Mabadiliko ya katiba yaungwa mkono na wananchi wengi Ivory Coast

Rais Alassane Ouattara amekuwa madarakani tokea mwaka 2010
Maelezo ya picha, Rais Alassane Ouattara amekuwa madarakani tokea mwaka 2010

Mamlaka nchini Ivory Coast inasema kwamba mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa na Rais Alassane Ouattara yamepata uungwaji mkono mkubwa katika kura ya maoni siku ya jumapili.

Maafisa wanasema kuwa asilimia 93 ya wapiga kura wote waliunga mkono hatua hiyo.

Wameongeza kuwa asilimia 42 ya wapiga kura halali hawakupiga kura zao.

Mabadiliko hayo yatawahusu pia machifu wa kimila na nafasi zao serikalini
Maelezo ya picha, Mabadiliko hayo yatawahusu pia machifu wa kimila na nafasi zao serikalini

Upinzani ambao imeitisha mgomo unasema idadi ya wapigakura haikuwa zaidi ya asilimia saba.

Maboresho hayo ya katiba yataruhusu mkuu wa nchi kuteua theluthi moja ya wajumbe wakuu na kupunguza vipengele vyenye vikwazo kuhusu wagombea wa nafasi ya urais.