Soko la Gikomba Kenya: Watu 15 wafariki katika moto

Muda wa kusoma: Dakika 2

Takriban watu 15 wamefariki katika moto mkubwa uliokumba soko moja katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Zaidi ya watu 70 walijeruhiwa katika moto huo uliotokea katikati ya usiku na kusababisha uhuribifu wa mali nyingi.

Soko hilo la Gikomba ndio soko kubwa zaidi katika mji huo na moto hutokea mara kwa mara swala linalosababisha uvumi kwamba huenda kuna watu wanaochoma soko hilo, kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya.

Hatahivyo chanzo cha moto huo bado hakijulikani.

Huduma ya ambalensi ya St John inasema kuwa moto huo ulianza saa nane za usiku Alhamisi afajiri kabla ya kuenea katika nyumba zilizopo karibu na vibanda vya soko hilo kabla ya kudhibitiwa baada ya dakika 90.

Baadhi ya waathiriwa walichomwa huku wengine wakivuta moshi wenye sumu walipojaribu kuokoa mali yao.

Maafisa wa hospitalini wanasema kulikuwa na watoto watano miongoni mwa waliofariki.

Picha kutoka shirika la habari la Reuters ziliwaonyesha watu wakitafuta mali yao katika na jivu.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali tofauti mjini humo. Soko hilpo ni maarufu sana kwa uuzaji wa nguo za mitumba , viatu na mboga, na pia lina maeneo ya kuweka mbao ambayo yaliharibika katika moto huo.

Soko hilo ni maarufu kwa uuuzaji wa nguo za mitumba viatu na hata mboga, na kuna maeneo ya kuuzia mbao ambayo yameharibiwa kupita kiasi katika moto huo.

Inaarifiwa huend amoto huo umetoka katika maeneo hayo ya kuuza mbao.