Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kikosi chabuniwa kupambana na moshi mchafu Beijing
Kikosi kipya cha kushughulikia masuala ya mazingira kinatarajiwa kupunguza viwango vya moshi mchafu unaotaka kweny mji wa Beijing nchini China.
Polisi hao watakuwa wakitafuta vyanzo vya moshi huo yakiwemo maeneo ya nje ya kuchomea nyama na barabara zenye vumbi, kwa mujibu wa meya wa mji huo Cai Oi.
Meya pia ameahidi kupunguza matumizi ya makaa ya mawe kwa asilimia 30.
Wakaazi wengi wa mji wa Beijing wamelazimika kubaki manyumbani mwao kwa siku kadha ili kuzuia kupumua moshi huo mchafu.
Watu wamekuwa wakitoa wito kwa serikali kufanya jitihada zaidi kupunguza moshi huo, ikiwemo kupunguza viwanda vinavyotegemea nishati ya mkaa wa mawe.