Luka Modric ateuliwa mchezaji bora wa kiume Fifa, Deschamps kocha bora

Luka Modric mchezaji bora wa Fifa

Chanzo cha picha, Fifa/getty image

Maelezo ya picha, Luka Modric mchezaji bora wa Fifa

Kiungo wa kimataifa wa Croatia Madrid Luka Modric,ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Fifa wa kiume katika shughuli ya utoaji tuzo iliyofanyika usiku huu London Uingereza.

Modric mwenye miaka 33, amewapiga kumbo mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, anayechezea Juventus, kwa sasa pamoja na winga wa Liverpool Mohamed Salah.

Marta Vieira da Silva, ametwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara sita

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marta Vieira da Silva, ametwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara sita

Kwa upande wa wanawake mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Orlando Pride, Marta Vieira a Silva, ndie aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Fifa na kuwa ni tuzo yake wa sita ya uchezaji bora akiwazidi Dzsenifer Marozsan na Ada Hegerberg.

Kocha wa mabingwa wa kandanda duniani Ufarasansa Didier Deschamps ameibuka kidedea kuwa ndie kocha bora na kuwapiku Zinedine Zidane na kocha wa timu ya taifa ya Croatia Zlatko Dalic

Didier Deschamps ametwaa tuzo ya kocha bora

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Didier Deschamps ametwaa tuzo ya kocha bora

Mohamed Salah ametwa tuzo ya goli bora(Puskas) goli ambalo alilifungwa dhidi ya Everton mwezi Desemba.Kipa wa zamani wa Chelsea Thibaut Courtois ametajwa kuwa ndie kipa bora .

Pia katika tuzo hizo kulitangazwa kikosi cha wachezaji kumi na moja wa dunia wa Fifa

Nyota kumi na moja wa kikosi cha dunia

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Kikosi cha nyota kumi na moja wa kikosi cha dunia