Marekani yaweza kukubaliana na makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi

Raisi wa marekani Donald trump

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Raisi wa marekani Donald trump

Raisi wa marekani Donald trump amesema kuwa Marekani inaweza kurudi katika makubaliano ya mabadiliko ya tabia nchi ya paris , kama makubaliano hayo yatakua na faida kwa marekani,.

Juni mwaka jana Trump alijitoa katika makubaliano hayo kwa madai kuwa makubaliano hayo yangegharimu marekani zaidi ya ajira milioni sita, huku nchi kama China na India zikiwa na ahueni.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri mkuu wa Norway , Trump amesema kuwa uongozi uliopita uliingia katika makubalioano ambayo yaliiweka marekani katika hasara ya kibiashara.

''ni makubliano ambayo mimi sina tatizo nayo lakini, nina tatizo na makubaliano ambayo yaliingiwa katika uongozi uliopita na kama kawaida walifanya maamuzi mabaya. Lakini tunaweza kuingia tena lakini tuu kama kutakua na maslahi ya marekani, na pia sio suala la mazingira tuu , tunataka biashara inayoweza kuwa na ushindani ,na ule kataba kwakweli ungeondoa ushindani wetu wa biashara, na hatuwezi kukubali suala hilo kutokea''Trump

Na kuongeza kuwa mwaka jana Marekani walishiriki katika mkutano wa makubaliano hayo kama waangalizi tuu ambapo mawaziri wan chi 30 walijadili masuala ya makubaliano hayo ya mabadiliko ya tabia nchi ya paris.

change

Chanzo cha picha, AFP

Kujiondoa kwa marekani kunaifanya kuwa nchi pekee ambayo haitahsiriki katika makubaliano hayo, jambo lilosababisha hasira miongoni mwa wamarekani na jamii ya kimataifa.

Marekani inachangia asilimia 15 ya uzalishaji kimataifa wa kaboni, lakini pia ni chanzo muhimu cha fedha na teknolojia kwa ajili ya nchi zinazoendelea katika juhudi zao za kupambana na ongezeko la joto.