Ban Ki-moon kugombea urais Korea Kusini

Muhula wa Ban Ki-moon unakamilika mwisho wa mwezi huu

Chanzo cha picha, AFP PHOTO /UNITED NATIONS/ ESKINDER DEBEBE

Maelezo ya picha, Muhula wa Ban Ki-moon unakamilika mwisho wa mwezi huu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amedokeza kuwa huenda akawania urais nchini mwake, Korea Kusini.

Muhula wake Ban kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa unakamilika mwisho wa mwezi huu wa Disemba

Wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari, Ban alisema kuwa baada ya kupata mapumziko anarudi nchini mwake Korea Kusini kuona vile ataisaidia nchi yake.

Uchaguzi wa uraia nchini Korea Kusini unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka 2017

Lakini huenda uchaguzi huo ukafanyika katika muda wa miezi miwili baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura ya kumuondoa madarakani Rais Park Geun-hye, kutokana na sakata, ambapo analaumiwa kwa kumruhusu rafiki wake wa karibu kunufaika kifedha.

Ikiwa mahakama ya katiba itadumisha kura hiyo ya kumuondoa, atakuwa rais wa kwanza wa Korea Kusini aliye madarakani kuondelwa katika kipindi cha uhuru wa nchi hiyo.

Mahakama ya katiba ina siku 180 kutoa uamuzi wa mwisho.

Matamshi ya Ban yanakuja huku yakishuhudiwa maandamano kwenye mji mkuu wa Korea Kusini, Seol.

Waandamanaji wanamtaka Bi Park kuondoka madarakani mara moja

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waandamanaji wanamtaka Bi Park kuondoka madarakani mara moja
Maelfu wamejiunga kwenye maandamano ya kumpinga rais Park Geun-Hye siku za hivi karibuni

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Maelfu wamejiunga kwenye maandamano ya kumpinga rais Park Geun-Hye siku za hivi karibuni