Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Chelsea itafanikiwa kumsajili mlinzi huyu wa Ufaransa?

Muda wa kusoma: Dakika 3

Klabu ya Chelsea iko tayari kulipa euro 50m (£43.3m) kwa mlinzi wa Ufaransa Jeremy Jacquet, 20, lakini Rennes wanataka zaidi ya euro 60m (£52m). (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Napoli huenda ikamsajili mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 21, ambaye yuko Roma kwa mkopo kutoka Brighton, ikiwa winga wa Uholanzi Noa Lang, 26, ataondoka mwezi huu. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Uongozi wa Tottenham unatarajiwa kukutana leo Jumapili kujadili mustakabali wa meneja Thomas Frank baada ya klabu hiyo kushindwa Jumamosi dhidi ya West Ham.(Independent)

Bournemouth inajadiliana na klabu ya Lazio kuhusu mkataba wa mkopo kwa kipa wa Ugiriki Christos Mandas, 24. (Sky Sports)

Newcastle imewasilisha dau la kumsajili mlinzi wa Uholanzi na Inter Milan Stefan de Vrij, 33. (Football Insider)

Aston Villa imefanya mazungumzo na Club Brugge kuhusu usajili wa Raphael Onyedika, 24, lakini Galatasaray inaongoza mbio za kumsajili kiungo huyo wa Nigeria. (Sacha Tavolieri),

Arsenal wanamuwania mchezaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22 na beki wa Eintracht Frankfurt Nathaniel Brown na kiungo wa kati wa Sporting wa Ivory Coast Ousmane Diomande, 22. (Caught offside).

Liverpool imeelekeza darubini yake kwa mlinzi wa Inter Milan na Italia Alessandro Bastoni, 26, baada ya kumkosa Marc Guehi wa Crystal Palace ambaye anakaribia kujiunga na Manchester City. (Team talk)

Juventus imeongeza juhudi za kumsajili Jean-Philippe Mateta wa Crystal Palace, 28, na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji huyo wa Ufaransa siku ya Ijumaa. (Mail)

Aston Villa, Tottenham na Manchester United zinapigana vikumbu kwa beki wa Juventus Pierre Kalulu, 25, lakinimchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa hatatolewa hadi mwisho wa msimu huu. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Manchester Unitedinataka kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 28, majira ya baridi lakini Al-Hilal inataka ada ya pauni milioni 20. (Football Insider)

Liverpool wameelekeza macho yao kwa kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga, 23. (Fichajes - kwa Kihispania)

West Ham imefanya mazungumzo na klabu ya Barcelona kuhusu uwezekano wa kumsajili Marc-Andre ter Stegen, 33, lakini kipa huyo wa Ujerumani anaonekana kujiandaa kujiunga na Girona. (Team talk)

Tottenham inachuana na Aston Villa na Newcastle kumsajili mshambuliaji wa Brentford na Ujerumani Kevin Schade, 24. (Caught Offside)

Chelsea inajiandaa kumrudisha David Datro Fofana, 23, anayelengwa na Celtic, kutoka k klabu ya Uturuki Fatih Karagumruk ambako amekuwa akikipiga kwa mkopo huku wakitarajia kumuuza mshambuliaji huyo wa Ivory Coast mwezi huu. (Football Insider)