Afghanistan: Wafungwa 100 waliokuwa wakishikiliwa na Taleban waokolewa

Waliookolewa ni pamoja na maafisa usalama wa nchi hiyo
Maelezo ya picha, Waliookolewa ni pamoja na maafisa usalama wa nchi hiyo

Maofisa katika jimbo la Helmand kusini mwa Afghanistan wanasema vikosi maalum vya nchi hiyo vimewaokoa wafungwa mia na moja amabo walikuwa wakishikiliwa na kundi la wapiganaji la Taliban.

Watu waliookolewa ni pamoja na maofisa usalama wa nchi hiyo.

Msemaji wa kundi la Taliban alikataa kusema chochote kuhusu tukio hilo.

Hii ni awamu ya mwisho katika muendelezo wa uokoaji wa wafungwa katika jimbo la Helmand.

Msemaji wa kundi la Taliban alikataa kusema chochote kuhusu tukio hilo
Maelezo ya picha, Msemaji wa kundi la Taliban alikataa kusema chochote kuhusu tukio hilo

Helmand ndio eneo linalokithiri kwa mapigano baina ya Taliban na vikosi vya serikali wakiwania kuthibiti maeneo muhimu ya jimbo hilo.