Soko la Gikomba Kenya: Watu 15 wafariki katika moto

Uharibifu katika soko la GIkomba kutokana na mkasa wa moto leo
Maelezo ya picha, Uharibifu katika soko la Gikomba kutokana na mkasa wa moto leo
Muda wa kusoma: Dakika 2

Takriban watu 15 wamefariki katika moto mkubwa uliokumba soko moja katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Zaidi ya watu 70 walijeruhiwa katika moto huo uliotokea katikati ya usiku na kusababisha uhuribifu wa mali nyingi.

Soko hilo la Gikomba ndio soko kubwa zaidi katika mji huo na moto hutokea mara kwa mara swala linalosababisha uvumi kwamba huenda kuna watu wanaochoma soko hilo, kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya.

Gikomba moto
Baadhi ya wafanyikazi wa soko hilo walioamkia mkasa huo
Maelezo ya picha, Baadhi ya wafanyikazi wa soko hilo walioamkia mkasa huo

Hatahivyo chanzo cha moto huo bado hakijulikani.

Huduma ya ambalensi ya St John inasema kuwa moto huo ulianza saa nane za usiku Alhamisi afajiri kabla ya kuenea katika nyumba zilizopo karibu na vibanda vya soko hilo kabla ya kudhibitiwa baada ya dakika 90.

Soko la Gikomba jijini Nairobi
Maelezo ya picha, Afisa wa polisi akiweka doria ili kulinda baadhi ya mali zilizookolewa kufuatia moto mkubwa katika soko la Gikomba

Baadhi ya waathiriwa walichomwa huku wengine wakivuta moshi wenye sumu walipojaribu kuokoa mali yao.

Maafisa wa hospitalini wanasema kulikuwa na watoto watano miongoni mwa waliofariki.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Picha kutoka shirika la habari la Reuters ziliwaonyesha watu wakitafuta mali yao katika na jivu.

Gikomba
Maelezo ya picha, Baadhi ya mali iliookolewa katika soko la Gikomba

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali tofauti mjini humo. Soko hilpo ni maarufu sana kwa uuzaji wa nguo za mitumba , viatu na mboga, na pia lina maeneo ya kuweka mbao ambayo yaliharibika katika moto huo.

Soko hilo ni maarufu kwa uuuzaji wa nguo za mitumba viatu na hata mboga, na kuna maeneo ya kuuzia mbao ambayo yameharibiwa kupita kiasi katika moto huo.

Inaarifiwa huend amoto huo umetoka katika maeneo hayo ya kuuza mbao.