Msichana aliyevaa hijab ashambuliwa na mtu aliyetaka kukata vazi hilo Canada

Chanzo cha picha, Reuters
Polisi nchini Canada wanachunguza shambulizi dhidi ya msichana mwenye umri wa miaka 11 wa kiislamu, baada ya mwanamme mmoja kudaiwa kwamba alijaribu mara kadhaa kukata kwa makasi vazi lake la hijab.
Msichana huyo kwa jina Khawlah Noman anasema alikuwa akielekea shule na nduguye wakati mwananmume huyo alipomvizia .
Bi Norman anasema alipiga mayowe mara ya kwanza kabla ya mwanamume huyo kutoroka ijapokuwa baadaye alirejea, akamvua kofia yake na kukata hijab aliyokuwa amevalia
Maafisa wa polisi wanasema mwanamume huyo ana asili ya bara Asia.
Wanasema kuna uwezekano shambulizi hilo likawa la chuki.
Shambulizi hilo limeshtumiwa na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau.








