Kikosi chabuniwa kupambana na moshi mchafu Beijing

Maafisa wanasema wanatafuta njia za kupunga uchafuzi wa hewa kwenye mij mingi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maafisa wanasema wanatafuta njia za kupunga uchafuzi wa hewa kwenye mij mingi

Kikosi kipya cha kushughulikia masuala ya mazingira kinatarajiwa kupunguza viwango vya moshi mchafu unaotaka kweny mji wa Beijing nchini China.

Polisi hao watakuwa wakitafuta vyanzo vya moshi huo yakiwemo maeneo ya nje ya kuchomea nyama na barabara zenye vumbi, kwa mujibu wa meya wa mji huo Cai Oi.

Meya pia ameahidi kupunguza matumizi ya makaa ya mawe kwa asilimia 30.

Wakaazi wengi wa mji wa Beijing wamelazimika kubaki manyumbani mwao kwa siku kadha ili kuzuia kupumua moshi huo mchafu.

Watu wamekuwa wakitoa wito kwa serikali kufanya jitihada zaidi kupunguza moshi huo, ikiwemo kupunguza viwanda vinavyotegemea nishati ya mkaa wa mawe.

Watu wamekuwa wakijifunika ili kuzuia kupumua moshi huo mchafu

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Watu wamekuwa wakijifunika ili kuzuia kupumua moshi huo mchafu