Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afghanistan: Wafungwa 100 waliokuwa wakishikiliwa na Taleban waokolewa
Maofisa katika jimbo la Helmand kusini mwa Afghanistan wanasema vikosi maalum vya nchi hiyo vimewaokoa wafungwa mia na moja amabo walikuwa wakishikiliwa na kundi la wapiganaji la Taliban.
Watu waliookolewa ni pamoja na maofisa usalama wa nchi hiyo.
Msemaji wa kundi la Taliban alikataa kusema chochote kuhusu tukio hilo.
Hii ni awamu ya mwisho katika muendelezo wa uokoaji wa wafungwa katika jimbo la Helmand.
Helmand ndio eneo linalokithiri kwa mapigano baina ya Taliban na vikosi vya serikali wakiwania kuthibiti maeneo muhimu ya jimbo hilo.