa kuwa ndie kipa bora .
Pia katika tuzo hizo kulitangazwa kikosi cha wachezaji kumi na moja wa dunia wa Fifa