Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Moto wateketeza soko la Gikomba, Kenya
Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa imeteketea baada ya moto kuzuka katika soko kuu la wazi nchini kenya, soko la Gikomba jijini Nairobi.
Moto huo ulizuka mwendo wa saa tisa usiku.
Ijumaa asubuhi, baada ya moto huo uliowaka kwa saa kadha kuzimwa, wachuuzi walikuwa wakichakura kutafuta bidhaa ambazo hazikuungua moto.
Soko la Gikomba ni miongoni mwa masoko makubwa zaidi Afrika Mashariki.
Wengi wa wachuuzi huuza nguo na bidhaa nyingine za mitumba.
Mmoja wa wachuuzi amemwambia mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi kwamba amepoteza marobota 250 ya nguo ya thamani ya karibu dola 23,000 za Marekani (Ksh2.3m).
Chanzo cha moto huo bado hakijabainika.